On Star TV: Chaguzi ndani ya vyama vya siasa - Nafasi ya vijana kuelekea 2015

Status
Not open for further replies.
Mada inawahusu vijana lakini kuna mgeni mzee wa miaka 51! Kwa ushauri sawa lakini kwamba na yeye ni kijana hapana!
 
Kuna ongezeko kubwa sana la vijana wanaojihusisha na siasa hivi sasa, lakini mabadiliko katika nchi na madogo au hayapo kabisa, siasa sasa imekua deal, dhamira ya vijana wengi wanaowania nafasi za kisiasa imekua kupiga deal, kupata black passport, kupata allowances zisizo na msingi na kupata mishahara ya kibunge

Nilitegemea kwa ongezeko hili la vijana lingekuja na vuguvugu la mabadiliko ya namna tunaweka vipaumbele vya taifa na namna tunasimamia rasilimali za nchi, lakini sioni hichi kama kinatokea
 
Kwa Kafulila, amekuwa akionesha upeo mkubwa sana katika masuala mbalimbali lakin hata hivo ameonesha si mvumilivu na ni mwenye ubinafsi. Ni nini nafasi yake katika siasa za Tanzania baada ya 2015
 
Vijana wa CHADEMA ndio wameonyesha kukomaa sana tofauti na wengine. Sijui hao jamaa hapo bungeni wansemaje kuhusu vyama vyao.

Je, vinakosa nini hadi kufanya vijana wa vyama vingine?
 
David Kafulila anasema siku hizi watoto wanachelewa shule wanaachwa tu wakati enzi zao ukichelewa shule unachapwa ndio maana wao (wakina Kafulila) wamekuwa na nidhamu, wakati anasema hayo yeye mwenyewe Kafulila kachelewa sana kufika studio kwenye kipindi cha leo...

Hawa ndio wanasiasa vijana!
 
Mmesikia majibu ya le MUTUZ kuhusu JF
Hahaha, tumemsikia. Hata kuongelea inakuwa haipendezi hahaha,,, JF inamilikiwa na kampuni hii:

attachment.php


Ana shares kampuni ya Palvos Group?

William kwa pumba nimemnyooshea mikono.

Msamehe, ndo siasa
 
Hivi mkuu kauli hii ya William kuwa tofauti ya kiitikadi kati yake na wamiliki wenzake ndiyo sababu ya yeye kujitoa JF huwa mnaielewaje?
Wamiliki wenzake wepi? Details za Palvos Group ukizisoma zina Directors WAWILI TU. Sasa kujibizana na mwanasiasa kwa mambo yasiyo ya kisiasa ni kuingia kwenye mtego uleule. Sidhani kila jambo linahitaji propaganda au kuingiza siasa.

Kwamba yeye ni mwanachama wa mwanzo kabisa JF? Hapana, amejisajili akiwa mwanachama #171 (see www.jamiiforums.com/member.php?u=171 ) hivyo hata katika 1st 100 waliojisajili JF wakati inaanzishwa hayumo. Mtu kama Nicholas ni mtu ambaye amejisajili JF kabla ya FMES, na yumo JF tangu enzi hizo, huyu Nicholas amejisajili akiwa mwanachama #51 (See www.jamiiforums.com/member.php?u=51 )

JF si Jukwaa la Siasa pekee, JF ni zaidi ya siasa. Kama ulifuatilia Interview utakuwa uliona niliyoyaongelea kwa ujumla - https://www.jamiiforums.com/great-t...ew-with-jamiiforums-founder-maxence-melo.html
 
Last edited:
Wamaanisha William sio?

Nadhani William, hayupo hapo kama kijana, pitia vizuri thread ya Yahya utaona William kaletwa kwa lengo kujibu mengi ambayo hayajapata majibu hapa JF sio kama kijana..

Mkuu ni kweli mna bifu na William naona anaongea maneno mengi sana hewani.
 
Ndugu Yahya, William kasema kakimbwizwa JF na tofauti ya itikadi kati yake na waliokuwa wenzie. Je, ni itikadi gani hizo ili na wanaJF na wananchi wengine tujue ili nasi inatubidi tujitoe ama la au tujiweke sawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom