Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,571
.Let me ask you.. nyumba aliyokuwa anapangiwa kwa karibu dola elfu nane (nusu ya mshahara wake) ilikuwa ni ya kimaskini kiasi gani? Je kuna nyumba yoyote ya "maana" kwenye Jiji la Dar ambayo mtu anaweza kupanga kwa dola 3000 hadi 5000? Je nyumba yake aliyokuwa anaishi yeye mwenyewe siyo ya "hadhi yake" (ukisema hapa tunauliza kwanini aliijenga sasa!?)
Hivi unaamini ingekuwa ni fedha zake mwenyewe (kutoka mfukoni) angetumia kujenga nyumba ya kiasi hicho inayogharimu mamilioni mengine kila mwizi kuihudumia? Kama hamuamini na mnaona anaistahili, muuzieni na muulize kama atakuwa tayari kuinunua iwe yake; mwambie agharimie malipo yote kwa vile anaistahili!
Mzee Mwanakijiji, nyumba ya 1.4 Biliion ni nyumba ya Gavana, siyo nyumba ya Ndulu. Kila kitu kilipangwa kabla ya ujio wake.
Nyumba anayokaa ni nyumba ya Benno Ndulu siyo ya gavana, sasa maadam imetokea gavana ndie Benno Ndulu, mwache akae nyumba ya stahiki yake.
Kwa walio dar, si mnapajua pale kwa JK, piteni muune, nini bilioni 1.4!, majirani wamehamishwa hekalu linateremka, si JK yule yule aliyeishi hapo miaka yote?, why now?.
Kama kuna nyumba za mpaka bilioni 10 ila kwa vile ni za wahindi, hao hao wanaoendesha serikali kwa remote, hizo ni hizo hizo top up za rada, gulf stream etc, hatusemi, lakini akijengewa mwenzetu!.
Mtu wa kwanza kuendesha Ferari bongo Bongo ni mhindi, wa pili mwarabu, mswahili bado sijaona na akitokea ataitwa fisadi.
Nasisitiza siungi mkono matumizi yoyote mabaya ya fedha za umma, bali siungi mkono shutuma kwa matumizi yanayoonekana, japo mabaya, huku tuko kimya kwa mabilioni na mabilioni yanatumiwa kwa vitu visivyoonekana.
Pale kwa gavana, si angalau jengo lipo, nimewaambia kila safari moja ya mkulu, zinatumika zaidi ya hizo, kipi kinaonekana?.
Tumemlipa Prof. De Sotto, consultancy ya Dola, 1,000,000 kwa siku moja iliyokuja nchini, tunawalipa wangapi kwa huduma kama hiza and what do we get there after? Si afadhali hapo jengo la hadhi ya gavana lipo?.