Kwa madhumuni ya kuweka sawa rekodi alichosema Waziri Kombani ni kuwa Katiba ya 1977ni Katiba ya tano(ingawa wanazuoni wengine wanasema ni ya nne). Kwa faida ya wenzangu naomba nizitaje:Wanabodi,
Leo ndio mara yangu ya kwanza kumuona Waziri wetu wa Sheria, Mhe. Selina Kombani akihojiwa live kwenye kipindi cha Jambo, kinachorushwa na TBC-1 asubuhi hii.
Alipokuwa akitetea mamlaka kubwa za rais kwenye utungaji wa katiba, Mhe. Kombani amesema, Tangu kutungwa kwa katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, Tanzania tumekuwa na katiba nyingine5 ambazo zote process ndio hiyo hiyo kwa rais kuwa na mamlaka kubwa hivyo na zote zimesainiwa na rais, kitu ambacho sio kweli.
Mhe. Kombani wakati akizungunzia katiba hizo tano, alimaanisha marekebisho ya matano ya katiba, yaliyofanywa kwenye katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, na sio katiba tano kama alivyoeleza Mhe. Waziri.
Usahihi ni kuwa Ile katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ndio hiyo katiba katiba iliyopo mpaka sasa, licha ya kufanyiwa marekebisho mara 5, marekebisho hayo hayabadilishi katiba na kuwa na katiba tano, katiba inabaki ni ile ile moja ya Mwaka 1977!.
Mhe. Kombani, hakuishia hapo, katika utetezi wake kwa mamlaka ya rais pale aliposema, katiba hizo zote 5, zimesainiwa na rais, kitu ambacho pia sio kweli. Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ilitokana na Bunge la Katiba 'Constituent Assembly' (Japo ni Bunge lile lile la chama kimoja lilijigeuza), ambalo ndilo liliipitisha katiba. Katiba ikishapitishwa na Bunge la Katiba, haisainiwi na rais, rais mwenyewe, anapata mamlaka toka kwenye katiba hiyo, ila kinachosainiwa na rais, ni yale marekebisho ya katiba.
Hivyo mpaka ninapoandika hapa, Waziri wetu wa Sheria, anaamini yuko right kabisa kutoa mamlaka kubwa zile kwa rais katika marekebisho ya katiba, kwa vile anaamini kinachofanyika sasa, ni marekebisho mengine ya katiba ile ile ya Tanzania ya Mwaka 1977 na sio process ya Uuundwaji wa katiba mpya.
Waziri wa Sheria, anajua kuwa ni rais ndiye ameisaini Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, kitu ambacho sio kweli.
Japo sio kosa kubwa kwa mtu wa kawaida kuyaita marekebisho ya katiba kuwa ni katiba nyingine, lakini kwa Waziri wa Sheria, Live kwenye TV ya Taifa, kusema Tumekuwa na katiba 5 baada ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ni uthibitisho kuwa tunaye Waziri wa Sheria Asiyejua Katiba.
Wasalaam.
Pasco.
NB.(Somo la Katiba, ndio somo la kwanza kwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, anapufundishwa 'What is Law?').
1. Katiba ya Uhuru ya 1961
2. Katiba ya Jamhuri
3. Katiba ya Muungano ya 1964 ambayo binafsi naamini ilikuwa ni marekebisho ya Katiba ya Jamhuri.
4. Katiba ya Muda ya 1965.
Aidha, ieleweke kuwa Katiba ya Mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko mara 14 tangu kitungwa kwake. Natumia neno Mabadiliko kwani kwa kawaida Katiba hufanyiwa mabadiliko na si marekebisho! Marekebisho hufanywa kwa sheria za kawaida.