Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 487
Watanzania tunakoelekea yawezekana hatupajui au tumekuwa kama watu tuliofungwa kitambaa cheusi usoni. Nasema hivyo kutokana na tabia yetu ya kulialia ambayo kamwe imekuwa haiwasilishi uhalisia wa yale tunayoyataka! Kwa nini nasema hivyo?. Kupitia vyombo vya habari nimeona baadhi ya watu wanaojiita wamiliki wa vitalu vya uchimbaji wa dhahabu huko Geita wakilalamikia Selikari kuwapandishia kodi ya Leseni za umiliki wa vitalu hivyo kutoka shilingi 150,000 hadi kufikia shilingi 800,000.
watu hao ambao hata kwa muonekano wa macho ya kawaida hawaoneshi uhalisia wa kumiliki vitalu hivyo ndiyo wamekuwa wakijiweka mbele ya hadhira kuonesha kuwa wao ni walengwa kabisa ambao wanstahili kuonewa huruma na selikari kwa mgongo wa kuinua wajasiliamali.Leo hii kuna watu wanamiliki zaidi ya Leseni tano za uchimbaji dhahabu, iweje kama unaweza kumiliki Leseni tano na wafanyakazi zaidi ya miatano ushindwe kulipa kodi ya shilingi laki nane kwa mwaka?
Kwa hili naomba nisimame kati kuwa Selikari inatakiwa kuwa macho na ulaghai huu.Ikumbukwe kuwa wakati wa harakati za bunge letu kutaka kupitia upya mchakato wa umiliki na marekebisho ya vitalu vya uwindaji, walijitokeza watu wengi wakilalamika kuwa viwango vinavyopendekezwa na selikari ni vikubwa mno ambavyo hawataweza kuvilipa wakati huo huo wao wakiwa wamevikodisha kwa wageni kwa gharama kubwa tena wakilipwa kwa pesa za kigeni.
Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa hawa ndugu zangu wa migodini, wanatumiwa na wana siasa ambao ndio wamiliki wa Leseni hizo kwa maslahi yao. Selikari iliangalie hili kwa macho ya ziada kwani mafisadi wanajaribu kuvumbua mbinu mpya kila uchao kwa lengo la kuendelea kulinda maslahi yao tu.Kaa chonjo, watch out!!