Ombi la kusitishwa kwa wimbi la sherehe za miaka 50 ya uhuru

mwananchit

JF-Expert Member
Oct 13, 2008
242
296
Kuna hili wimbi la kila wilaya, mkoa, wizara na taasisi mbalimbali kufanya sherehe kwa kutumia gharama kubwa wakisherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi ambayo hata haipo ambapo hitimisho litakuwa ni tarehe 09 Disemba.

Kama kweli JK ni msikivu kama inavyodaiwa, ningeomba hili wimbi la sherehe chini ya kauli mbiu ya Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele, ZIAHIRISHWE na badala yake Watanzania kwa ujumla wetu bila kujali asili zetu, dini zetu nzuri, tamaduni zetu na itikadi zetu za kisiasa, tutumie muda huu kutafakari kwa kina Tulikotoka kama Taifa, Tuko wapi kama Taifa, na Tunaelekea wapi kama Taifa. Tafakari yetu izingatie mambo mengi na hapa chini nitapendekeza machache ninayodhania yanafaa kujadiliwa.

1. Je, Tumeweza kuboresha uchumi wa nchi yetu na wa mwananchi mmoja mmoja kwa kumwezesha awe na makazi bora, elimu bora, afya bora na maisha bora kwa ujumla? Kama sivyo, tumekwama wapi? Je tufanyeje kama Taifa ili tusonge mbele? Hivi uchumi wetu unakua? Hivi shillingi yetu tuisaidie vipi? Hivi kwa nini tulitumia 1.7 trillioni kuwalipa wafanyabiashara wasdiojulikana badala ya kuziingiza kwenye miradi ambayo ingeweza kuinua maisha ya watanzania? Hivi ni kwa nini hizo hela za EPA zilizobakia huko benki kuu tusiamue kuzitumia kwenye miradi ya maendeleo badala ya kuziacha huko halafu baadae zitushawishi ili tukopeshane na baadae kuzirudisha bila riba? Hivi kwani kuna mtu au taasisi inatuzuia tusifanye yale ambayo yanaweza kumuinua Mtanzania? Hivi ni kwa nini Watanzania ambao ni matajiri wa kupindukia ni wale ambao sio weusi? Hivi maharamia wa EPA, KAGODA, MEREMETA, DEEP GREEN, TANGOLD, RICHMOND, DOWANS, WALIOSAINI MIKATABA YA MADINI KAMA BUZWAGI NK, WALIONYONGA VYAMA VYA USHIRIKA NCHI NZIMA, NA HAWA WANAOENDELEA KUPORA UCHUMI WA MAMA YETU TANZANIA TENA MCHANA KWEUPE TUWAFANYEJE? Tuendelee kucheka nao wakati tunajua kwamba ukicheka na nyani....?

2. Je, Tumeweza kuboresha miundombinu yetu katika nyanja za barabara, reli, maji, umeme, mashule, hospitali? Je Ni lini Tutathubutu kufikisha miundo mbinu ya umeme kwa asilimia 86 ya Watanzania? Je, hawa asilimia 14 tu ya Watanzania angalau wenye miundombinu ya umeme majumbani mwao kwa sasa-ni lini watakomeshewa masuala ya mgao? Ni lini wananchi wa mijini watakuwa wanapata maji kutoka bombani badala ya kutumia madumu na magari (water bowsers)? Ni lini Tutaweza kujenga mabweni kwenye shule zetu zote za sekondari ili kuwapunguzia wanafunzi wetu adha ya kugombania daladala au kupachikana mimba kwa sababu ya kupanga vyumba mitaani katika mazingira hatarishi? Ni lini tutaboresha maslahi ya walimu na madaktari hata kama ni kwa kupunguza mapato ya wanasiasa? Hivi kwani wanaochangia kukua kwa uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi ni wanasiasa au ni wataalamu wetu ambao kwa kweli wamechoka? Ni lini tutaboresha hospitali zetu ili tuondokane na hii aibu ya viongozi wetu na wananchi wetu kwenda kusongamana huko India wakifuata matibabu hata kama ni tumbo kuuma? Hivi kweli tutaendelea kusafifirisha mizigo ya kwenda mikoani kwa malori (ambayo yanazidi kuharibu barabara zetu chache tulizo nazo na pia gharama yake ni kubwa hivyo kumwongezea mlaji gharama zisizo za lazima) wakati tuna reli aliyotujengea mkoloni wa kijerumani na imekaa bure bila kutumika?

3. Je, Tumeweza kuwapatia wananchi wetu amani na usalama wao na mali zao? Mbona nyumba nyingi licha ya kuwekwa ma-grill, bado zimefichwa ndani ya maukuta marefu ya uzio hadi nyumba zenyewe hazionekani vizuri labda ukiwa kwenye ndege ndio unaziona vizuri? Mbona kila siku watu wanaibiwa vifaa kwenye magari yao halafu wanaishia kuvinunua vifaa hivyo hivyo huko sinza na kariakoo gerezani na wahusika hawakamatwi? Mbona ukienda polisi, mahakamani au idara za ardhi hauwezi kupewa huduma stahili hadi utoe kitu kidogo?

4. Je, Tumeweza kuinua uchumi wa wananchi wetu au tunainua wa wageni tu? Hivi hizi haya mapumziko ya kodi (tax holidays) kwa nini iwe ni kwa wawekezaji wa nje tu? Hivi TRA imepewa hadidu rejea zipi, za kumwinua mzawa au kumdidimiza? Hivi ni kwa nini Mtanzania, tena wa hali ya kawaida anapoingia nchini ka gari ka cc 1000 au hata pungufu ili kumpunguzia adha ya daladala aishie kutozwa kodi kubwa kuliko hata gharama yote aliyonunulia na kusafirishia? Yaani serikali lazima ipate hela nyingi kuliko gharama za mtengenezaji na msafiririshaji zikiunganika?

5. Je, Tumethubutu kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali? Hivi hili wimbi la uundwaji wa mikoa na wilaya mpya una tija kweli kijamii na kiuchumi? Hivi kweli kiongozi hawezi akawa kiongozi hadi atembelee gari kubwa mithili ya nyumba? Hivi hili wimbi la semina elekezi lina tija yoyote kwa Taifa? Hivi haya matumizi makubwa tunayoyafanya kila baada ya miaka 5 tuyaite kuwa ni kwa ajili ya uchaguzi wa kumpata Rais ambaye ameshaapa kwamba ushindi ni lazima, au tumechanganyikiwa? Hivi kweli ni haki kwenda kumwomba ridhaa ya kuendelea kumtawala mtu ambaye tumemfanya asijue kiswahili, kusoma wala kuandika na anaishi kwenye nyumba ya miti na nyasi wakati amekuwa akitupa ridhaa hiyo hiyo kwa miaka 50 iliyopita lakini haoni mabadiliko yoyote? kwani sisi tumelogwa? Ni nani aliyetufanya tuwe hivi tulivyo? Yaani tuwe mkia kwa Kenya, Uganda, Rwanda na hata Burundi walio vitani tangia wapate kile wanachokiita uhuru?

6. Je, ardhi kubwa tuliyonayo na yenye bahari, maziwa, mito, chemichemi, vijito na maji mengi chini ya ardhi vimeweza kutupa mafanikio mazuri kiuchumi? Hivi haya madini, gesi, mafuta, misitu, wanyama pori, milima na vivutio mbalimbali vilivyotapakaa kila kona ya nchi yutu vimeweza kutupa mapato stahiki ya kuweza kutoa mchango madhubuti wa kukuza uchumi wa nchi yetu? Ni kwa nini pombe ndio ziendeshe uchumi wa nchi yetu? Hivi ni kwa nini viwanda vya pamba/nguo, korosho, ngozi, nyama, kahawa, vyuma (Mangula na kilimanjaro machine tools) vimekufa huku viwanda vya bia ndio kwanza vinashamiri? Au tumefanya maamuzi magumu ya kwamba tuwe walevi? au ndio maana tunaendesha uchumi wetu kilevi kwa kuwaachia hao wezi chini ya mwanvuli mzuri wa "wawekezaji" wachukue kila kitu hahi mchanga halafu watukopeshe hela zetu walizotuibia kwa masharti magumu na riba kubwa huku wakiturushia vizawadi vya vyandarua?

7. Je, tunahitaji kuwa na selikali kuuubwa bunge kuuubwa kama ilivyo sasa? Kwanini tuwe na majimbo zaidi ya moja ndani ya wilaya moja? kwani mwenye kazi kubwa ni mbunge, mkuu wa wilaya au ni mkurugenzi? Hivi anayeongoza wilaya (mtu ambaye ni final) ni nani kati ta wabunge (maana baadhi ya wilaya zina wabunge zaidi ya mmoja), mkuu wa wilaya, mkuugenzi na mwenyekiti wa halmashauri? Je, ni sahihi kwa bunge letu tukufu kukaa dodoma zaidi ya miezi miwili wakijadili hotuba za bajeti halafu mwisho wa siku zile hela hazipelekwi mikoani na wilayani kama ilivyokubaliwa? Hivi ni nini hasa lengo la kuwa na mijadala mireeefu hadi kupitisha bajeti halafu mwisho wa siku hela hazipo au zinakuwepo lakini zinafanyiwa shughuli nyingine? Hivi je, kweli ni halali na haki kuendelea kutumia hela za walipa kodi masikini kuendelea kupeana RUZUKU za kisiasa kwenye vyama vyetu huku walipa kodi walewale wakikosa huduma muhimu?

8. Hivi kuna muungano wowote uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar? Hivi kama Zanzibar wana Rais wao wanayemchagua kwa kura na kumwapisha wao wenyewe, wana serikali yao ya mapinduzi, wana bunge lao, wana jeshi lao (KMKM), wana mamlaka yao ya mapato, wana vitambulisho vyao vya utaifa, wana bendera yao, wana wimbo wao wa Taifa, HIVI HAPO KUNA MUUNGANO KWELI? Hivi ni kipi ambacho kimepungua kwao hadi wazuiwe kiitwa Taifa huru? Kwani hilo Taifa jingine lililoungana na Zanzibar hadi ikazaliwa Tanzania ni lipi? Bendela yao ikoje na Rais wao anaitwa nani? Hivi Zanzibar ikiachwa ikawa na uhuru kamili jhalafu tukawa wote ndani ya EA itakuwa na ubaya gani? Kwanini tung'ang'anie muungano ambao hata mtoto mdogo hawezi kuuona? Hivi tunadanganya, tunadanganywa, au tunajidanganya wenyewe? Tutaendelea kuishi katika hali hii hadi lini?

9. Je, hivi tunahitaji mwenge uendelee kuwamulika mafisadi na waporaji hadi lini? kwani hadi sasa hatujawaona? Naomba niulize: kwani huu mwenge wetu siku hizi UNAWAMULIKA mafisadi au UNAWAMULIKIA?

10. Je, nchi yetu inafuata itikadi gani? N akama ni ya ujamaa kama alivyodai kiongozi mmoja wa chama chetu tawala hivi karibuni, mbona sijawahi kumsikia Rais wetu akitamka neno UJAMAA NA KUJITEGEMEA japo kwa bahati mbaya hata siku moja? mbona neno WAWEKEZAJI haachi kulitamka hata kama anaongea na wananchi wa vijijini?

11. Je, hivi majukumu ya Rais wetu ni yapi? Je, katiba imempa majukumu ya kutosha ili asiwe na muda mwingi ambao hana kazi ya kufanya hadi aishie kusafiri-safiri au kuhudhuiria kila msiba? Kwani misiba yote ni ya kitaifa?

12.Au je, watanzania hasa wasio wanachama wa mavyama ya kisiasa wanapoona mambo katika nchi yanaenda isivyo, wanatakiwa wakasemee kwenye jukwaa lipi?


JK, sijui kama utaweza kuona huu ujumbe mfupi, lakini kama ungweuona, ningeomba siku moja ugome kweenda ofsini ili upate muda wa kutosha wa kutafakari na hatimae ufikie kwenye maamuzi magumu ya kusitisha hiki kiwewe cha sherehe ya miaka 50 ya uhuru na badala yake uruhusu watanzania watoe yale yaliyo mioyoni mwao juu ya mwenendo wa kiasiasa, kiuchumi na kijamii kuhusu nchi yao ili baadae tupate mwelekeo sahihi, Unaweza pia kuamua kuunda chombo huru cha kuratibu maoni na mapendekezo ya watanzania juu ya mustakabali wa nchi yao.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu na umpe hekima ya kutosha ili kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu muhimu katika historia ya uhai wa Taifa letu la TANZANIA-AMEN!


Wenu mtiifu kwa Tanzania, Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.


Mhandisi Dereck Mbanzendole (0784-858552)
 
Ni sherehe kwa kwenda mbele bila kujali huduma muhimu za jamii yetu ziko katika hali gani. Wabunge wetu wa upinzani mtuulizie gharama hizi hadi Desemba 9 zitakuwa kiasi gani.
 
Ni sherehe kwa kwenda mbele bila kujali huduma muhimu za jamii yetu ziko katika hali gani. Wabunge wetu wa upinzani mtuulizie gharama hizi hadi Desemba 9 zitakuwa kiasi gani.

WildCard na Dereck
Nakubaliana na kuwaunga mkono.kwa maoni yangu tusherehekee miaka 50 kwa kuwa ni historical fact sawa. Lakini on top of proposal za Dereck fedha zote za sherehe zinazoendelea sasa na michango inayoendelea nchi nzima badala ya kutumika kwa sherehe na vyakula/vinywaji 09.12 tuelekeze kwenye mpango maalum kufuta tatizo sugu la maji ili iwe tangible and concrete kumbukumbu ya achievement ya miaka 50 yetu. Tutakuwa tumethubutu na tumeweza bila wahisani. Ni hela nyingi zinatumika bila huruma kana kwamba tuna uhuru wa kweli.
 
Kama sikosei JK aliahidi kuwa sherehe hizi za miaka 50 zitaambatana na kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya. Sasa mbona masuala ya katiba yako kimya? Mimi ningefurahi kama mamilioni yanayoliwa sasa kwenye hizi sherehe yangetumika kuweka taratibu za kuandika katiba mpya na pia mijadala ingekuwa katiba, katiba, katiba na katiba. Sasa tunasherehekea mafanikio ambayo kwa kweli hayapo ukilinganisha na raslimali Mungu alizotukabidhi.
 
Back
Top Bottom