Rugemeleza
JF-Expert Member
- Oct 26, 2009
- 668
- 136
Wasomi hawaihitaji kujiunga na chama na siasa kwani itikadi za kisomi ni kuwa unasimamia principles za fairness and truth. Kujiunga na chama fulani cha siasa ni kuhama kutoka kuwa msomi na kuwa mwanasiasa. Kuna msemo mmoja maarufu unasema " A Politician is a failed academician" . Hivyo sidhani Tanzania inahitaji wasomi kujiunga na chama fulani cha siasa bali ni suala la Watanzania kujitoa katika limbi la ujinga na kuelewa nini kinaendelea. Kwani tukiwa na taifa lenye kujua nini kinaendelea nadhani changes will come otherwise hata wasomi wote wakijiunga na chadema hakuna changes zozote zitatokea Tanzania. Kumbuka wanaopiga kura tanzania si wasomi pekee bali watanzania wenye kujua na wasiojua kusoma.
Si kweli. Wasomi wenye mapenzi ya kweli ya nchi yao na wenye upeo wanatakiwa kuingia katika siasa ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli. Katika nchi zetu maskini siasa ni kila kitu na hivyo kuacha nchi iendeshwe kishikajishikaji ni uhaini. Kama Mwalimu alivyosema ili tuendelee twahitaji, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Kwa bahati mbaya Tanzania haina siasa safi na kibaya zaidi uongozi bora. Hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ule tunahitaji kuwa na wasomi wazalendo na sio wale wanaokwenda kuganga njaa au kulamba nyayo za watawala-uchwara ili kuweza kuipatia nchi yetu siasa safi na uongozi unaostahili. Nimesoma na baadhi ya wale ambao sasa ni mawaziri katika serikali ya CCM, mtu unajiuliza hivi kweli huyu kwa uelewa na upeo wake mdogo pamoja na kukosa kwake uzalendo ilikuwaje akawa waziri? Hao watu wameingia katika uongozi kutafuta mali na kuifuja nchi yetu kushinda ambavyo hata wakoloni.
Rai yangu ni kuwa Tanzania inahitaji uongozi mzuri na sera nzuri kutoka kwa viongozi wasomi wenye nia njema nayo hali kadhalika ni lazima viongozi hao wawe tayari kujisadikisha kwa manufaa ya watu wao.