Elections 2010 Ombi kwa Mzee Mwanakijiji na weledi wengine wa aina yake

Status
Not open for further replies.

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Ninaomba kuwasilisha ombi langu kwa Mzee Mwanakijiji na wengine wenye uwezo kama wake wa kujenga hoja ili wasaidie kutengeneza vipeperushi vitakavyosambazwa nchi nzima hasa maeneo ya vijijini ili viweze kutoa elimu ya urai.

Ningependekeza weledi hawa waandike na kujenga hoja kuelimisha yafuatayo:
  • Dhana kuwa vyama vya upinzani vitaleta vita vikichaguliwa kushika dola
  • Umuhimu wa kuwa na katiba mpya - Wengi wa wanavijiji hawajui na hawaoanishi umasikini uliopo na mfumo mbovu wa kiutawala unaosababishwa na katiba ya enzi za ukoloni na vita baridi
  • Umuhimu wa watawala wa mikoa na wilaya kuchaguliwa na wananchi ili kuongeza uwajibikaji
  • Dhana kuwa huduma za elimu na afya haiwezekani kutolewa bure
Ninajua muda uliobaki ni mchache lakini pia bado kuna nafasi ya kuweza kupenyeza elimu hii na kuleta mabadiriko makubwa tarehe 31 October 2010.

Hii ni nchi yetu na tunatakiwa sote tupambane na wote wanaotaka tuendelee kuwa gizani kwa propaganda zisizo na mashiko kama ambazo zinatumiwa sasa na chama twawala.

Naomba kuwasilisha
 
RC NA DC nao wakiwa wanachaguliwa naona itasaidia tena kuokoa mda wachaguliwe na madiwani na wabunge wa eneo husika
 
Ningependekeza weledi hawa waandike na kujenga hoja kuelimisha yafuatayo:
  • Dhana kuwa vyama vya upinzani vitaleta vita vikichaguliwa kushika dola
  • Umuhimu wa kuwa na katiba mpya - Wengi wa wanavijiji hawajui na hawaoanishi umasikini uliopo na mfumo mbovu wa kiutawala unaosababishwa na katiba ya enzi za ukoloni na vita baridi
  • Umuhimu wa watawala wa mikoa na wilaya kuchaguliwa na wananchi ili kuongeza uwajibikaji
  • Dhana kuwa huduma za elimu na afya haiwezekani kutolewa bure

Dr. Slaa yupo vijijini na kazi hii anaifanya kwa ujasiri wa aina yake. Ninaamini amewezeshwa na ROHO MTAKATIFU.

SOTE TUSEME AMEN
 
Heshima kwako Ntemi Kazwile.

Inataka muda wa kutosha kuhubiri elimu hii ili watu wa vijijini waelewe, mind you we are now talking of two weeks to d-day!
Mi nashauri wazo lako(kama lilivyo) lifanyiwe kazi hata baada ya uchaguzi ili iwe potential ya huko 2015!
 
Ninapoandika ujumbe huu simu yangu inaendelea kupata ujumbe wa kuwatisha watanzania kuwa Slaa ataleta vita. Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kuwa siasa ingekuwa ya kihuni nama hii... PLATO aliwahi kusema hivi "Wasomi, waadirifu na watu wenye weledi ambao hawaingii kwenye siasa, huwapa nafasi watu wasio waadirifu na wahuni katika siasa na watu wale (weledi na waadirifu) huishia kutawaliwa na watu hao wa hovyo"

Haya ndiyo tunayoyaona, tumewaachia nchi hii mbweha na fisi walafi wagawane urithi tuliopewa na Mwenyezi Mungu. Hakika tutajuta na kusaga meno siku ile tutakapotakiwa kutoa hesabu yetu mbele ya Mwenye Haki......

Ni wajibu sasa kuingia katika siasa ili tuikomboe nchi hii midomoni mwa mbweha na fisi hawa, tuwapeleka wanakostahili, jela!!!
 
Heshima kwako Ntemi Kazwile.

Inataka muda wa kutosha kuhubiri elimu hii ili watu wa vijijini waelewe, mind you we are now talking of two weeks to d-day!
Mi nashauri wazo lako(kama lilivyo) lifanyiwe kazi hata baada ya uchaguzi ili iwe potential ya huko 2015!

Kwa matokeo yoyote ile inabidi tuangalie kuitoa nchi hii katika giza totoro la ujinga na uoga mwingi
 
ni muhimu sana unachopendekeza na ni kweli kinaweza kuongeza idadi ya kura. lakini fikiria muda wa kuandaa kuhariri kudesign kuchapisha na kusambaza. pengine kwa muda uliobakia ni tija zaidi kutumia vyombo vya habari hata ikibidi kulipia. wangapi watachanga?
 
Mimi niliahidi 50,000 ya mdahalo wa wagombea, hii bado ipo na inaweza kutumika kwa ajiri hili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom