Ombaomba kila siku: uhuru u wapi

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
BAADHI ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini, wanadaiwa kuunda mtandao wa kufadhili shughuli za vyama vya siasa na wanaharakati kwa lengo la kuleta vurugu, ikiwamo kwenye mchakato unaoendelea wa kupata Katiba mpya.

Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema hayo jana bungeni wakati wa mjadala wa
Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011 na kuongeza, kwamba umekuwapo mtindo wa baadhi ya mabalozi kuingilia masuala ya kitaifa.

“Naomba watuache sisi tufanye mambo yetu wenyewe, mabalozi wanawakilisha nchi zao kwetu, lakini wanapotuingilia na kutaka kutuhujumu si vizuri,” alisema Ndassa.

Alisema mbaya zaidi mabalozi hao wamekuwa wakitumia baadhi ya vyama kufanya hivyo, hali ambayo aliilaani na kuwataka kuitumia CCM ambayo ni chama tawala, iwapo wanataka kukaa na kushauriana na vyama.

“Nchi hii tumejitawala wenyewe miaka 50 sasa, naomba msituingilie,” alisema huku akishangiliwa na wabunge wengine.

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), alisema kuna chama kimoja hivi karibuni kilipokea ufadhili kutoka nchi fulani (hakuitaja) na sasa chama hicho kinaeneza
mambo ya uongo.

Alisema huenda ufadhili huo ulikuwa na masharti kwa chama hicho, ndiyo maana kimeanza kufanya shughuli hizo za kueneza uongo.

Aliongeza kuwa haiwezekani kikundi cha watu wachache kiwe na haki na uzalendo wa kutaka mawazo yao pekee ndiyo yathaminiwe na kuwakilisha Watanzania zaidi ya milioni 42, hali ambayo alisema inatia shaka kutokana na watu wengine kutumikia mabwana wawili.

MTAZAMO WANGU:

Inasikitisha kuona kuwa kuna wabunge bado wana dhana kuwa tuko huru, uhuru unatoka wapi wakati hata kuwaomba wananchi kuacha pombe inabidi tupate ufadhili wa nchi za nje, vyandarua ufadhili, kufunga mikanda ufadhili, elimu ufadhi, afya ufadhili, barabara ufadhili kila kitu ufadhili.

Utawala bora ufadhili Katiba ni component kubwa ya utawala bora, msishangae kama mlisaini mikataba ya utawala bora basi fwedha za wafadhili ndo zinafanya kazi, serikali yenu ilisaini sana mkuki unawarudia msilie kaeni kimya, ndo utawala bora huo, vinginevyo tusiwe ombaomba yatakuja yaleyale ya sera za conservative


 
Sasa hivi imeshaamuliwa kuwa atakayeomba msaada basi hana budi kuolewa.

Waarabu wanatangaza sana nchi zinazotaka msaada toka kwao...wanakaribishwa.

Kuna suti nyingi bado ziko kule uarabuni.Mugabe alizikataa
 
Back
Top Bottom