Omba Mgomo wa Madaktari ukupitie Mbali!! Inasikitisha sana huko kitaani

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Tukio la Kwanza:
Hii imetokea leo alfajiri: Dada anawahi kazini saa kumi na mbili maeneo ya Kijitonyama sayansi. Yeye ni Muajiriwa wa kampuni ya simu za mikononi maeneo ya Moroko na Drive Inn Cinema. Wakati wa kuvuka, gari likamkanyaga na kumvunja mguu mara mbili. MOI pamefungwa, Hospitali zote wanamshahuri aende huko Muhimbili au alipe milioni nne kasha apate tiba.

Tukio La Pili:
Kijana apata Ajali. Kikanyagio kinaning'inia. Kapelekwa Temeke Hospitali, wakamwambia kwamba aende Mwanyamala Hospitali. Mwananyamala wakasema hawawezi kumtibu…wakamwambia aende MOI. MOI kumefungwa!
Wote wako kwenye dawa za kutuliza maumivu!

Ndugu zanguni tuombe Mungu sana janga hili lituepuke na serikali 'yetu' itatue hili suala la madaktari. Ni hatari na haichagui kipato ….Madaktari na walimu wawezeshwe!! Na si EWURA, TRA, BOT, TCRA et al.
 
ngoja kigogo mmoja apate ajali kitaeleweka tu!ataenda Dodoma watamuambia yule surgion mzuri yuko Muhimbili.akifika muhimbili madakta wamegoma.akipanga safari ya Apollo watamwambie appointment ni mwezi ujao.mpaka hali hii itokee ndio wataelewa huu mgomo unamaanisha nini.
 
Kwanza pole sana kwa hao ndugu zetu waliopata hayo matatizo,Ni kweli huu mgomo umeleta shida kubwa kwa watanzania wengi,Watanzania tumwombe Mungu il;i Serikali na madaktari wetu wafikie muafaka maana yeye MUNGU anaweza yote na yote yanawezakana kwa wewe na mimi tunayeamini kwamba MUNGU anajibu maombi.
 
Hakika, kwa scenarios hizo hapo mbili, huo mgomo ni wa kuusikia redioni tu!
Poleni sana hao ndugu!
 
Tunangoja nini kinachotakiwa ni sisi waannchi kuingia mtaani kuishinikiza serikali iwalipe madakatari maslahi bora
 
tukio la kwanza:
hii imetokea leo alfajiri: Dada anawahi kazini saa kumi na mbili maeneo ya kijitonyama sayansi. Yeye ni muajiriwa wa kampuni ya simu za mikononi maeneo ya moroko na drive inn cinema. Wakati wa kuvuka, gari likamkanyaga na kumvunja mguu mara mbili. Moi pamefungwa, hospitali zote wanamshahuri aende huko muhimbili au alipe milioni nne kasha apate tiba.

tukio la pili:
kijana apata ajali. Kikanyagio kinaning'inia. Kapelekwa temeke hospitali, wakamwambia kwamba aende mwanyamala hospitali. Mwananyamala wakasema hawawezi kumtibu…wakamwambia aende moi. Moi kumefungwa!
wote wako kwenye dawa za kutuliza maumivu!

ndugu zanguni tuombe mungu sana janga hili lituepuke na serikali 'yetu' itatue hili suala la madaktari. Ni hatari na haichagui kipato ….madaktari na walimu wawezeshwe!! Na si ewura, tra, bot, tcra et al.

kama ni kweli, waambie waende kibaha!
 
Yaani dah! Poleni sana wote mlioathirika au kuguswa moja kwa moja na impacts za mgomo huu. Naimani serikali imepata funzo kubwa sana na kama haitachukua hatua yeyote basi wananchi hatuna budi kuiangalia serikali ambayo haiwajibiki kwa wananchi wake. Nguvu ya umma tu
 
Kuwezeshwa kwa madkatari kulingana na mfuko wa serikali sio tatizo. Ni pande mbili hizo kukaa wakaelewana ni kiasi gani ama vipi. Naona kuna tatizo zaidi ya hilo.

Kama ni ukata wa pesa serikali nyingi hata zilizoendelea pia wana matatizo kama kwetu.

Busara zitumike madaktari wawaonee huruma wagonjwa. Watanzania tunamjua Mungu tuwaokewe wagonjwa kwa ajili ya Mungu tupate utulivu wa Moyo wote wagonjwa na madaktari.
 
Inatisha na inauma sana ila tusimhusihse MUNGU kwenye issue ambazo Walafi fulani hawataki wenzao nao wafaidi, hapa tunampa MUNGU majukumu ambayo yapo within our capabilities.
 
Tuangalie upande wa pili,haya ni matukio yanayotokea sana huko mikoani au maeneo ambayo hayako privileged.kwasababu yametokea dar,watu wanaona kama ni mara yakwanza kutokea Tanzania. Huduma za afya ni duni sana, imagine watu wangapi wanavunjika miguu huko vijijini,hata option ya kutibiwa moi hua hakuna, hakuna wataalam,hakuna vifaa!kama TMK au mwananyamala wanakuambia uende muhimbili wao hawawezi, you can imagine hospitali nyingine za wilaya huko mikoani walivyo na hali ngumu.Hapo ndipo utaona madai ya madaktari yana maana.kuboresha huduma za afya, kuboresha maslahi ili watu waende huko vijijini pia kuhudumia watanzania wenzetu. Vinginevyo option wanazo,wanaweza kwenda Bostwana,Namibia au wabaki mijini kwenye hospitali za wahindi na kupiga mishemishe za town. But hizo option zitawasaidia watanzania wote?au waliopo mijini tu? Umeshawahi kufikiria maisha ya watanzania yanayopotea kila siku kwa kukosa huduma bora za afya au kukosekana kwa wataalam au kuhudumiwa na mtaalam ambaye yuko demoralized? watanzania wangapi wanapata vilema huko mikoani kwakua hakuna huduma kama inayotolewa Moi?
 
Inatisha na inauma sana ila tusimhusihse MUNGU kwenye issue ambazo Walafi fulani hawataki wenzao nao wafaidi, hapa tunampa MUNGU majukumu ambayo yapo within our capabilities.

Kweli kabisa mkuu !
 
Yaani dah! Poleni sana wote mlioathirika au kuguswa moja kwa moja na impacts za mgomo huu. Naimani serikali imepata funzo kubwa sana na kama haitachukua hatua yeyote basi wananchi hatuna budi kuiangalia serikali ambayo haiwajibiki kwa wananchi wake. Nguvu ya umma tu
Siajelewa concept kwamba serikali ndio mkosaji ktk kadhia hii inatoka wapi.
 
Tuangalie upande wa pili,haya ni matukio yanayotokea sana huko mikoani au maeneo ambayo hayako privileged.kwasababu yametokea dar,watu wanaona kama ni mara yakwanza kutokea Tanzania. Huduma za afya ni duni sana, imagine watu wangapi wanavunjika miguu huko vijijini,hata option ya kutibiwa moi hua hakuna, hakuna wataalam,hakuna vifaa!kama TMK au mwananyamala wanakuambia uende muhimbili wao hawawezi, you can imagine hospitali nyingine za wilaya huko mikoani walivyo na hali ngumu.Hapo ndipo utaona madai ya madaktari yana maana.kuboresha huduma za afya, kuboresha maslahi ili watu waende huko vijijini pia kuhudumia watanzania wenzetu. Vinginevyo option wanazo,wanaweza kwenda Bostwana,Namibia au wabaki mijini kwenye hospitali za wahindi na kupiga mishemishe za town. But hizo option zitawasaidia watanzania wote?au waliopo mijini tu? Umeshawahi kufikiria maisha ya watanzania yanayopotea kila siku kwa kukosa huduma bora za afya au kukosekana kwa wataalam au kuhudumiwa na mtaalam ambaye yuko demoralized? watanzania wangapi wanapata vilema huko mikoani kwakua hakuna huduma kama inayotolewa Moi?

shukran kwa kuona hilo.wananchi wanaangalia ombi letu la nyongeza ya mshahara tu hawaangalii ombi letu la kuboreshwa huduma ya afya.huko mikoani hali tete..wananchi hana hela,nikikuambia ni mara ngapi baada ya kumtibu mgonjwa wananiomba nauli utashangaa..ukipata ajali maeneo kama ya wami next stop ni tumbi,muda wote huo kutoka wami hadi tumbi ushakufa
 
Back
Top Bottom