Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,462
- 154,333
Huyu jamaa alikuwa na majibu ya ajabu sana na maneno makali.
Nakumbuka siku moja alikuwa anahojiwa BBC na Tido Mhando, kwa kweli majibu aliyomjibu yalikuwa ni kichefuchefu, na hakika yaliidhalilisha tasnia ya habari na hata Tido Mhando pia.
Siku chache baada ya hapo akiwa ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi, alitoa amri ya maaskari magereza kupiga waandishi wa habari walio enda kuripoti ubabe wa maaskari hao walipokuwa wakiwahamisha kwa nguvu wafanyakazi wa ATC.
Baada ya hapo akaongea tena maneno mbofumbofu.
Huyu ndio Omary Ramadhan Mapuri ambaye sasa ametunukiwa ubalozi.
Kweli CCM hawatupi jongoo na mti wake.