Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

Nundu naye hawezi kukwepa kashfa hii.Kama aliyaona hayo yote siku za nyuma alichukua hatua gani?
By the way alishaonekana naye hafai kitambo baada ya kuonyesha wazi wazi kutaka kuua ATC na TRL mpaka alipolazimishwa na wabunge kutenga hela ya kufufua mashirika hayo.
 
Ni kweli hapa madudu ni kuliko Richmond maana Waziri anaingilia TPA kama walivyofanya wenzake kuingilia Tanesco!!! Hahaaa!! Richmond kumbe ilikua mbaya Pasco?!! I like that!!! Hawakuonewa kumbeeee!!!
Halafu bila aibu bado anataka huyo huyo mfanya madudu ndio tumkabidhi ikulu yetu, huwa nashindwa kuelewa kabisa ubongo wa Pasco una category ngapi!!
 
Complaint moja dhidi ya Waziri Nundu ni kwamba alitengua kazi ya Shukuru Kawambwa,Waziri aliyemtanglia katika ile wizara. Nakumbuka last month nilikutana na mtu mmoja alikuwa anasema kwamba ''Shukuru Kawambwa anaharibu kila anapokwenda''[Kama ni kweli Kawambwa anaharibu kila pahali,I have no way of knowing.] Kwa hiyo I hope they will double check kila wanaposema wanataka waziri yoyote ajiuzulu.
Lakini in this case nadhani hakuna utata. Waandishi wa habari walikuwa modest tu,na kuziita hizi habari kuwa ni 'tetesi' Hili jambo inaonekana kama vile mjadala umekwisha,bado tangazo tu. Ili mambo kama haya yasitokee in the future, I hope Ndugu Pinda atachukua muda kueleza umuhimu wa kufanya kazi kwa maadili mema ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali.
 
WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitarajia kutoa tamko la kujiuzulu kwa mawaziri kadhaa, siri nzito zimeanza kufichuka baada ya Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu kumtupia kombora naibu wake, Mhandisi Athuman Mfutakamba.

Waziri Nundu, alimtuhumu hadharani naibu wake, kwa kile alichodai amekuwa akisafirishwa nje ya nchi na Kampuni ya Kichina ya China Construction Company (CCC) na kumpeleka sehemu mbalimbali kwa gharama zao, ikiwamo China na Equatorial Guinea na Mauritius.

Alisema kibaya zaidi, Mfutakamba amekuwa akiondoka bila kupata kibali kutoka kwake.
Akizungumza na wandishi wa habari mjini hapa leo, Waziri Nundu alisema ameamua kuweka bayana nini kiini cha matatizo ambayo anatuhumiwa kukiuka taratibu za kiutendaji.

Alisema bodi na viongozi wakuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakiungwa mkono na Mfutakamba, Katibu Mkuu, Omar Chambo na Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kwa pamoja, wamemkalia kooni ili aachie ngazi, bila kujua chanzo ni nini.

Tunamshukuru Allah wote ni walewale,vinginevyo hadithi ingalikuwa nyengine hapa yarabi!Jakaya weye waokoe hawa

kwa nini umewaza hivi? au unamaanisha ingelikua vinginevyo, ile redio na lile gazeti la wiki wangepiga sana kelele?
 
WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitarajia kutoa tamko la kujiuzulu kwa mawaziri kadhaa, siri nzito zimeanza kufichuka baada ya Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu kumtupia kombora naibu wake, Mhandisi Athuman Mfutakamba.

...

Alisema bodi na viongozi wakuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakiungwa mkono na Mfutakamba, Katibu Mkuu, Omar Chambo na Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kwa pamoja, wamemkalia kooni ili aachie ngazi, bila kujua chanzo ni nini.

Hii wizara ilipangwa, ikapangika - Kweli Mfumo X unafanya kazi yake ipasavyo. Hapa hutawaona Rejao, Ritz1, KIM KARDASH, Mpemba Mbishi, Tume ya Katiba, Malaria Sugu, Faiza Fox, et al.
 
Alikuwa wapi kuyasema haya kabla kimbunga hakijaingia BUNGENI?
WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitarajia kutoa tamko la kujiuzulu kwa mawaziri kadhaa, siri nzito zimeanza kufichuka baada ya Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu kumtupia kombora naibu wake, Mhandisi Athuman Mfutakamba.

Waziri Nundu, alimtuhumu hadharani naibu wake, kwa kile alichodai amekuwa akisafirishwa nje ya nchi na Kampuni ya Kichina ya China Construction Company (CCC) na kumpeleka sehemu mbalimbali kwa gharama zao, ikiwamo China na Equatorial Guinea na Mauritius.

Alisema kibaya zaidi, Mfutakamba amekuwa akiondoka bila kupata kibali kutoka kwake.
Akizungumza na wandishi wa habari mjini hapa leo, Waziri Nundu alisema ameamua kuweka bayana nini kiini cha matatizo ambayo anatuhumiwa kukiuka taratibu za kiutendaji.

Alisema bodi na viongozi wakuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakiungwa mkono na Mfutakamba, Katibu Mkuu, Omar Chambo na Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kwa pamoja, wamemkalia kooni ili aachie ngazi, bila kujua chanzo ni nini.
 
Ina make sense maana tunajua king maker mwingine hapo wizarani na ilishasemwa sana mbona huyu jamaa Omar Chambo ni fisadi namba moja wameungana na watendaji wengine kumhujumu waziri Nundu!amezungukwa na mafisadi tu pole Nundu ulikaa sana nje hapa tz ufisadi kwanza uzalendo baadae sana
 
Tatizo kubwa ni kwenye uteuzi. Kikwete kajaza marafiki wake kwenye nafasi zote tatu yaani waziri, naibu waziri na katibu mkuu na hii ni kwa kila wizara. Waziri hawezi kusema chochote mbele ya naibu wake, naibu hawezi kusema chochote mbele ya katibu kwa sababu kila mmoja ni personal friend wa JK na huwezi kusukuma mtu.

Inakuwaje Naibu waziri asafiri nje ya nchi bila waziri wake kujua? Na hata akijue anaweza kweli kumzuia?

Pili, Watanzania tunatakiwa kutambua kuwa China inabebea kwenye 'state corruption' Siongelei rushwa ya mtu mmoja, hapana, ila linapokuwa swala la kampuni ya Kichina kushinda tenda kuna mtandao mkubwa toka kwenye serikali yao wa kusaidia kampuni zao zipate tender. Hili tatizo ni kubwa kuliko maelezo. Wanatumia makampuni makubwa kukopesha nchi masikini lakini ukweli ni serikali ya china iko nyuma yake.

Kikwete angekua ana interest na hii nchi ya Tanzania angevunja baraza lote la mawaziri na kuunda upya. Lakini ninachoona kinaendelea sasa hivi ni maonesho ya kutunisha misuli kati yake yeye (JK) na Lowassa! Maamuzi mengi anayofanya yanalenga kujibu mapigo ya Lowassa! Tanzania kwa sasa ni sawa na yatima! Hivi kweli Kikwete hashutushwi na ubadhirifu uliooneshwa na CAG? Achilia mbali sarakasi za wabunge wa CCM, yeye kama kiongozi mkuu anafikiri nini kuhusu report ya CAG?
 
Kwenye press conference nilikuwepo, kiukweli, upepo haumwendei vizuri waziri Nundu kaamua liwalo na liwe, kausema ukweli wa moyoni mwake na kuna uthibitisho beyond reasonable doubt, kuwa Waziri Nundu sio fisadi ila amezungukwa na mafisadi left right and centre, hivyo yeye kuishia kuonekana an enemy of the people and soon atafanywa kondoo wa kafara kwa kufutwa kazi kwa mtindo ule ule wa "funika kombe mwanaharamu apite".

Hili la uzalendo wa Nundu kutanguliza mbele maslahi ya taifa dhidi ya maslahi ya mafisadi, itamcost.

Iliwahi kutokea kule nyuma kwenye kisa cha IPTL aliyekuwa Katibu Mkuu wa Madini, Patrick Rutabanzibwa alipelekewa rushwa nene na Rugemalila siku ya Xmas Ave, na siku ya Boxing Day akairudisha kwa Rugemalila na kwenda kumripoti Waziri wake Kikwete kwa rais Mkapa, kilichofuatia Rutabanzibwa akahamishwa fasta, IPTL ikapitishwa juu kwa juu!.

Sasa ni zamu ya Nundu, subirini kama atafikia J.4!.

Paskali
 
Back
Top Bottom