Ole wenu CHADEMA!

Ogah,

Mimi nimesema tujadiliane jinsi ya kufanya kubadili katiba ili kuwe na fair ground kwa vyama vyote Rufiji anasema fikira zangu ni duni.

Sasa mimi na wao = Mtawala na mtawaliwa, nani ana akili zaidi ya mwingine?!!!!!

Ndio maana tutaendelea kuwatawala MILELE!

Guys sichangii topic hii tena!
 
Mheshimmwa Mbowe na wapinzani wote.
Ushauri wangu kwa sasa ni kuwa acheni kuota kwenda ikulu kwa sasa. Wekeni mikakati ya kupata wabunge wengi wazuri baada ya miaka 5 ijayo, ili tuwe na bunge makini na lenye changamoto. Hiyo ndiyo iwe vision yenu. Acheni kuota big dream before a small dream. Kama CHADEMA mnaweza kupata wabunge 50 katika bunge lijalo nina hakika baada ya miaka 10 mnaweza kuleta mapendekezo ya kusimamisha uraisi. Nyerere mzee wetu alimshauri Mrema akazanie ubunge kwanza, lakini hakuliona hilo na leo yuko wapiii???. Kuing'oa CCM siyo kitu rahisi hata kidogo bila ya kufanya big homework. Na homework ya kwanza ni kupata wabunge wa kutosha.

Ila kuna mjumbe hapa aliuliza hivi ni kwa nini CHADEMA ilishindwa vibaya kuweka mbunge katika jimbo la Hai ambako ndiko nyumbani kwa Mheshimiwa Mbowe???. Hili ni swali CHADEMA ni lazima mjiulize. Maana ni mategemeo ya kila mtu kuwa watu wa nyumbani kwako ni lazima wawe pamoja na wewe!!!!

Ushauri wa bure kwa Mbowe:
Mheshimiwa Mbowe, baada ya kumalizika uchaguzi nakushauri urudi tena vijijini kuwashukuru wachache waliokupa kura, na pia kujifunza ni kwa nini wananchi wengi hawakukupa kura za kutosha??? Wananchi watakupa majibu abayo yatakusaiia kujiandaa na uhaguzi ujao lakini focus yako iwe ni wabunge. Hata wewe rudi bungeni mheshimiwa.
 
Mbowe kuwa CCM sidhani kama ni kweli ni kupotosha ukweli kama walivyosema wengine. Mzee ES ametoa hoja kuwa mbowe ni ccm kwa vile moja ya hoja zilizotolewa ni kuwa anashinda na viongozi wa CCM nk.

Sidhani kama ushahidi uliotolewa unatosha kumuhukumu kuwa huyu bwana ni CCM. Alipokuwa London akitokea kuhudhuria mkutano wa chama cha Conservative ambacho ni chama rafiki na CHADEMA, Freeman Mbowe alipata fursa ya kuwa-adress tanzanian journalists waliopo London ambapo mwandishi mmoja Juma Pinto alimuuliza Mheshimiwa Mbowe unaonekana sana na viongozi wa CCM na Ikulu unahudhuria sana sasa hivi ni kweli habari kuwa wewe ni CCM au una mpango wa kujiunga na chama hicho?

Majibu yake yalikuwa ni darasa zuri kwa waliohudhuria manake alisema tatizo viongozi wetu hawajui mipaka baina ya siasa na mahusiano mema ya viongozi, sio dhambi la kiitikadi wala kiitifaki kwa Kikwete kuja kwangu au mimi kwenda kwake lakini kinacho-matter ni namna gani nchi itasonga mbele. Umuhimu wa kitaifa ni muhimu kuliko majungu kama hayo. Waliosema hayo wana haki ya kufungua vinywa vyao lakini najua kwa vile nasema mimi basi mimi ni mti mzuri wenye kufaa kupigwa mawe na nawathibitishieni kuwa mimi sio CCM sina haja ya kuwa huko na wala hawana haja na mimi lakini hii haimaanishi kuwa mimi niwe adui yao kimaisha vile vile kwa kuwakimbia! tufike wakati watanzania tuwe tunazikana na kutembeleana na tukubali kutofautiana katika mijadala-mwisho wa kunukulu.

Naam kwa maelezo hayo nadhani imefaa kuelewa kuwa sio kweli yeye ni ccm.

Lakini nadhani turejee kwenye moyo hasa wa mjadala huu kuwa kuna njama za kumbomoa Mbowe nadhani habari ile haina ushahidi wa kutosha ni speculation ya kawaida sana iliyopewa kicha kizuri kwa lengo la kuuza gazeti, ethically it is a bad policy kupursue stori za namna hii manake katika maudhui hakukuwa na lolote.

Beside nadhani kwa sasa CHADEMA ni moto wa kuotea mbali lakini bado hawajafikia level ya kuwakuna kichwa viongozi wa nchi.

Nadhani it is not true kusuggest kuwa kiongozi anapangwa kumalizwa!

Again napenda kuungana na wengineo humu kumkaribisha JJ MNYIKA, we go way back a bit na najua sasa tutaondokana na hadithi za baraza la kahawa.

Mwanakijiji nimefurahia sana analysis yako kuhusu tanzania's role in illegal arms trafficking, well done! keep it up.
 
Unajua thanks God kuwa hii sio mahakama, ni forum ya wananchi kutoa mawazo yao wakiwa huru, huku wakiiingia kwa majina ya bandia,

By the way, talking about habari za barazani!,

kwa majina kamili ni Dr. Hassy Kitine - sio Form Six maana asingeweza kufundisha University huko Canada hawaruhusu Form Six kuwa Professors,
Na Mzee Mzena ni Undergraduate wa Makerere University, akiwa darasa moja

na Balozi Lusinde, na Mzee Chiume, ambao wamenithibitishia kwa ushahidi ambao pia nimethibitishiwa na hata mtoto wake ambaye ni mshikaji toka utotoni Bob Richie, ambaye pia amenikabidhi the whole CV, ikibidi nitaitoa yoteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, kwa hiyo sio darasa la nne au la nane!

Halafu stop this obsession na Mzee Es, maana ni ngoma kubwa unacheza na ukuta, sauti ya wananchi haitazimwa na LOGIC, Mzee ninamjua Free kuliko unavyofikiri, bro wewe hunitishi ni mtu mdogo sana, halafu acha jina langu unapoandika LOGIC zako!

By the way kuna USHAHIDI, kuhusu balozi wetu mwenye SEXUAL RELATIONSHIP na mama wa Ki-Sirilanka? Tuzifanyie kazi ili balozi huyo arudishwe mara moja?
 
i am a bit puzzled na hii comment manake nashindwa kuelewa basis ya kuwekwa akina kitine na mzena, tunamove on hapa hakuna kurudi nyuma.

I am not sure mahusiano ya mwandishi na Freeman na wala haiwezi kuwa hoja kama wanajuana basi awe ni ccm au vinginevyo, mimi pia namfahamu Freeman vizuri tu au niseme tunafahamiana sana lakini nadhani sio la muhimu lililo muhimu hapa ni ukweli kuwa hoja imekuwa supported vipi na kwa maoni yangu it was poor performance ya mchangiaji sasa kama hataki hoja zake zijadiliwe nadhani ni muhimu tujue aweke wazi.

As far as I am concerned mimi ni mwanachama halali wa forum hii na nina haki kama wengine ya kuchangia hoja, kuunga na kuungwa mkono au kupinga na kupinga...sijamtisha yeyote humu na kama yupo basi ningeomba kuelekezwa niombe radhi ila nami nina machungu na nchi yangu sana more than others humu would care to imagine ila ninakereka na matatizo ya wananchi wetu lakini pia na mijadala isiyo na kichwa wala miguu tunayoweka humu.

Kama lengo ni kujenga nchi tujadili issues sio personalities unless iwe personality ni relevant na hoja husika.

mungu ibariki tanzania...
 
marekebisho in the last post:

kupinga na kupingwa

na pia sentensi mijadala isiyokuwa na kichwa wala miguu humu isomeke BAADHI ya mijadala isiyo na kichwa wala miguu humu...

samahani kwa usumbufu.
 
Freeman hasaidiwi na Conservative Party, hiyo ni kanyaboya yake kwa watu kama wewe, Freeman hupewa hela na WESTMINISTER FOUNDATION, charity group ambayo inaongozwa na kumilikiwa na Tony Blair, ambaye tunaambiwa anapaswa kuwa ni RAFIKI wa karibu wa Mkapa,

kwa hiyo mzee tunamfahamu Freeman, wakati anazungumza kwenye huo mkutano wako wa waandishi wa habari Freeman hakusema hiyo foundation imempa hela zenye thamani ya SHILLINGI MILLIONI MIA SITA ZA TANZANIA, kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge, na madiwani, ila alizungumzia huo usiasa ambao wewe unauita ni ukweli kuwa hakuna ubaya kuwa marafiki na kina Kingunge, Kinana, na Malecela!

Sasa kwa taarifa yako ni kuwa sisi ndani ya CCM tulishajua hilo hata kabla hajaingia kwenye huo mkutano wako na waandishi wa habari, sasa nisaidie tulijuaje wakati yeye hana uhusiano na CCM?

Unafikiri ni kwa nini hakuzitumia hizo hela kusaidia wabunge wengine na madiwani, badala yake akazichoma kwenye hellikopta tuuu?

Mzee angalia hapa kuna watu wazima, usichezee motto, sas tuko Cuba, tunaelekea NY, karibu tukutane kama unao ubavu huko NY, badala ya kuwasumbua wananchi hapa!., halafu aliyeandika hiyo mada ni mzee Bob Mkandara, nafikri amesikia kuhusu mada isiyokuwa na kichwa wala miguu, katika dunia ya leo ya vyama vya siasa na upinzani hakuna kiongozi anayepata kura asilimia 80%, unless wale upinzani ni waongo kama Freeman!
 
Jamani kuna issue hapa mnaikwepa au hamuifahamu, hilo gazeti la Tanzania Daima ni la Freeman Mbowe,na ofisi zake ziko pale pale Billicanas
 
MzeewaBuasara
Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu nilikuwa Moshi na nilikaa kweney hotel moja hapa ambapo alikuja Katibu Mkuu wa CCM Mangula na baadhi ya CCM and Govt Officials .Mimi nikabahatika kusikia maongezi yao maana owner wa hotel ile ni mwana CCM mkubwa .Mzee ushindi wa CCM Tanzania achilia mbali Kilimanjar haukuwa wa kura za kawaida na hili utalikataa hdi kufa lakini hata JK siku ya kutangazwa mshindi alisema he never expected to have CCM winning 80% Mzee Es hapa utakataa lakini unajua what you did guys ili baadaye mseme kama leo kwamba why he did not clinch an MP seat toka jimboni kwake .

Maneno ya maana hapa ni kariba kubadilishwa na kuwekwa mchezo uwe sawa kwa sawa utaona mwisho wa CCM. A ruhusuni Mgombea Binafsi muone kazi . Ila nakubaliana nae kwamba Chadema they still need to learn Mbowe aende akaseme asante kwao ndiyo siasa hizo .

Zanaki nimeanz akuogoa kidogo hoja yako. Ina maana gazeti likiwa la Mbowe lisiandike habari zinazo mhusu Mbowe ama una maana gani ? Nifafanulie .
 
Mzeeshughuli, hapana,huko nyuma kuna mtu ali-suggest kuwa hilo gazeti ni la CCM au wanamtandao,kwa hio ni kampeni ya hilo gazeti dhidi ya Mh Mbowe.

Kuhusu kuandika au kutokuandika,kwa kweli sisi ni wasomaji tu,na wakiandika ni vizuri zaidi kwetu kwani tutalisoma tu na kudebate hizo hoja sehemu kama hizi.Pia inategemeana mhariri wa hilo gazeti,ambaye naamini kabisa sio mmiliki wake kama ana uhuru kamili wa kuandika what he deems news worthy,kama Sunday News la juzi lilivyoirudi serikali juu ya issue Manji na Salamander hse.

Kwenye mambo kama haya unaweza kuangalia kutoka kwenye pande tofauti.Inawezekana ni kampeni zake mwenyewe Mbowe,maana kama tunavyojijua watanzania huwa tunapenda harufu ya rangi!Ikiisha na wao uhama...Hii nikiwa na maana kuwa watanzania wanapenda kitu kipya wakati wa upya wake.Free alikuja na upya au tuseme an aura of freshness,topping it up with a helicopter.Kwangu mimi hio ndio harufu ya rangi mpya!Uchaguzi ukiisha,na harufu imepotea,kwa hio Mwenyekiti wa Chadema anabaki na waChadema wake,hivyohivyo kwa wengine,na watanzania wanarudi kwenye nyumba yao ya zamani yenye nyufa,paa kuvuja ambayo ni CCM.Tuliona ya Mrema,as from then on u never get stronger in this country as long as ur in the opposition.Kwa kifupi ni kwamba all the hype wakati wa uchaguzi ndio kilele,kutoka pale ni kushuka tu,na hii inatokana na mfumo mzima wa hali ya kisiasa nchini kwetu,main objectives za hivyo vyama pinzani...sasa hapo hatujaweka defections suffered by these parties.

Sawa,CCM inaweza kulaumiwa kwa mengi ya haya mambo,naturally...Wasiwasi uliopo ni kwamba watanzania wengi wanazidi kuona ya kuwa ni bora ya jini ulijualo.Kinachohitajika ni fikra mpya kabisa ambazo naamini kabisa watu kama Mh Mbowe wanazo na wanao uwezo wa kuzitambulisha kwa wananchi.

Sera za kuendelea kuisema tu CCM zimeonekana kuwa hazifanyi kazi kama watu walivyotegemea, kwa sababu watu haohao baadae wanahama vyama vyao na kujiunga na CCM hiyo hiyo tena kwa sababu ya maslahi.Sasa hio imani kwa wananchi kwenye upinzani itatoka wapi?Ndio unakuta anabaki mtu kama Mbowe na Mbatia,ambaye amekuwa mkimya kidogo,tofauti na cheche alizokuwa anatoa miaka ya nyuma.

Ukiangalia utatambua kuwa sijaitaja CUF humu kwa makusudi tu,kwa sababu kwa maoni yangu ile imekuwa ni kama dini.Miaka nenda rudi wagombea ni walewale,kura ni zilezile,wabunge/wawakilishi ni idadi ileile,gia yao ya uislam imeishia hapo,na rais wa sasa ni mwislam pamoja na makamu wake na viongozi wote wa Z'bar,kwa hio kwa mtaji huo CCM inawaonyesha kuwa nao wamo!Ndio maana yangu ya kusema tunahitaji fikra mpya ndani ya upinzani,kutega masikio mapya ya watanzania ambao hawana imani na upinzani kabisa,na wengi ya hawa unakuta hata kupiga kura hawapigi,as they feel they have no choice.

Freeman Mbowe ni mfanyabiashara na mlipa kodi,pia biashara zake ziko kwenye jengo la serikali (NHC) ambapo analipa kodi,kama kweli serikali inataka kummaliza,Manji si angeuziwa jengo lile ambalo haliko kwenye orodha ya majengo yanayohitajiwa kuhifadhiwa,au ndugu zanguni mna mtazamo tofauti?
 
Mzee Es said:
Freeman,

(1). Kwanza ni rafiki yangu, na ninajua kuwa ni wachangiaji wawili tu hapa wanaomjua personally, Bob na Jasusi, lakini ninaamini kuwa part yake ya siasa ninaifahamu kuliko wengine wote. Free is a good man na ni visionary man, nimemuona kwa macho yangu akiigeuza Mbowe Hotel kutoka just another Guest house mpaka kuwa Hotel ya kweli, na mpaka sasa Bilicanas. Hata siku moja siwezi kusema Free ni msaliti, hapana! lakini I believe kuwa within his heart Free ni CCM, cham cha marehemu baba yake, na ni kupitia Azimio la Arusha ndipo baba yake aliweza kuinunua hilo jengo kupitia (CCM-TANU), baada ya kazi kubwa ya mzee Haikaeli kumsaidia sana Mwalimu enzi zile.

Katika uchaguzi uliopita CCM kama kawaida yao, waliingia na full gears, lakini toka baada ya Dodoma kulikuwa na wasi wasi mkubwa ndani ya CCM kuwa wananchi walioendelea ni vigumu kumpigia kura mgombea wao, maana hakuwa na record, na mikoa iliyoendelea sio siri inafahamika kuwa ina wananchi ambao sio rahisi kuwadanganya, na sio siri Free aliwika sana kwenye hiyo mikoa, sasa matokeo ya uchaguzi ndiyo yaliyowashangaza sana CCM, kwani hakuna aliyetegemea kuwa Freeman angepata kura chache vile, na mpaka leo hii hakuna anayeelewa exactly what happened? Na hata Freeman mwenyewe haelewi ni nini kilitokea? Sio kwamba angeweza kushinda, no! lakini ilitegemewa kuwa wabunge wengi wangetoka Chadema, ukweli ni kwamba hata mimi binafsi niliamini kuwa bunge lingekuwa nusu kwa nusu, kati ya CCM na Upinzani na hasa Chadema, kwa hiyo yes!, wakati wa uchaguzi Free alikuwa tishio lakini matokeo yalimaliza kabisa nguvu yote ya Free kisiasa kwa maoni yangu, na Chadema itafanya makosa makubwa kumsimamisha tena uchaguzi ujao.

Freeman alikuwa ni a strong candidate kuliko wote waliogombea kwa maoni yangu, na JK alikuwa ni the weakest candidate, Free alikuwa na strong political points kuliko wote, lakini tatizo ni kuwa alikuwa peke yake mtu mmoja, akiwa Songea maana yake ni Chadema nzima iko huko, as opposed to CCM! Halafu vyama vyote upinzani vinaendelea kuwa tatizo moja sugu, nalo ni kwamba wako mijini tu! Hawako vijijini, kura karibu zote za CCM zinatoka vijijini, kama vile kura za Bush kwenye uchaguzi wa mwisho zilitoka vijijini. Halafu Free alisindwa kuzi-simplify point zake ili zieleweke na wananchi wa chini, kwa mfano majimbo ilikuwa ni a very strong one kuliko zote alizokuwa nazo, lakini baada ya kushindwa kuisema vizuri CCM wakai-simplify kuwa ni chanzo cha kuleta ukabila na udini na wananchi wakakubali kuwa ni kweli!

(2). Kufunga magazeti yasiyokuwa na muelekeo ambayo kazi ni kuwapotosha tu wananchi na kupandikiza chuki za bure miongoni mwa wanajamii ni hatua moja muhimu sana katika kufanikisha kuwaelimisha wananchi na taifa na kuwaamsha kisiasa, wewe mwenyewe unajua kuwa tatizo letu kubwa bongo ni wananchi wasioelewa kitu chochote, wakipewa pilau tu wanakuja na kukupa kura! Media ni a very powerful tool ya kuwapotosha wananchi,

ninasema haya magazeti yazungumzie our real problems, kama vile rais kusafiri na wajumbe 50, yaulize EL alikwenda kufanya nini huko Majuu ambalko rais tayari alikuwa huko majuzi tu, magazeti yaulize ni nani aliyeruhusu wabunge kupewa shillingi millioni 40 za magari, badala ya 30 kama ilivyokuwa ni nani aliyeruhusu nyongeza ya millioni 10? Magazeti aulize ni kwa nini tunjenga bunge jipya na wakati tuna Karimjee na Dodoma tayari, wakati hospitali zetu zinatisha kwa uchafu na umasikini? Wananchi wanahitaji kujua ni kwa nini tunagawana umeme? Yapige kelele kuhusu mikataba mbuzi? Wote tumeona jinsi Media ilivyosimama kidete juu ya nyongeza za wabunge mpaka rais mwenyewe akaogopa na kujitoa kuwa yeye hahusiki, sasa kwa nini wasifanya hivyo kwenye issue zote? Badala yake wanakuja kuandika ujinga, I mean NONESENSE! CCM kummaliza Free wanahitaji kukaaa kikao kizima cha CCM?, badala tu ya kumtumia TRA kufunga biashara zake? I mean ukifunga biashara za Free basi na siasa zake zimekwisha kwa sababu aslimia 80% ya shughuli zake za kisiasa Free anatumia hela zake binafsi kwa hiyo akiwa tatizo ni kufunga njia za kuingia pesa zake!

Kwa hiyo mzee kuhusu magazeti, kinyongo changu ni kuwa hayazungumzii real issues ambazo ni muhimu kwa wananchi, na ndio maana hayauzi tena siku hizi, yamebakia kutegemea vikundi vya vyama vya siasa! Isipokuwa kama wananchi kama wewe wanaona kuendelea kuandika ujinga badala ya issues ni sawa, basi yadumu!

(3). Mzee Jasusi,

Swali la mil 40, ninaona mzee Bob amelijibu vizuri, kuhusu sera ni kweli sera almost zote za JK, originally zilikuwa za Free lakini akaweza kuziwahi na kuzigeuza kuwa zake, kama vile Bill Clinton alivyokuwa akiwafanya Republicans, kwa mfano ile issue ya Welfare mwaka 1996, politically sio dhambi ila sasa tatizo linakuja utekelezaji, sasa magazeti yetu yalipaswa kuanza kumuuliza JK vipi zile ahadi za ajira millioni moja kwa mwaka au mwezi?

Kwa kumaliza ninasema kuwa Free alijitahidi, na laifanya kazi nzito na inahitaji kupewa heshima, lakini katika siasa tunaangalia umeangukia wapi sio umeangukaje! Ndio maana huko majuu uchaguzi ukiisha tu, kina Gingrich wanaambiwa wajitoe waingie wengine, huu ni wakati muafaka kwa Free na chadema kuanza kumpromote JJ, na wengine, Free akae pembeni na kuendeleza chama chake, mamboi mengine kama ninavyosema siku zote siwezi kuyaingilia kiundani mno maana tunamuamini Mungu na kufunga milango ya magari yetu!

Mzee ES,

1.Inawezekana unamjua sana Mbowe but how far sure are you that wewe unamjua zaidi ya wote,as you have claimed?That's overgeneralization.Pengine hata mkewe hawezi kusema anamjua zaidi ya watu wote.Yaani kwa kifupi,wewe kama rafiki unamjua,nduguye wa damu moja anamjua zaidi,lakini hakuna mtu anayejua zaidi ya anavyojijua mwenyewe.Na pia unafanya makosa kudhani wewe pekee ndio unamjua Freeman zaidi ya wengine.

2.Vigezo vyako ulivyotumia kuonyesha kuwa Freeman ni CCM damu moyoni mwake havina uzito.Suala la Baba yake kuwa karibu na Mwalimu halina uhusiano na tabia ya mwanaye.Tuna kajitabia flani huko nyumbani ya kuhisi kila mpinzani ni mwana-CCM wa siri.Ni kweli kwamba ni vigumu kuwa mwanasiasa nchini Tanzania bila kuwa ulipitia CCM kwa vile nchi yetu ilikuwa ya mfumo wa Chama kimoja kwa miongo kadhaa.Mimi sio mwana-CCM lakini nilipokuwa mwanafunzi zamani hizo nililazimishwa kuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM.Ilikuwa ni lazima,sio hiari.Sasa kwa vile Mzee Aikaeli Mbowe aliweza kununua jengo kutokana na Azimio la Arusha basi lazima mwanae Freeman atakuwa CCM damu?Hiyo ni hoja Finyu kwa sababu unashindwa kuelewa kuwa sear ya Azimio la Arusha ilikuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja na sasa tuko kwenye zama ya vyama vingi.

3.Hivi magazeti yasiyo na mwelekeo ndio yapi hapo?Ya udaku kama KIU na IJUMAA,ya chama na serikali kama Uhuru/Mzalendo na Daily News,au ya watu binafsi kama Nipashe,Tanzania Daima,Mtanzania,etc?Wana CCM mna kasumba moja ambayo ni matokeo ya mfumo wa chama kimoja:siku zote fikra na kauli za kiongozi ziko sahihi,hivyo zinapaswa kudumu,na zinatakiwa kuandikwa kama zilivyo bila kuzihoji au kuzidadisi.Na kwa hilo magazeti ya Chama (UhURU na Mzalendo) na ya serikali Daily/Sunday News yamefanikiwa sana.Yanaripoti kile kinachosemwa na waajiri wao,CCM na serikali yake.Nyie wenye fikra za chama kimoja hamuwezi kamwe kuona magazeti yanayodiriki kuwakosoa viongozi wenu.Sio kosa lenu kwa vile mazowea yenu yamekuwa kama desturi.Hivi kati ya Tanzania Daima na Uhuru lipi linazungumzia real issues za Watanzania?Hivi unatarajia Mhariri wa Uhuru anaweza kutoa habari ambayo ni ya maslahi kwa wananchi lakini ina madhara kwa mwajiri wake?Kwako real issues za wananchi ni zipi?Na ni kipi kinachokushawishi uamini kuwa hayo magazeti usiyoyapenda haya-address real issues za watanzania?Na ni kwa vipi "magazeti makini" yana-address hizo ishu?Tusirudishane nyuma,acheni vyombo huru vya habari vifanye kazi zake unless tunataka kurejea kwenye zama za kusikia mema tu ya watawala na ni mwiko kuwazungumza vibaya.Inaelekea umeathiriwa sana na udikteta wa mfumo wa chama kimoja mpaka unakimbilia kushauri magazeti yafungiwe.Unadhani kufungiwa kwa magazeti ndio utakuwa mwisho wa sie walalahoi kudai haki zetu?Siku hizi kuna njia nyingi zaidi za kupashana habari ikiwa ni pamoja na fora kama hii.

4.Kupora sera si tatizo lakini kwanini CCM ikimbilie kupora sera za CHADEMA kabla haijaanza kutekeleza sera zake yenyewe?Hivi hawa watu walitoa ahadi ngapi wakati wa kampeni za uchaguzi?ni ngapi kati ya hizo wameshatekeleza kabla ya kukimbilia kupora sera za wenzao au kuja na ahadi mpya?Ni dhahiri kuwa vyama vya upinzani vinahujumiwa sana na CCM,na sababu ya kufanya hujuma hizo ni simple:kuendeleza ulaji.Nani ndani ya CCM yuko tayari kuona upinzani unachukua madaraka na probably kupelekwa mahakamani kutueleza alikopata utajiri wa kutupa alionao?CCM inatumia kila njia ilizonazo kukaa madarakani,lakini kubwa zaidi ni matumizi ya fedha.Na mazingira yanaruhusu matumizi ya fedha katika siasa:watu ni masikini,ukiwapa flana na pishi za mchele,au senti za bia,basi unaingia madarakani.

5.Nyie wenzetu mlio nyumbani mna nafasi nzuri ya kuboresha nchi yetu kwa mawazo positive kuliko haya ya kurejeshana kwenye udiktata wa chama kimoja.Tukumbuke kuwa viongozi nao ni binadamu kama sie,kwa maana hiyo wanaweza kukosea kama sie binadamu wengine tusio viongozi.Kuipenda CCM ni OK kwa wanoipenda,lakini sio dhambi kutoipenda,na ni upuuzi kufikiri kwamba kila gazeti linaloandika kinyume na matakwa ya watawala linapaswa kufungiwa.
 
Duh, Maneno makubwa na mazima sana hayo Mlalahoi.

Nasubiri kutoa pongezi iwapo kauli ya kutaka magazeti yafungiwe itakuwa withdrawn ... kuwa mchangiaji aliteleza tu katika kutoa hoja.
 
Mzee Mlalahoi,

Heshima yako mkuu, kwa kweli siwezi kukujibu maneno yote uliyoandika ila nitavuta machache,

(1). Ninaomba unitajie nchi ambayo ni mafno mkubwa duniani ya mabadiliko ya maendeleo kutokana na mgombea binafsi?

(2). Ninakuomba unitajie gazeti moja huku bongo ambalo linajihusisha na kuandika siasa unalifahamu kuwa halina influence ya CCM au Upinzani?

(3). Ninakuomba uniambie ni kwa nini Freeman hakutumia hela alizopewa UK kwa ajili ya uchaguzi, kuwasaidia wabunge na madiwani? Mpaka ikabidi Ndugu Lusinde kule Mtera aliyekuwa akigombea na JM, ajitoe kutokana na kutokuwa na hela wakati yeye anapanda Helikopta tuuu?

Ninaomba majubu ya hayo kwanza wakati ninaitafakari hiii habari yako nzima na nitaijibu kikamilifu kwa sababu ninapenda watu positive kama wewe, na hii ulioindika hapo juu ndiyo siasa yenyewe ya bongo, yaani huku kukaye!

Kuhusu kumfahamu Freeman, ni kwamba toka nianze kusoma na kuandika hizi forum, nili-conclude long ago kuwa ni Bob Mkandara tu anayemjua Free, au "Mchagga", kama tunavyomwita kama ninavyomjua, kwenye hili la Freeman kwa kweli sina zaidi la kuongeza maana siwezi kwenda deep zaidi na kutoa mengine, ila nitakubaliana na wewe kuwa simfahamu na kwamba sio CCM, maana maneno yako kama walivyosema wazee wengine hapo ni mazito sana,

isipokuwa I will get back to you soon kwenye mengine yote, isipokuwa Freeman.
 
Mzee Es said:
Mzee Mlalahoi,

Heshima yako mkuu, kwa kweli siwezi kukujibu maneno yote uliyoandika ila nitavuta machache,

(1). Ninaomba unitajie nchi ambayo ni mafno mkubwa duniani ya mabadiliko ya maendeleo kutokana na mgombea binafsi?

(2). Ninakuomba unitajie gazeti moja huku bongo ambalo linajihusisha na kuandika siasa unalifahamu kuwa halina influence ya CCM au Upinzani?

(3). Ninakuomba uniambie ni kwa nini Freeman hakutumia hela alizopewa UK kwa ajili ya uchaguzi, kuwasaidia wabunge na madiwani? Mpaka ikabidi Ndugu Lusinde kule Mtera aliyekuwa akigombea na JM, ajitoe kutokana na kutokuwa na hela wakati yeye anapanda Helikopta tuuu?

Ninaomba majubu ya hayo kwanza wakati ninaitafakari hiii habari yako nzima na nitaijibu kikamilifu kwa sababu ninapenda watu positive kama wewe, na hii ulioindika hapo juu ndiyo siasa yenyewe ya bongo, yaani huku kukaye!

Kuhusu kumfahamu Freeman, ni kwamba toka nianze kusoma na kuandika hizi forum, nili-conclude long ago kuwa ni Bob Mkandara tu anayemjua Free, au "Mchagga", kama tunavyomwita kama ninavyomjua, kwenye hili la Freeman kwa kweli sina zaidi la kuongeza maana siwezi kwenda deep zaidi na kutoa mengine, ila nitakubaliana na wewe kuwa simfahamu na kwamba sio CCM, maana maneno yako kama walivyosema wazee wengine hapo ni mazito sana,

isipokuwa I will get back to you soon kwenye mengine yote, isipokuwa Freeman.

1.Sijui hilo la independent president limetoka wapi,lakini nafahamu some few successful politicians who stood as independents and have so far farred well in politics eg the current Mayor of London ambaye before re-joining Labour alikuwa an independent.Hivi ndugu yangu,hao wagombea tulionao huko kwetu sio binafsi in the real meaning of the word,na wanatumia tu tiketi ya chama kupata nafasi hizo wao binafsi?Labda nikuulize swali dogo,iwapo kuna wagombea wawili:mmoja independent na mwingine wa chama flani,kigezo chako cha kumpa kura kitakuwa ni nini hasa?Au wewe ndio wale mnaopigia kura hata watu wabovu kwa vile tu wanatoka chama flani?Asilimia 38% ya Wamarekani wanajihesabu wenyewe kama "independents" wakati wa kupiga kura,yaani hawana affiliation na chama cha siasa,kwao cha muhimu ni ubora wa mgombea.Political apathy hapa UK inahusishwa kwa kiasi flani na wananchi hususan vijana kupoteza faith in politcal parties and processes.Pengine kwa hawa wenzetu mgombea ni muhimu pengine kuliko chama anachotoka ni kwa vile hapa ni nadra kuona mambo kama ya akina Lowassa kuwaita wabunge wa CCM kila wanapotishia kutopitisha madudu ya mawaziri flani bungeni (kwa lugha nyingine,chama kinawapatia wabunge uhuru mkubwa wa kuwakilisha majimbo yao rather than kuwa watumwa wa chama hicho).Mwajiri wa Mbunge au Rais ni wananchi,ila anawatumikia kupitia chama flani.Je ukiwa na uwezo,huwezi kuwatumikia wananchi bila chama?Kwani unapoiongoza familia yako unahitaji chama? (that's uongozi in its simplest form)

2.Huku kwa wenzetu,vyombo vya habari vina tabia ya kum-endorse mgombea flani au chama chake wakati wa uchaguzi.Kwa mfano,katika Uchaguzi uliopita wa Rais wa Marekani gazeti la Washington Post lilitamka bayana kuwa linamsapoti John Kerry,kama ilivyokuwa kwa Boston Globe.Kwa hapa UK,The Sun lilitamka bayana kuwa linamsapoti Tony Blair dhidi ya Michael Howard katika Uchaguzi Mkuu uliopita.Hata hivyo,baadhi ya vyombo vya habari huwa "vinahisiwa" kuegemea upande flani japo havijatangaza msimamo wao.Kwa mfano,katika Uchaguzi uliopita,FOXNews ilikuwa ikidaiwa kumpendelea zaidi Bush kuliko Kerry huku CNN wakilaumiwa kuelemea kwa Kerry.Huko nyumbani hali ni tofauti.Dokezo pekee kuhusu sera za gazeti ni nani anaelimiliki.Kwa mantiki hiyo,haihitaji digrii ya rocket science,kutambua kuwa sera za Uhuru na Mzalendo ni kuitetea CCM kwa nguvu zote,na Daily News na Sunday News wana jukumu hilohilo kwa serikali (tofauti na hapa ambapo BBC imekuwa "mwiba" kwa bosi wake,yaani serikali).Pia TVT na RTD ni hivyohivyo kama ambavyo Redio Tumaini (sijui bado ipo) inavyowajibuka kwa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki DSM.Sasa,ukija kwa Tanzania Daima,Mwananchi,Mtanzania,Majira na magazeti ya Mengi,unaweza kuwa na wakati mgumu kukimbilia kusema gazeti flani linafanya kazi kwa influence ya CCM,kwa vile hayamilikiwi na CCM.

Pia,inabidi ufahamu kuwa "influence" inaweza kuwepo kwa ridhaa au bila ridhaa ya chombo cha habari,au ikawepo kwa makubaliano au bila chombo cha habari kujua kuwa kiko influenced na chama flani.Vipo vyama vya siasa vinavyoingia mikataba na vyombo vya habari,na vipo ambavyo vinatumiwa na vyama vya siasa bila vyenyewe kufahamu eg pale chama cha siasa kinapopandikiza waandishi wa habari kwenye chombo cha habari.Hapa hatujazungumzia vyombo vya habari vinavyojipendekeza kwa manufaa yao binafsi.

Nilikuwepo huko home wakati wa Uchaguzi,na nashawishika kusema vyombo vingi vya habari vilielemea CCM.Hata hivyo, kwa mtazamo wangu,nilidhani Tanzania Daima lilikuwa likitoa coverage kubwa zaidi kwa Chadema,to the extent nikadhani gazeti hilo ni mali ya Mbowe (sina uthibitisho,who owns it).I used to like Rai,lakini unfortunately,nililikuta limekumbwa na kimbunga cha wanamtandao japo bado kuna critics kama Fr Karugendo (sijui kama bado yuko hivyo au kishamezwa na mtandao).Mwananchi ni gazeti makini,but lina connection ya Rostam na sasa hao Wakenya (Nation Group) wanategemewa kutojenga mahusiano mabaya na wenyeji wao (CCM na Serikali).Hata hivyo,pamoja na distant affiliation yake na CCM,bado limekuwa linafanya kazi kama gazeti huru kwa vile linakosoa pale linapopaswa kufanya hivyo.Nadhani vyombo vya habari vya Mengi viko at the middle of the road,

3.Unasema Mbowe hakutumia fedha alizopewa UK kwa ajili ya kampeni,sasa hizo gharama za helikopta na kampeni yake zililipwa na nani?CCM au wewe?Mwenye jukumu la kujua misaada inayotolewa kwa chama imetumikaje ni wanachama wa chama husika,wewe mkereketwa wa CCM hayakuhusu.Mbona hujahoji mamilioni yaliyochangwa kwa kampeni za CCM yametumikaje?Quality Group ya Manji ilitoka shs milioni 500 kwa kampeni za CCM,nani anajua zilivyotumika?Kama mgombea mmoja wa CHADEMA alijitoa kama ishara ya malalamiko yake dhidi ya msaada huo wa fedha kutoka UK,mbona akina Slaa na wengineo hawakujitoa?Huyo aliyejitoa alishajua atashindwa kwenye uchaguzi,na hilo la fedha lilikuwa kisingizio tu.Rafiki yangu flani ambaye amefanikiwa kukwaa ubunge kupitia CCM aliwahi kuniambia kwamba iwapo mgombea atatategemea kushinda ubunge kwa msaada wa chama KIFEDHA basi bora asingegombea in the first place.Pia utafiti wa Dr Max Mmuya na Dr Amon Chaligha kuhusu vyama vya siasa na demokrasia Tanzania unaweza kukupa mwanga zaidi wa ninachokieleza hapa.Kiuchaguzi,Tanzania ya leo ni kama Marekani,unahitaji fedha za kutosha sana kabla hata hujajiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kupitishwa ngazi ya mtaa,acha hiyo ngazi ya ubunge au urais.Kwa vile Freeman ni rafiki yako,jaribu kumdadisi kuhusu hilo la matumizi ya fedha (binafsi au za marafiki/wafadhili) katika kugombea

4.Kuna ukweli mmoja ambao unafahamika katika siasa zetu mpya za vyama vingi barani afrika:CHAMA TAWALA HAKITOLEWI MADARAKANI KWA KUSHINDWA NA VYAMA VYA UPINZANI BALI KINATOLEWA KWA KUSHINDWA CHENYEWE KUTETEA NAFASI YAKE KUBAKI MADARAKANI ie kukosea kupanga karata zake vizuri (eg kumteua Kitwana Kondo kuwa mgombea Urais badala ya JK...unajua kabisa nini kitatokea hapo:).Watawala wetu wa Kiafrika wanatumia sana taasisi za dola kuhakikisha chama tawala kinabaki madarakani...kuikumbatia idara ya usalama na taasisi za uchaguzi.Hadi taasisi hizo ziamue kuvunja uhusiano na chama tawala basi ujue kuna utoto flani umefanywa ndani ya chama,au mgawanyiko ndani ya chama tawala eg KANU kule Kenya.

Nikipata wasaa tutaendelea kujadiliana.Japo sina interest sana na malumbano ya kisiasa esp CCM vs Others ila huwa najiskia nina wajibu kuzungumzia maswala yanayohusu ustawi wa Taifa letu "changa" (miaka 40 bado changa?!!)
 
Mlalahoi,
Mchango wako bomba! Kwa mtaji huu forum inaelekea pazuri sana.
 
Mimi tibwilitibwili nasema maneno yako ni mazito .Ungalikuwa kwetu Songea leo nakupa mke tena toka kwa rafiki yaani mke wa rafiki nakupa wewe japokuwa wewe hutapenda lakini heshima kuu hii . Hapa hapa wa kunyumba nasema maneno mazito haya na CCM wameeelewa kwamba tumesha amka bwana .Ndiyo si kama zamani na iko siku tutapata mwanya kuhubiri Injili hii kwa uwazi .Tina nkuu mpya wa Uchalama wa Tanzania sasa sijui ataelezwa kwamba hila twazijua na iko siku tutawahoji kama chi chichi bachi ntoto wetu .Ndiyo bwana Mbwai mbwahi tu kwa nini ?
 
Jasusi said:
Mlalahoi,
Mchango wako bomba! Kwa mtaji huu forum inaelekea pazuri sana.

Asante mzee Jasusi,nyie ndio mmetuonyesha njia kwa kutuletea forum hii maridhawa.
 
tibwilitibwili said:
Mimi tibwilitibwili nasema maneno yako ni mazito .Ungalikuwa kwetu Songea leo nakupa mke tena toka kwa rafiki yaani mke wa rafiki nakupa wewe japokuwa wewe hutapenda lakini heshima kuu hii . Hapa hapa wa kunyumba nasema maneno mazito haya na CCM wameeelewa kwamba tumesha amka bwana .Ndiyo si kama zamani na iko siku tutapata mwanya kuhubiri Injili hii kwa uwazi .Tina nkuu mpya wa Uchalama wa Tanzania sasa sijui ataelezwa kwamba hila twazijua na iko siku tutawahoji kama chi chichi bachi ntoto wetu .Ndiyo bwana Mbwai mbwahi tu kwa nini ?

Mzee Tibwilitibwili,

Natamani ningekuwa huko "kunyumba" Songea...asante kwa comments zako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom