Ole wenu CHADEMA!

Kwasakwasa,

Hebu acha hizo, wewe "shusha nondo" hapa ueleweke, kama huna nondo nyamaza. Hebu soma posts za Wazee kama Kyoma, Rufiji, Mnyika uone wanavyojibu hoja na utaelewa nini maana ya hii forum. sio kuzidi kushambulia watu
 
FK
Unajua umegusia kitu ambacho mimi mwaka 2001 kwenye forum ya BCStimes nilikiongelea kuhusu hawa wapinzani. Nakumbuka nilisema wapinzani kama kweli wapo kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii, kuna mambo ya muhimu ya kushughulikia. Mojawapo ni katiba. Niliwashauri wasusie uchaguzi. Tena hapo wangepata support ya nguvu kutoka kwa wote ambao ni enlighetened kama walivyo humu kwenye forum na kwingineko.

Kuacha kwao kuelekeza juhudi kwenye mambo ya maana ndio kunawafanya kushindwa uchaguzi kabla ya kura kupigwa.

Mzee ES
Umetoa point ya maana kwamba kuwa na uchungu kwa maendeleo ya taifa sio lazima kwenda upinzani. Mwelekeo wa wapinzani wengi kama sio wote ni polarization politics: Kujitenga na kulaani upande mwingine. Natumaini pole pole wataelewa kwamba hakuna maendeleo yoyote yatakayopatika kwa fikra za namna hii.
 
Kwasakwasa,

Binafsi naamini kuna vichwa ambavyo vinaweza kuleta matatizo kwa chama tawala. Ndugu yangu naona umepitwa na mengi sana, maanake unafanya kurudia yaliyokwisha jadiriwa na kila mara vijiwe vyetu vimefungwa wakati issue nzito inapojadiliwa. Kijiwe hiki ni tishio kuliko vyama vya vyama upinzani. Na utakluja nambia JJ atakuwa kiongozi mzuri sana na tishio kubwaaaa!.

Kwasakwasa, wenzako kila mara huwa tunaondoka na mikwaruzo kama hii, na tumekuwa tukiamshana pale mmoja wetu anapotoka nje ya mada lakini mara nyingi kama sii zote tumekuwa na mwisho mzuri sana kwa kufikia maamuzi na kupata dawa ya mapungufu..

Sasa ebu angalia kwa ukaribu tu, Invincible aliwambia Chadema kabla kabisa ya uchaguzi kuwa katiba mbaya na tulijadili swala hili kwa marefu na mapana hadi kufikia mada ikasimama bila kuendelea. Wapo waliokuwa wanaamini kabisa kwamba Chadema wangeshinda ndani ya katiba hiyo mbaya na nakumbuka Mzee Es alisema over my dead body!... pale watu wakaja juu wakitaka kujua kamaanisha nini hali Chadema ngangari, sijui mbadala na kadhalika. Haya maneno kuhusu Mbowe tunayarudia tu yaliisha ongelewa mwaka jana mwezi wa nane tena kwa mwezi mzima.

Hakijaharibika kitu kabisa hapa kwasakwasa, wewe mnazi lakini wanachama halisi wa Chadema watayafanyia kazi malumbano haya. Mzee ES alishawahi kusema mengi mazito kuhusu JK, nakumbuka hata tishio lake la ku-cross over kwenda Chadema kama hatachaguliwa. Kuna wana CCM wenyewe ndani ya mjadala huo walianza kuvimba wakaja juu lakini mwisho wake walikuja amani baada ya ukweli kujitokeza. mara kibao tumejikuta kila asemalo kweli hutokea hata kama kaongeza chunvi. na hakuna mboga inayopendeza mdomoni kama haina chunvi maadam isizidi tu. Hutaki kula nawa mikono futa midomo wengine bado tupo. (sijatukana). usinielewe vibaya.

Sisi wengi wa kusahau, Kila Mzee akianzisha vagi jingine vumbi kali hutokea utadhani mechi ya USA na Italy, lakini mwisho wake huwa salama...kwani sote tumepata somo.

Haya tunarudia tena ikiwa KATIBA itabaki kama ilivyo vyama vyote vya upinzani hawatakiwi kuchukua fomu za kugombea. Acheni CCM wenyewe wapiganie na tuone kama kweli dunia bado itakuwa nyuma yao.
 
Man! go home!

(1). Mazingira magumu ya serikali yanawafanya upinzani wasiwe wanavyotakiwa? What a joke? Kule Kenya Moi aliwapa mazingira safi? Kina Mandela walipewa mazingira safi na makaburu? Chiluba alipewa mazingira safi na Kaunda? Mlitegemea CCM, chama kilichotawala for the last 44 years kitawapa madaraka kama kununua samaki sokoni? Je CCM ilimuwekea JK mazingira mazuri? Sasa umafiya ulikuwa wa nini?

(2). Serikali ya nchi yoyote duniani haiwezi kutishwa na agenda za upinzani zisizokuwa na kichwa wala miguu, tena za kuwekwa chini na magazeti kama Mtanzania, ambalo toka lianzishwe ni habari za Freeman tuuuu jinsi alivyo tishio kwa CCM, na walioonewa kwenye uchaguzi wa rais wa CCM Dodoma, basi halina lolote la muhimu kwa wananchi! Rai ndio kabisaaa, wakimnyima tu uraia, na kumtoa kwenye kampeni za rais ndio ananza kuandika hoja muhimu, wakimpa tayari ni kusifu tuuuu, Mengi na IPP ndio hivyo akithubutu tu atalipa madeni yote anayodaiwa na makaburu, na upinzani wenyewe ndio hoi bin taabani, halafu mnashangaa wananchi wanampa JK kura 80%, ni kwa sababu upinzani bado hawajapa sababu ya kuchagua tofauti, sio mazingara magumu, hayo yalianza pale tu upinzani ulipoanzishwa na kumbuka ulianzishwa baaada ya kupewa ok na Mwalimu, muanzilishi wa CCM, sasa mlitegemea nini? Hawa kina Mrema walipokuwa wanakwenda kujikomba kwa Mwalimu, walikuwa wanategemea nini? Kuwa Mwalimu na CCM watawapa tu power bureeee? bila kutoa jasho?

(3). Katiba ya nchi yetu ni mbovu na ndio mwanzo wa upinzani kuishiwa nguvu, great! Je upinzani wamefanya nini kukabiliana na hili tatizo la katiba? Look at CCM kila siku wana mapya ya kuwakandamiza upinzani na kuendelea madarakani, yaani upinzani hamuwezi hata kugomea kupigia kura miswaada mbuzi? Hamuwezi hata kukataa kuongezewa hela bila sababu, shillingi millioni 10 za kununulia magari? Hivi kweli mngezigomea hizi hela si angalau wananchi wangeshituka kuwa na nyinyi mko bungeni?? Hii issue ya nyongeza za marupu rupu ya wabunge imekufa only kwa sababu baadhi ya viongozi wa CCM waliikataa, lakini sio kwa sababu ya upinzani, WHY na hizi ndio hasa issues ambazo tunazisikia dunia nzima zikiwapa upinzani ujiko? Juzi umesikia huko Nepal upinzani walivyoweka mguu chini, mpaka mfalme analia kwenye TV!

((4). Yes, ni mimi niliyesema kuwa sitajiunga na hii forum kwa sababu ni ya Idd Simba, nilisema na baadaye nikajiunga nayo na ninaweza nikatoka wakati wowote kwa nafasi yangu, na sikuvunja sheria ya nchi au ya hii forum? now what is your problem? Sasa wewe mwenye hii forum mbona sijaliona jina lako toka niingie humu? Yaani nyinyi upinzani hamna jipya kazi kulia tuuuuuu, sasa hata unalia eti kwa nini nimeingia hii forum, tena wewe ni mpinzani wapili kuuliza kwa nini nliingia hapa, maana yake ni kwamba kuna mnaotaka hoja za kubembelezana, yaani hamuwezi kuacha hiyo tabia ya kulia lia tu, mimi nilifikiri ungekuwa na shukrani kuwa hii forum ambayo posting zilikuwa kwa siku mbili au tatu sasa ni kwa masaaa, mpaka kwa dakika mpaka wakati mwingine posting zinapandana, sasa nenda huko kwingine amabako hatupo uone, kuna moja niliingia kuchungulia tu yaani posting ya mwisho ilitumwa January! kuwa na shukrani kijana, huwezi malumbano kaa pembeni waachie wengine wanaoweza,

Ukweli utaendelezwa kuwa upinzani bongo ni a big joke, leo 2006 hakuna nchi duniani rais anachaguliwa kwa kura 80%, hata China ambako hakuna upinzani bado rais hapati kura 80%, just simple as that, hakuna! Maana yake ni kwamba upinzani ni hakuna, maana yake ni kuwa viongozi wa upinzani bongo ni CCM watupu na wafanya biashara, Yes! that is exactly what is means! fungeni virago and go homee! Upinzani gani? Hawa kina Morales, Vincente Fox, unajua mambo waliyoyapitia mpaka kuwa marais toka upinzani? Kina Chavez wameshafungwa jela kwanza ndio wakawa rais sio kulia lia tuuu na kulaumu wanabodi wasiokuwa upande wako wanatafuta nini hapa, jibu mapigo kijana hakuna watoto hapa, unafikiri kwa nini BCS ilifungwa, Mzee Mwanasiasa si uliwahi kuuliza kule BCS kuwa hizi forum zitaweza mitulinga ya kina ES?, yes here I am halafu siendi kokote bro, it is tough!
 
Waungwana,

Hii mada nimejaribu kuikwepa kwa muda, ila nadhani itabidi nami niweke senti zangu mbili hapa. Kwa kuanza tu napenda kutangaza kuwa mimi siyo mwanachama wa chama chechote kile na ninachoandika kitakuwa ni nionavyo mimi na siyo kutokana na chama changu cha siasa (kwani sina).

Nimefuatilia kwa muda ila ninasikitika kusema kuwa Mzee ES anavyosema kuna ukweli mkubwa zaidi. Naamini kuwa kwa kipindi hiki hakuna chama cha upinzani ambacho kinaweza kuitoa kamasi CCM !!....Chama kama CUF kingeweza ila kampeni kali ya CCM kukigeuza kuwa ni cha kidini na pia kutokea kwa JK kulikimaliza kabisa. Chadema nimekuwa nakifuatilia kwa karibu na nakubaliana na sera na mengi wayasemayo..na inaelekea kuwa wanajuwa wakifanyacho na hawana dhiki ya kununuliwa kirahisi au ya kupewa senti kumi na kunyamaza kama baadhi ya wabunge au wagombea wa vyama vingine vilivyomalizwa nguvu na CCM.

Kama chama pekee cha upinzani, CCM weshagundua kuwa Chadema ndicho chenye mikakati migumu na watu waonao mambo na mbali, hivyo basi wanajaribu kwa karibu kuwaweka upande wao ili wajaribu kula nao sahani moja...na hicho ndicho kitakachoimaliza Chadema kama upinzani. Tatizo la ushirikiano wa Chadema na CCM ndiyo utakaokimaliza kwani U KGB na umafia wa CCM ndiyo unaokifanya kiwe karibu na Chadema na watakapowapiga kombora itakuwa kama mambo ya NCCR, Labour Party na hata CUF. Lengo la CCM ni kukisambaratisha kwani kama nilivyosema weshakiona kuwa ni tishio. Binafsi nia uhakika kuwa weshapandikiza mtu huko, na kama hawajapandikiza mwana CCM ndani ya Chadema watatafuta njia nyingine madhubuti ya kukisambaratisha, na binafsi nadhani muda si mrefu kabla hawajateua mwana Chadema kwenye posti ya serikali, (ila nadhani hii itatokea wakishindwa mbinu nyingine zote).
 
Nimefuatilia hii mada kwa muda na kusema ukweli nimesikitishwa sana na baadhi ya wanabodi wanavyojaribu kuupinda ukweli . Mzee ES umetumia muda mwingi sana kuusema upinzani bila kuangalia upande mwingine wa shilingi, Umezungumzia masuala ya ruzuku na jinsi wapinzani wanavyogombania na kusema ukweli nimecheka sana kwani imeonyesha ni jinsi gani ulivyo close minded!

Tofauti na vyama vya upinzani CCM ina source nyingi sana za mapato na nyingine atuzifahamu wanazijua wenyewe lakini mimi nitazungumzia zile ninazozijua , Kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vyingi CCM kilikuwa ni chama pekee na nadhani wanabodi bado mnakumbuka ile slogan " Chama kimeshika hatamu" . Wazazi wetu walilazimisha kutoa michango mbali mbali kwa CCM bila ya ridhaa zao , CCM ilitumia hela hizo kujenga vitega uchumi mbali mbali kama viwanja , kumbi za mikutano n.k . Hivi vitu vyote kwa sasa ni mali CCM ila in reality vinatakiwa kuwa mali ya nchi na sio CCM.

Wanabodi vile vile ni muhimu kujua ya kuwa Tanzania iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila ya kujiandaa na hii ilitokana na pressure toka kwenye financial institutions, watanzania wengi awakupenda kabisa mfumo wa vyama vingi lakini kutoka na busara za mwalimu Nyerere leo hii tuna hivyo vyama ! sasa kama wananchi wengi hawakuandaliwa kuelewa manufaa na mabaya ya vyama vingi then what do you expect ? Mwaka 2000 nilikuwa Geita kipindi cha uchaguzi na kusema ukweli nilishtushwa na kampeni zilizokuwa zinafanywa na CCM huko , walikuwa wanaonyesha picha za Rwanda na kuwaambia wananchi that is what they should expect once wapinzani are elected . Kwa hiyo unapozungumzia 80% ya ushindi wa kikwete kuna mambo mengi sana ya kuangalia kwani kampeni za CCM mijini na vijijini ni tofauti sana.

Mzee ES , Katiba yetu pia ilikuwa designed kukandamiza upinzani ! katiba inasema ya kuwa majibu yakishatangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi hakuna mtu wala chombo chochote cha dola kinachoweza kutengua matokeo hayo , ili ni tatizo kubwa na inaonyesha ni jinsi gani tusivyo na check and balance katika serikali yetu .kitu kingine ambacho bado sikielwi ni uteuzi wa hii tume ya uchaguzi , wajumbe wote wa hii tume wameteuliwa na rais wa CCM kwa maana nyingine mwajiri wake ni serikali iliyo madarakani ............
 
This discussion has taken sides na mimi ninanpenda kujadili mambo ya Nchi kwa faida ya Taifa sasa naona mmeacha kujadili issues naongelea mapenzi yenu kwenye vyama .Najua Mzee Es utanisamehe kwa hili lakini I was in Arusha , Mwanza , Mara , Singida niliona mambo ya ajabu kwamba baadaye nasikia CCM walikomba kura zote .Mahita ndiyo maana anasifiwa na of course vijana wa Usalama pia .Walifanay kazi ya ajabu ya kupata 80% kwa ajili ya CCM mimi bado siamini katika siasa hizi.Nakumbuka Mkapa na Shein kwa muda tofauti walifika Musoma na Tarime walipata kichaa maana walichoa ambiwa si walicho ona .Hawakuwa na watu na FFU wakaanza kuwapiga wananchi bila ya sababu .Mimi nataka kusema kwamba CCM haikushinda kwa 80% na kama ni kweli basi leo hii maneno ya mbinu za ajabu hadi kuwapinga wagombea binafasi kwamba CCM akina JM na AK wanahangaika na sasa Serikali inashika bango kwa rufaa tusingaliyaona.Kuna uchafu mwingi ulitumika kuiba kura na kuwanyima wapinzani kura zao za haki .Nimeshudia baadhi ya maeneo.

Hadi sasa pale Musoma Mjini Matayo hatakiwi na watu bado wamegawanyika .Arusha mjini TLP walishinda kijana kaporwa ushindi na akapozwa kwa mamilioni ya pesa kaacha kukata rufaa kupinga matokeo.Arumeru juu ni balaa na kwingineko ambako wasimamizi wa Vituo walitanga matokeo kwa nguvu tu .Matukio ni mengi yalifanyika ndugu Es .Sasa tuache mabishano ya kiupenzi wa Siasa tuongelee mwelekeo wa Tanzania
 
Mugishangwe na Rufiji
Bado kabisa mnababaisha hapa. Upande wa shilingi hii sio matokeo ya JK huko mikoani. Navyoelewa mimi kama sikosei mlinambia kwamba kura za wabunge hazihusiani kabisa na matokeo ya mgombea urais. Kwa hiyo Mkapa na Shein walikwenda Musoma kuuza wabunge ambao hawakukubalika. Na hata JK mwenyewe alipotembelea mikoa alipedwa yeye na kuambiwa wabunge wake hawakubaliki. Yes CCM walitumia kila mbinu kuhakikisha wabunge hao wanapita.

Je, wapinzani wamefanya nini kupinga matokeo hayo. Hata CUF mwaka 2000 walisikika wakilalamika na hadi leo madai yao yapo ktk vitengo vya haki za kibinadamu. Madai ya Mtikila miaka ya nyuma yanajulikana na hata siku moja Mtikila hajafunga urafiki na viongozi wa CCM kwa sababu hakuna haki. Sief Sharrif kwa miaka ya kwanza alikuwa kweli mpiganaji hodari, mjasiri na alikubali kwenda jela kuhakikisha haki inasimama lakini kama Mrema alipopewa nafasi kwa maslahi yake na sio ya wananchi, usaliti wake ulikuwa wazi.

Sijaona kiongozi mwingine yeyote akichukua nguvu kama hiyo tena. Mbowe anaweza kuwa tishio kwa CCM lakini hadi leo hii kashindwa kusimama kutetea wanyonge kwa vitendo isipokuwa politics.

Upande mwingine wa shilingi ni ule utakao onyesha nguvu yake na chama chake ktk kutetea haki ya wananchi wa Musoma, Tarime, Arusha na kadhalika walioibiwa kura zao. Tumeyaona Zimbabwe, Malawi, Zambia na Kenya ambako wote waliibiwa sawa na sisi lakini sii Tanzania, wapinzani wana fanya urafiki na viongozi wa CCM wakati mbaya kwa wananchi.
 
Mzee Rufiji,

Kama watanzania hatukuwa tayari kwa mfumo wa vyama vingi, isipokuwa kwa pressure ya International Finance Institutions, na kwa kwa kuwa Katiba bado ina kasoro kuhusu maelekezi ya uchaguzi mbali mbali then
1.UPINZANI HAKUNA BALI NI KIVULI
2.KWA KUWA UPINZANI NI KIVULI NDIO MAANA HATA HOJA YA KUSUSIA UCHAGUZI KUTOKANA NA KATIBA MBOVU KWAO NI MWIKO, kwani ni kama hawaioni. Kama Katiba ni mbovu kwa nini ushiriki ktk uchaguzi nahali ukijua utashindwa!!!!!

Kuna wakati Mzee Rufiji umeongea jambo la BUSARA na kama Upinzani wanaliona hilo basi leo tungekuwa tunasema maneno mengine. Uliwashauri wapinzani wasimamie issue ambazo siku zote zitawafanya CCM wawe kwenye defensive side, Issue ziko nyingi sana za kukifanya chama tawala kihahe huku na kule kujitetea (moja wapo ni issue za vitega uchumi vya wananchi, Mikataba FEKI nk nk. Still hilo HAWALIONI KWANI WAO NI VIVULI. naweza kusema nchini kwetu kuna "GHOST" la upinzani na wala hakuna upinzani wa kweli.

Sherrif kurudishiwa marupurupu tu, kimyaaaaaa, wengine ndio duuuhh kila mara kugombana na Tendwa
 
Upinzani will die a natural death, lets hope true upinzani will emerge with first elections that will allow independent candidates!
 
Wanabodi ,

Ishu ya matatizo ya upinzani ni ngumu sana na sio nyepesi kama watu wananvyofikiri . Mwaka 2000 katika uchaguzi wa zanzibar baadhi ya masanduku ya kura yalipelekwa kituo cha polisi na yalikaa pale siku mbili kabla ya kuhesabiwa na wakala awakuruhusiwa kabisa kuwepo kwenye hivyo vituo ! sasa nani wa kulaumiwa hapa ?

sasa watu wanasema wapinzani wagomee uchaguzi , ukishagomea uchaguzi then what next ? unajua kuna kipengele ambacho kinampa nguvu msajili wa vyama kukifuta chama kama akitashiriki katika uchaguzi ? na usiposhiriki katika uchaguzi watapata vipi wa wakilishi katika bunge ? nadhani watu tunajump to conclusion without thorough analysis on the matter. Na once ukigomea uchaguzi which message are you going to send to your loyal supporters ?

Sijaona mtu hata mmoja aliyegusia tume ya uchaguzi , tume ambayo wajumbe wake wote ni wana CCM " ingawa wana pinga hilo " , na wanachaguliwa na Rais wakati huo huo Rais anaweza kuwafukuza kazi wakato wowote ! Don't you think they are going to be biased ! tatizo ni kuwa wanabodi wengi wakishasoma theory zao wanataka kuzifanya practical .....sasa wapinzani watashinda vipi .
 
Mzee Es,
Nakubaliana na wewe, hii inaonyesha wazi watu hawaelewi na wala hawatakuja elewa maana. Tunachozungumzia hapa. masanfuku kukaa kituo cha polisi kwa siku mbili hali matokeo yanatakiwa kutangazwa usiku huohuo!
Je CUF walifanya nini kuhakikisha masanduku hayo yanahesabiwa na kwa nini mahakama haikuhusishwa?... mtasema katiba haisemi hivyo ama nguvu ya dola!
Bado jibu lahoja hii ambayo ni upande wa pili wa sarufi hii.
Head:- inasema maonezi ya CCM
Sisi sote tunakubali na ili tupate thamani ya hii sarufi tutazame upande wa pili?
Tail:- Wapinzani ni Kivuli kama alivyosema Ogah ktk hoja zake mbili hapo juu.
Hamkubaliani na picha hii hali dhahiri inaonyesha wazi kwamba bila marekebisho hakuna ushindi.
 
Maana watu wamesahau kabisa siasa za Tanzania , Mahakama itafanya nini zaidi ya serikali ? Nadhani wanabodi wengi wamekaa nga'mbo kwa muda mrefu sana kwa hiyo wamesahau kabisa mambo ya nchini na itakuwa ni vigumu kuwaelewesha.

Mbona hamtaki kuzungumzia tume ya uchaguzi ?
 
watu wamesahau kabisa siasa za Tanzania , Mahakama itafanya nini zaidi ya serikali ? Nadhani wanabodi wengi wamekaa nga'mbo kwa muda mrefu sana kwa hiyo wamesahau kabisa mambo ya nchini na itakuwa ni vigumu kuwaelewesha.

Mbona hamtaki kuzungumzia tume ya uchaguzi ?
 
Mzee Rufiji,

1.Hao supporters wa upinzani unaowasema, wako wapii??, ukiachilia mbali Pemba kutokana na historia, sehemu nyingine Tz yetu hii hakuna, yote hii ni VIINI MACHO VYA VIVULI VYA UPINZANI. taratibu naanza kuamini maneno ya baadhi ya wanabodi hapa kuwa wanaojiita wapinzani sehemu kubwa ni CCM, kwani CCM inawezekana ilipandikiza hiki kiini macho cha demokrasia ili kuridhisha mataifa makubwa na hizo Bank zao.

2.Hakuna mtoto hapa asiyejua utendaji kazi wa serikali yetu, tena inawezekana walio ng'ambo wakaijua vizuri zaidi ya walio nyumbani. mahakama ipo na kazi inafanyika endapo watu serious wa issue wakiwepo.

3.Hiyo tume ya uchaguzi unayoisema hakuna anayekataa kuw aina walakini. What is the solution then?, utagundua kuwa utarudi kule kule kwenye katiba.

However,pamoja na kusema yote hayo hapo juu, hata leo hii ukitisha kura za maoni Tanzania yote juu ya Katiba, i have a doubt kuwa wananchi kwa propaganda za CCM hawatasupport mabadiliko ambayo ninyi wachache mlioelimika mnayataka.

What do to then:......Mtuelimishe sisi wananchi.
 
Rufiji na Kwasakwasa,

Mimi ni CCM damu(narudia), tunachofanya hapa ni kujaribu kusaidia Tanzania yetu, na kwa mtazamo wangu na wa ES (CCM naye) na Mkandara, Ogah na Invicible tunataka upinzani wa kweli kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Nini kifanyike ili muwe wapinzani wa kweli ndio tunataka mseme tujadili.
First and foremost ni kubadili katiba. Mfanye nini ndio tunataka tujadiliane.

Ila wewe mwenzetu umeng'ang'ania UWEZESHWE!! ebo!! we unaweza kumwezeshaje mshindani wako (chukulia kwenye michezo) ashinde?, hapo mkuu haukufikiria kabisa!!!

Badilisha topic tukusaidieni mawazo

Mzee es Safi sana juu hapo (sio ya mwisho)

FD
 
Fikiraduni ,

i don't want to waste my preciuos time urging with you , cause you are totally out of touch with reality .........anyway your name speaks for itself.
 
Tuyaache kama yalivyo naona mada hii imekwisha natumaini Chadema na wapizani wengine wataifanyia kazi, hili ndilo ombi letu.
Ashakum sii matusi!
Kuna kitendawili kisemacho..
Who is the best gynecologist?.... Jibu lake ni
Chooo.
Maanake kisha ona kila sura na kuponya wengi tunapopunguza oil na kusafisha engine. :lol: :lol:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom