Elections 2010 Ole wao Wapinzani Mwaka 2010

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Ole wao wapinzani mwaka 2010
• Mambo ya Ndani Kuajiri askari wapya 7,000 kukabili vurugu za uchaguzi

na Salehe Mohamed, Dodoma


SERIKALI inatarajia kuajiri askari 7,000 pamoja na kununua magari na vifaa vya kisasa, yatakayotumika na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa ajili ya kukabiliana na vurugu wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, alisema hayo jana bungeni wakati akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010.Huku akishangiliwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Masha alisema Jeshi la Polisi lilianza maandalizi hayo tangu kipindi cha mwaka wa fedha wa 2008/2009, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kuimarisha ulinzi wakati wa uchaguzi.

“Kuanzia mwaka 2008/2009, Jeshi la Polisi limeanza mikakati ya utekelezaji wa kuimarisha ulinzi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu, utakaofanyika mwakani,” alisema Waziri Masha.

Kumekuwa na vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu, hasa visiwani Zanzibar ambapo mwaka 2001, zaidi ya wafuasi 34 wa Chama cha Wananchi (CUF), waliuawa walipopambana na askari polisi, waliokuwa wakitawanya maandamano ya wafuasi hao, wakipinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais Amani Abeid Karume.

Mwaka 2005, serikali iliingiza nchini gari la maji ya kuwasha ambalo lina uwezo wa kurusha maji hayo umbali wa zaidi ya mita 100 na ndilo lililotumika kuzima vurugu zingine za uchaguzi mwaka huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Masha, aliwatoa wasiwasi wananchi na wabunge kuwa, mchakato wa utengenezaji wa vitambulisho vya uraia, unaendelea vizuri.

Masha alisema, hakutakuwa na mizengwe au upendeleo katika upatikanaji wa mzabuni atakayetengeneza vitambulisho hivyo.

“Hakutakuwa na mizengwe, upendeleo wa aina yoyote katika zoezi hili ambalo katika siku za hivi karibuni, limeibua gumzo kubwa nchini,” alisema Masha.

Wakati Masha akiwatoa hofu wananchi, kambi ya upinzani imesema imeshangazwa na hatua ya serikali kuchukua muda mrefu kukamilisha mchakato wa vitambulisho vya uraia, huku fedha za wavuja jasho zikiendelea kuwafaidisha baadhi ya watu.

Aidha, kambi hiyo, pia imeonyesha kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya kukubali uraia wa nchi mbili.

Msemaji mkuu wa kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ibrahimu Muhammad Sanya, akisoma hotuba ya kambi hiyo, alisema mchakato wa vitambulisho vya taifa, umekuwapo tangu mwaka 2006.

Alisema katika kipindi chote hicho, hadi sasa suala hilo limeendelea kupigwa danadana, hali ambayo inawafanya wananchi washindwe kupata haki zao za msingi.

Mbunge huyo alisema, kambi hiyo inashangazwa na hadithi zinazotolewa kila kukicha na serikali kiasi cha kulifanya jambo lenyewe lianze kuwa na utata.

“Sisi tunashangazwa na hadithi za serikali juu ya suala hili la vitambulisho vya uraia kwa kuwa ni la siku nyingi na fedha za Watanzania zinazidi kuwaneemesha baadhi ya watu, kwa nini serikali haiwatendei haki wananchi?” alihoji Sanya.

Kuhusu sula la uraia wa nchi mbili, kambi hiyo, imesema kuwa haioni sababu ya serikali kutoamua kulikubali kwa kuwa ni la muda mrefu na lina faida kubwa kwa Watanzania.

Alisema katika hotuba za miaka ya 2006/2007 na 2008/2009, kambi hiyo imekuwa ikizungumzia suala la uraia wa nchi mbili, ambao ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi.

Alibainisha kuwa, majibu ya serikali ni kwamba mchakato bado unaendelea, lakini kambi ya upinzani haioni kama jambo hilo linakwenda kwa kasi inayotakiwa.

Aliongeza kuwa, nchi zilizoendelea zimekuwa zikunufaika zaidi na jambo hilo, lakini Tanzania inaonyesaha kusuasua bila kuwapo kwa sababu za msingi.

“Faida ya kuwa na uraia wa nchi mbili zipo wazi na tulishazieleza hapa kwa muda mrefu, sasa kwa nini serikali inachukua muda mrefu kwa kutuambia kuwa inaendelea na mchakato?” alihoji Sanya.

Aidha, kambi hiyo imetaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda atimize ahadi alizozitoa katika kupunguza matumizi ya serikali, hasa kwa kuchagua Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), kufanya kazi ya kushughulikia suala la vitambulisho vya uraia.

Alisema wakala wa kutengeneza vitambulisho vya uraia (NIDA) na RITA wanaonekana kufanya kazi moja jambo ambalo ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

“Kuwa na RITA na NIDA ni sawa na kupoteza fedha za wavuja jasho, ni afadhali tukawa na taasisi moja ambayo ni RITA kwa kuwa ina uwezo mkubwa wa kulishughulikia suala hili,” alisema Sanya. Kambi hiyo pia imeitaka serikali iyafanyie kazi kwa haraka upungufu, ulioainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyeonyesha kwamba kuna malipo ya sh milioni 74, yaliyofanywa bila kuwapo kwa nyaraka za matumizi hayo. Kwa mujibu wa kambi hiyo, pia kuna masurufu yasiyorejeshwa ya kiasi cha sh milioni 131, huku kiasi cha sh milioni 98, hakijakusanywa.
 
Jeshi la polisi lina siri kubwa katika kui boost CCM kila mwaka.Si hao kuajiriwa pekee kwa ajili ya ulinzi na hata Uchaguzi mkuu huwa wanatumika vibaya kuipigia CCM kura na ndiyo maana wanatakiwa kila mmoja kujiandikisha na ma RPC husimamia shughuli nzima kujua wangapi wamejiandikisha na hata wakifa bado kura zao huhesabiwa .Kulinda nje ni moja lakini kuna kupiga kura kwa ajil ya CCM .Tutasema hili baadaye maana data ziko nje sasa tunangoja muda ufike .

Siamini kama Mwema anaweza kufanya yale ya Mkapa na Mahita kwa kweli .Lakini kwa tangazo la Masha nadhani jadi itaendelezwa .
 
Huyu waziri Masha anaongelea kuimarisha ulinzi katika upigaji kura au anawatishia wapinzani kuwa polisi wa CCM wapo tayari kuwapa kibano wapinzani pindi watakapolalamika kuibiwa kura zao?
 
Amebadilika PM wetu, Amebadilika Jk, Amebadilika kila hivyo hata yeye atabadilika tu
 
Back
Top Bottom