Ole wako Tanzania, viongozi vijana ni wanafiki haswa Zitto: Posho alisema hivi...

Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.

Posho ni saratani serikali inabidi ipigwe vita. Mfumo mzima wa hizo posho ambazo wakati mwingine watu wanapelekewa attendance sheet ili wasaini na kilipwa posho ni mbovu kabisa. Kuna aina za posho zaidi ya kumi na watu wanatumia hicho kichaka kuhomola mapesa. Zitto katika hilo mimi binafsi nakuunga mkono. Endelea kuwaelimisha kuna siku watakuelewa. Penzeza elimu kwa akina Joseph Selasini, Joseph Mbilinyi, Wachungaji, Mnyika, nk ili wakuunge mkono.
 
Zitto ana akili kuliko wewe, ni vigumu sana kumuelewa alichokuwa anamahanisha. Ukitaka kujua Zitto anamaana gani kwenye huo usemi wake basi nyie lipaneni hizo mil 12, harafu zipeni jina lingine, wala msiite posho muone matokea yake.
 
Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.

Huyo aliyeleta huu upuuzi ni kibaraka wa mafisadi.Tuko na CDM hata mfanye nini.Kumbuka Zitto anaongea kwa niaba ya wanachama wote.Tafuteni uongo mwingine wa kufitinisha CDM na wananchi
 
Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema “Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho” ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema “Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana”

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.
kinyesi.
 
Haya bwana ila sio vizuri Ndio yako na iwe ndio na hapana yako naiwe hapana na ( KAMA UKIWA KIGEUGEU WA MANENO HUWEZI KUFIKA POPOTE)
 
wewee ni mbunge? huoni kama hata wewe una jukumu la kupinga kwa nafasi yako kwani zitto alizaliwa kukuonesha kila mwelekeo na kama uligundua hoja ya zitto awali ilikuwa sahihi mbona hukutoka hadharani kumuunga ili asikate tamaaa weka pia sababu kwa nini huwezi wewe kupinga hadharani? lakini pia kumbuka zitto si msaafu wa vijana nchi hii wala siye QURAN AU BIBLIA kuna vijana wengi bado tunawangazia macho

Inaelekea mwanzisha thread ni mbunge wa ccm ambao wanafumbwa midomo kuzipinga hadharani hizo posho
 
Jamani hizo ni habari za gazeti.....tuweni makini kwani gazeti hilihili ndo limeandika kua JK abariki posho za wabunge kwa kuzisaini baadae ikulu inakuja na kupinga kua JK hajafanya upuuzu km huo....so tuweni makini kwani tutahukumu ndivyo sivyo
 
Kama Zitto ni Mnafiki,wewe tukuweke kundi gani unaedai kusema ukweli lakini unaogopa kujitkeza Hadharani na jina lako kamili? USIKWEPESHE MADA,ZITTO HAPINGI NYONGEZA YA POSHO ANACHOPINGA NI UWEPO WA HIYO POSHO YA KUWEKA M.I.K.U.NDU YENU BUNGENI,IWE KUBWA AU NDOGO
 
Huyu mbunge feki hata sijui wajimbo gani, wewe unategemea zitto atetee nchi na wewe umshangilie tu pembeni hv wewe ni wale wakupewa nini?

Si unajua siku hizi ccm wanaendeshwa kwa matukio ya cdm na wako teyari kukabiliana na hoja hata kama nizamsingi ili tu cdm waonekane hawana jipya na huwa nauita ulevi wa madaraka badala ccm kutumia wingi wao bungeni kutetea maslahi ya wananchi badala yake wanatumia wingi wao kupingana na cdm na wanaposhindwa wanatumia ubabe
 
Zitto ni mnafiki hakuna anachotetea , ila anatafuta hoja za kuugilibu umma wa watanzania ,huku akiwa kwenye vikao ni unafiki mtupu anaendekeza , nimeamua kuweka wazi hapa na kama anabisha aeleze kwenye press yake anayotegemea kuifanya leo nini alisema kwenye kikao.

Mhe. sana mbunge, ahsante kwa taarifa ya kutuweka wazi kuhusu Mhe. Zitto.
Unasema Mhe. Zitto ni mnafiki, wewe ni nani kwa tabia kama hizo? Ni msema kweli au mwoga?
Au ndiyo kama unavyojiita mwenyewe mwongozo wa spika??
Naona umeamua kujiunga haraka katika jukwaa hili la busara JF ili kutuletea hii crap???
 
Kwa upande mwingine zeto kama ni ndumila kuwili vile kwa upande wa ccm yumo cdm yumo kupinga posho huku anapokea yumo yani hata simwelewi elewi vile
 
Huyu atakuwa ni wale walio bungeni kuonyesha shepu,kama Zitto mnafiki mbona wewe hukusema kuna haja ya kufuta hizo nafasi za lifti
 
Huyo aliyeleta huu upuuzi ni kibaraka wa mafisadi.Tuko na CDM hata mfanye nini.Kumbuka Zitto anaongea kwa niaba ya wanachama wote.Tafuteni uongo mwingine wa kufitinisha CDM na wananchi

mkuu ata kama unamahaba na cdm kiasi icho uko umeenda mbali sana..yani kila kauli ya Zitto ndio msimamo wa wanachama wote??sikuwai kutambua ili.
 
mkuu ata kama unamahaba na cdm kiasi icho uko umeenda mbali sana..yani kila kauli ya Zitto ndio msimamo wa wanachama wote??sikuwai kutambua ili.

Ata mie nimestuka sana,yani jamaa anasema kauli za Zito zinawakilisha wanachama wote wa cdm..ili jipya!
 
Mleta hoja anaweza kuwa na upungufi(na nikweli anao)...
Lakini hoja yake ina maana mno! Zitto mie binafsi sijawahi kumwamini toza anaanza kupata umaarufu feki!!
Toka enzi hizo hajawahi kuwa mtu wa maana wa kumpigia mfano kama mtu mwenye akili na busara.....kilichombeba kupata umaarufu ni jina lake tu.... unajua kuna majina mengine yaongeza umaarufa wa mtu hata kama hana kipaji, mfano Mwaikimba, Bujaga Kadagao n.k

Awaombe radhi na watanzania wote kwa ujumla na akiri kuwa alinafikika!
 
Tatizo wabunge wa CCM wanaongozwa na fikra za kifisadi, Zitto yuko sahii kabisa katika kuipinga hiyo posho, kwa nini mbunge alipwe posho ya kukaa wakati pale ndo ofisi yake. Mshahara hata kama utakuwa mil. 3 lakini kwa nini alipwe hiyo sitting allowance? Kama ghalama za maisha basi wapendekeze kuongezewa mshahara
 
ulichopaswa kufanya mleta hoja ni kueleza wazi msimamo wako ni upi na juhudi zako ulizo fanya ili kutekeleza hilo kusudi lako kuhusu posho

ulicho kileta hapa ni umbea tu ili tukae tumjadili mtu au lengo lako ni create anermity tu ili tumuone Zitto hafai kabisa kama hafai nani anafaa, Je ni wewe kwa sifa zipi zilizo wazi

hata kama zitto aisaliti kauli yake ya awali suala ni kujiuliza kwa nini kaisaliti ??? NI KWA SSABABU ALIKOSA USHIRIKIANO WA WAZI KUTOKA KWA WENZAKE DHIDI YA MAFISADI MLIOPO MJENGONI

That is all !!!
 
Back
Top Bottom