Ole Sendeka amtwanga konde M/kiti UVCCM!

Ndugu zangu wapenzi katika kristu, kweli tutafika kama wabunge wanaanza kuwarushia ngumi watu. Sasa ustaarabu uko wapi, halafu sababu zenyewe za kurushiana ngumi...du! kweli makubwa sasa jaribu kufikiri mtu kama huyu kutetea maslahi ya wananchi. Mtu yeyote mwenye uzalendo wa kweli hatakasirika anaokosolewa kwani kwa njia hiyo ndio anajiboresha katika madaraka yake. Kadili yangu mim huyo jamaa hafai kuwa mbunge...kwani hata wananchi watakapomkosoa atawarushia ngumi huyo kiaina, mpigeni chini huyo akalime viazi kama mikono inamuwasha.
 
Bwana angehesabu maovu yetu nani angesimama? usitoe hukumu wakati hujui hakika kilichotokea. Vita vya kisiasa ni vibaya sana mtumishi, vinakusingiziana na kila aina ya rafu, wala usimlaumu Sendeka, ni mtu muhimu katiaka vita dhidi ya ufisadi.
 
"...wala usimlaumu Sendeka, ni mtu muhimu katiaka vita dhidi ya ufisadi..."

This kind of thinking is what puts me off completely! Vita dhidi ya ufisadi gani? Amefanya nini so far zaidi ya kutoa maneno ya kuuma na kupuliza? Can somebody put on the net an audio device of whatever Ole Sendeka has ever said watu wenye akili zao wachambue content? Kwanini watu mnakuwa wepesi wa kupokea mbwa mwitu il hali mnapaswa "kuzipima kila roho?"

Supposing that this guy was mpambanaji dhidi ya ufisadi as some of you have poorly been swept to believe, ni mwenda wazimu peke yake ndiye angesapoti kitendo cha Mbunge mzima, kumtwanga makonde kijana mdogo na hata kumtishia kwa bastola kisa amemsema katika presentation yake ya haki za ardhi. (Indirectly even!) Uvumilivu wa Kitanzania uko wapi?? This is a mystery!

Tupambane na ufisadi. Lets do it 24 hours 7 lakini kwa kufanya hivyo tusihalalishe u "Dito Pile" dhidi ya vijana wenzetu na watanzania kwa ujumla. Kama ambavyo urais siyo kinga dhidi ya ufisadi, kuongea against mafisadi siyo kinga dhidi ya matendo maovu ya kuua demokrasia na kuonea vijana wanaochipukia katika siasa kisa eti wametangaza kugombea ubunge. How PATHETIC????
 
Kwa mujibu wa maelezo ya Ole Sendeka ni kwamba alijihami baada ya Millya kutaka kumdhuru.Hata hivyo suala hilo lipo mahakamani litaamuliwa huko.Lingine ni kuwa mafisadi wapo nyuma ya sakata hili kama lilivyokuwa sakata la Nape.Kikao cha mila cha wamasai kiliitishwa na Mmeru/masai Lowassa kuhusu masuala ya Ardhi.Tatizo la Ardhi mfano Monduli Lowassa angeyatatua akiwa Mbunge wa Monduli na alipokuwa Waziri Mkuu.Lakini sasa ndio anataka kutatua masuala hayo sijui alishindwaje wakati ule,halafu ukiangalia Lowassa alichangia kushabikia migogoro ya ardhi iliyojitokeza wakati wa uongozi wake dhidi ya marafiki zake na wapinzani wake kisiasa.Ukiangalia kwa upana Ole Sendeka aliingia mtegoni kuhudhuria kikao kilichokuwa na lengo la kumhujumu,unajua ukitaka kumchokoza Simba ili kujua hazira zake na ukali mzingire akose pa kupitita ndipo utaona muziki wake.Hivyo Sendeka awe makini na mitego kama hiyo,ingawa hakuna asiyejihami akitishwa na Sendeka hakuwahi kusema simanjiro ni yake mbona kwa utendaji wake anaweza kuchaguliwa Mbunge popote na kwa Chama chchote.
 
Unajua kabisa kuwa unachosema huwezi kuthibitisha. Ole Sendeka amekuwa mbunge kwa miaka mitatu sasa. Ni kipi hicho alichofanya cha ajabu? Anaweza kuchaguliwa mbunge popote? You must be dreaming my friend!
 
CCM leaders' fracas in Arusha: MP to be formally charged in court

-As Speaker awaits official word on exactly what happened

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

POLICE have now officially confirmed that the Simanjiro Member of Parliament, Christopher ole Sendeka (CCM), will be arraigned in court this week to face assault and death threat charges.

The Arusha Regional Police Commander (RPC), Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Matei Basilio, told THISDAY that the MP's formal arraignment in court is scheduled for today or tomorrow.

The RPC said the lawmaker will be charged with two counts of causing bodily harm to the Arusha regional CCM youth wing (VIJANA) chairman, James ole Millya, and making the alleged death threat against Millya.

If convicted of such serious criminal charges, Sendeka faces the possibility of serving time in jail, as well as automatically losing his parliamentary seat.

Commander Basilio said investigations into the incident were ''almost complete.''

''He (Sendeka) will be arraigned in court within the next two days,'' he remarked on Monday.

He said police are now recording statements from witnesses who were present at the function where the MP is alleged to have attacked Millya.

The Arusha regional police chief explained that Sendeka, who is presently out on bail, will be arraigned in Monduli District where the alleged skirmish occurred.

Police in Arusha recently confiscated the outspoken legislator's personal firearm days after he was reported to have attacked Millya.

It is alleged that Sendeka threatened to kill the regional CCM-VIJANA leader on Friday last week during an altercation at a Maasai tribal meeting.

Both Sendeka and Millya are Maasai tribesmen.

Sendeka was initially arrested by the police following the incident, but was later released from custody on bail posted by his relatives.

Millya told reporters after the incident that the skirmish was motivated by his (Millya's) decision to run for the Simanjiro parliamentary seat in 2010.

National leaders of the ruling CCM have opted to remain silent as the reported rift between the two regional leaders prepares to take a new turn.

The Speaker of the National Assembly, Samuel Sitta, also declined to comment on the alleged unparliamentary behaviour by Sendeka, saying his office was yet to receive official information from the police on exactly what transpired.

''I can't comment on this issue at the moment since I have not been formally briefed on what really happened...Otherwise, I have only heard and read about the matter from the media,'' he stated.

He said he would only be in a position to comment after receiving official communication on the incident.

Asked what course of action might be taken by the Speaker's Office if the MP was indeed prosecuted and found guilty of criminal charges, Sitta remarked: ''I wouldn't want to make such assumptions at the moment.''
 
Kuna watu mediocre sana humu nchini kwetu. Ndiyo maana ni rahisi kwa kila mbwa mwitu kuvaa ngozi ya kondoo na kupeta bila kushtukiwa na mtu yeyote. Yaani maneno tu yametosha kuwatongoza watanzania na akili zao kumuona Ole sendeka kuwa anapambana na ufisadi. Can any sensible person tell me why they regard him as such? Historia yake mnaijua? Huko Simanjiro mana fahamu umafia alioutenda in the past 3 years kiasi cha kuigawa wilaya katika makundi? Yeye alipokuwa mwenyekiti wa CCM wilaya alimfanyia vituko gani Parseko Ole Kone aliyekuwa Mbuge wa Simanjiro by then? Kwa kifupi chama kilichukua hatamu Simanjiro!

Elimu ndogo ya Sendeka si tatizo sana (kama alivyosema mchangiaji kuwa Mahalu ni Prof lakini kauibia) kama haitumii kumjengea infiriority complex na kuvuka mipaka ya utu yaani kufikiri. Kutokana na kielimu chake basi anaogopa kinvuli cha Millya.

Mimi nafikiri tuangalie kila jambo on its own case. Hii ya Sendeka kuijumlisha na uhasama wake na Lowassa ni kupoteza dira. There is nothing like mkono wa mafisadi in this particular thing. Ni kweli mheshimiwa Mbunge ana maadui wengi kutokana na maneno yake makali lakini hii haimpi kinga dhidi ya vitendo vyake viouvu na makosa ya jinai. Kwa mwendo huu itakuwa kila anayekemea ufisadi (kwa maneno) anajijengea aina fulani ya immunity against criminal actions iwe ujambazi, ubakaji, unajisi na kutishia kuua. Wake up my fellow Tanzanians!
Mkulu Matejoo
Kila mtu ana historia yake.
Paulo alikuwa akiitwa Sauli na under that name, wakristo wanajua nini Sauli alikuwa akifanya.

Millya anaposema yeye kumsamehe Ole Sendeka ni pale tu Ole sendeka atakapojivua Ubunge,unajiuliza kama hakuna kitu kingine nyuma ya hili sakata la kupigana ngumi hadharani.

Mchango wa Ole Sendeka na Mama Kilango katika sakata la Richmond utakumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo.

Kazi ya Mbunge ni KUSEMA hashiki jembe au msumeno na kulima pamoja na kukata mbao respectively.

Mungu ibariki TZ.
 
Malumbano ya Sendeka, Millya yaikera CCM
• Yasema ugomvi wao ni wa kijinga

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeyaelezea malumbano yanayoendelea hivi sasa kati ya makada wake wawili, Christopher ole Sendeka na James Millya, kuwa ni ya kijinga.

Mbali ya hilo, chama hicho kimesema kitendo cha makada hao wawili, ole Sendeka, ambaye ni Mbunge wa Simanjiro na Millya anayeshika wadhifa wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho mkoani Arusha cha kuendelea kuzozana hadharani, kinawaaibisha wao wenyewe wawili na si CCM.

Msimamo huo wa CCM uliwekwa bayana jana na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Taifa, Kapteni John Chiligati, katika mahojiano ya simu aliyofanya na Tanzania Daima.

Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema CCM haiwezi kujiingiza wala kujihusisha kwa namna yoyote na mzozo huo aliouelezea kuwa ni ugomvi binafsi unaohitaji utashi wa wahusika kuumaliza.

"Jamani, huo ugomvi ni wao binafsi. CCM haipakwi matope hapo. Ni ugomvi wa kijinga na chama hakiwezi kuingilia kati kwa hiyo ni suala la mtazamo tu, ni nani anayeabika kati ya chama au wahusika," alisema Chiligati.

Katika hatua nyingine, katika kuonyesha namna mzozo huo uliotokana na madai ya Millya kupigwa na Sendeka kuwa usio na maana, aliufananisha na ugomvi wa mtu na mkewe.

"Wewe au mimi nagombana na mke wangu, halafu unataka chama kiingilie kati ugomvi wetu, eti chama kinaaibika kwa ugomvi tu wa kwenye baa, hilo haliwezekani ndugu yangu," alisema Chiligati wakati akijibu iwapo hawaoni kwamba mzozo huo unaiaibisha CCM.

Hata hivyo, alisema CCM inaweza kuingilia kati ugomvi wa namna hiyo endapo wahusika hao wataleta malalamiko yao rasmi ndani ya chama katika taratibu zinazoeleweka na lazima waanzie katika wilaya yao, kabla ya madai hayo kuletwa makao makuu.

"Hadi sasa CCM makao makuu haijapata malalamiko kutoka kwa yeyote kati yao na lazima waanzie chini, sasa sijui kama katika wilaya zao wamepeleka malalamiko hayo. Hilo mimi silijui," alisema.

Chiligati alisisitiza kuwa Sendeka na Millya, wana haki ya kupeleka ugomvi wao mbele ya vyombo vya dola au hata kutumia busara kuumaliza.

Pamoja na kutoa maelezo hayo, Chiligati alikiri kuwapo kwa taarifa zinazoeleza kwamba, mzozo wa wawili hao unatokana na kinyang'anyiro cha ubunge wa Simanjiro mwaka 2010.

Katika hili, Chiligati alisema hakuna jambo baya kwa mtu yeyote kuonyesha dhamira ya kugombea ubunge, kauli ambayo ilionyesha kuunga mkono msimamo wa Millya kuonyesha dhamira hiyo.

"Ugomvi huo chanzo nakisoma kwenye vyombo vya habari kuwa ni ubunge wa Simanjiro, sasa ieleweke kwamba hakuna ubaya kwa mtu kuelezea nia yake ya kutaka ubunge, ila kama ataanza kampeni mapema, hapo ndipo penye shida," alisema.

Ugomvi huo ulioanza wiki moja iliyopita katika Wilaya ya Monduli sasa umehamishiwa katika Jiji la Dar es Salaam, baada ya wahusika hao kuamua kufanya mikutano yao na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti kuelezea hali hiyo.

Siku moja tu baada ya Sendeka anayetuhumiwa kumpiga ngumi Millya na kisha kumtisha kwa bastola kutua Dar es Salaam na kuzungumza na wanahabari kuhusu ugomvi wao huo, Millya naye alifanya hivyo hivyo siku moja baadaye.

Tayari ugomvi umeshaanza kuwagawa viongozi wa CCM na makada wengi maarufu katika makundi mawili, moja likimtetea Sendeka na jingine likimuunga mkono Millya.

Sendeka mwenyewe ameshakaririwa katika vyombo vya habari akiuhusisha ugomvi wake huo na kile alichokieleza kuwa ni mkakati mahususi unaoongozwa na kundi moja la watu lenye lengo la kummaliza kisiasa kutokana na msimamo wake wa kupambana na vitendo vya ufisadi.

Source:Tanzania Daima
 
Hatimaye Ole Sendeka atinga kortini
Hemed Kivuyo Arusha
BAADA ya kuripotiwa sana kwamba angefikishwa mahakamani, hatimaye mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka jana alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Arusha, James Ole Milya.

Tangu mapema wiki hii, kumekuwa kukiripotiwa habari kadhaa kuwa Ole Sendeka amepandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo, lakini suala lake lilikuwa polisi hadi jana wakati mbunge huyo alipofikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha akikabiliwa na shitaka la shambulio la kudhuru mwili.

Sendeka, mmoja wa wabunge machachari, aliwasili mahakamani hapo kwa gari aina ya Land Rover, Defender ya polisi na kupelekwa katika chumba cha mapumziko kabla ya kupandishwa kizimbani.

Mbunge Sendeka alikuwa amesindikizwa na watu wa kada mbalimbali waliosababisha umati mkubwa mahakamani hapo, akiwemo mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, mbunge wa jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro pamoja na wananchi mbalimbali na wanachama wa CCM kutoka mkoani Manyara na Arusha.

Akisomamewa hati ya mashitaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Kalayamaha, mbunge huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 9 mwaka huu majira ya saa 10:30 wilayani Monduli wakati alipompiga Mallya kibao upande wa shavu la kulia na kumsababishia maumivu mwilini mwake.

Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Ole Sendeka pamoja na Mallya wakiwa katika semina ya wazee wa kimila iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Monduli.

Mbunge Sendeka anatetewa na mawakili, Michael Ngalo wa kampuni ya Ngalo and Company yenye ofisi zake jijini Dar es salaam na Arusha akisaidiwa na wakili wa kujitegemea, Neema Mtayangula huku upande wa mashitaka unaongozwa na wakili Hashimu Ngole akisaidiwa na wakili Augustino Kombe.

Akizungumza mahakamani hapo wakili wa upande wa mashitaka, Ngole aliiomba mahakama kuwapa muda wa kukamilisha upelelezi wa keshi hiyo kwa kuwa bado haujakamilika na kuomba mahakama hiyo kuipangia tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Kwa upande wao mawakili wa upande wa mtuhumiwa walimuomba hakimu kumpatia dhamana mteja wao kwa kuwa ni mtu anayefahamika ambaye hawezi kutoroka na ni mbunge ambaye anatakiwa kufanya shughuli zake za kibunge hadi hapo atakapohitajika.

Hakimu aliikubali hoja hiyo kwa masharti ya kudhaminiwa na watu wawili ambao kila mmoja anatakiwa adhamini kwa Sh500,000 na kuhakikisha mtuhumiwa anafika mahakamani pindi atakapohitajika.

Hakimu alikubali na kusema masharti ya dhamana yako wazi na hivyo wadhamini kujitokeza, akiwemo meneja wa Bonite mkoani Arusha, Mwangole Segule ambae alipingwa kuwa mdhamini kutokana na hati yake kukosa muhuri wa uongozi wa kampuni hiyo.

Baadaye, mfanyabishara wa madini ya Tanzanite, Baraka Kanunga alijitokeza badala yake na kuungana na mfanyabiashara mwenzake Joel Sabore Lesirya ambao wote kwa pamoja walifanikiwa kumdhamini mbunge huyo wa Simanjiro.

Wadhamini hao walitakiwa kuhakikisha Ole Sendeka anatinga mahakamani Februari 10 kwenye kesi hiyo ma iwapo kutakuwa na tatizo watapaswa kutoa taarifa mahakamani hapo.

Akizungumza nje ya mahakama, Sendeka aliwashukuru wote waliofika mahakamani hapo na kuwataka kuliacha suala hilo kwenye vyombo vya sheria ili vifanye kazi yake na kuwatahadharisha dhidi ya maneno machafu na kuwatuhumu watu kuhusu suala hilo pamoja na kuacha kufanya maandamamo wakati wanapotoka mahakamani hapo.

Source: Mwananchi Read News
 
Jana mbunge wa Simanjiro mheshimiwa Christopher ole Sendeka alifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kosa la kumshambulia na kumdhuru mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM mkoa wa Arusha Bwana James Milya. Katika kile kinachoonekana kuungwa mkono na wananchi wengi na baadhi ya watu wazito.

Mheshimiwa Ole Sendeka alisindikizwa na mamia ya washabiki wake akiwemo mwenyekiti wa makampuni ya IPP mzee mengi
 
Uwepo wa Mengi kumsindikiza Sendeka, ni uthibitisho wa kuunga mkono hoja ya Sendeka kuwa chanzo ni msimamo wake dhidi ya vita vya ufisadi.
Mzee Mengi amejiweka kimbembele kwa Sendeka ili kutangaza personal vendeta na Lowasa aliye nyuma ya Milya.

Tena nadhani (hypothes) ni Mengi ndiye anayemlipia Sendeka gharama za wakili Ngalo mdogo, maana juzi Ngalo alikuwa akisoma kwa kutetemeka huku akijikanyaga kanyaga, kusuudio la Mengi kulishitaki gazeti la TAZAMA kwa kumkashfu. Halafu jana Mengi na Ngalo wakatinga mahakamani kumsindikiza Sendeka.

Ni Sendeka alisaidia kufacilitate Mengi kupata kitalu kikubwa Mererani na kuwashawishi wazee wa Kimasai kumsimika Mengi kuwa Laibon na kumbatiza jina la Reginandi Ole Mengi pale Mererani mwanzoni mwa mwaka 2006. Hivyo huu ni wakati wa kulipa fadhila.
Karibu utabiri wa Mzee Mwanakijiji kuhusu anguko la Mengi, utatimia maana sasa yuko usawa wa front line ya siasa dhidi ya mafisadi.
 
please mkuu,naomba unikumbushe ni wapi Mzee Mwanakijiji alipotoa huo utabiri!?
 
Kweli nimeamini kuwa "Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi". Hili swala ukilichunguza bila ushabiki na bila emotions utajifunza mambo mengi sana.

1.. Ole Sendeka hawaelewani na Lowassa. Kwa sababu hii kila mpinzani wake somehow anakuwa attached na Lowassa. Hata ugomvi huu usingetokea, Sendeka bado angeunganisha upinzani dhidi yake na "hujuma" za kufikirika za Lowasa.

2. Vita dhidi ya mafisadi inatumiwa vibaya na baadhi ya watu kuwaweka watanzania katika hali ya taharuki na kusahau kutafakari. Kila mtu anayekwenda kinyume na "Sendeka-Kimaro-Kilango-Mwakyembe" SEKIKIMWA Syndicate, hata kwa maswala binafsi, anaonekana kuwa mpinzani wa vita dhidi ya mafisadi, something which is untrue and very unfortunate. Inahitaji vyombo vya sheria visivyo endeshwa kwa emotions la sivyo haki haitakaa itendeke nchini. Kupambana dhidi ya ufisadi hakumpi mtu kinga dhidi ya uovu wake na uvunjaji wa sheria. Hata hivyo, katika hali ya taharuki iliyoikumba nchi (its quit natural, any historian will tell you so) ni vigumu kupata public opinion tofauti. Vyombo vya sheria visifuate public opinion, vifuate haki.

3. "Reigand Ole Mengi" amepata sehemu ya "kulipa fadhila" alizotendewa na Sendeka. Pia ni njia ya kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa hakuwa "pamoja" na Lowassa enzi za ufalme wake, something which only GOD can prove. Mengi ni mfanya biashara, just like any other businessman. Kusoma alama za nyakati ni moja ya mbinu za kubakia kwenye soko. Kwenda mahakamani in person ni ushabiki uliopita mipaka. Ni kujishushia heshima, ukizingatia Sendeka ana nguvu, umri, uzoefu na hata pesa nyingi kuliko Millya.

4. Hapa Millya ni Daudi anayepambana na Goliath. Ole Sendeka yuko na Mengi, (with his whole media) one one hand na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzanite, wabunge wenzake na "anti-Lowassa" network on the other. Millya ameshika "manati" ambayo ni haki yake kama Mtanzania huru anayetafuta haki na ukweli kuwa kapigwa kibao na kutishiwa kwa bastola. One does not need PhD in Quantum Physics to predict the results.

5. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari haiwezekani kwa sasa kutenganisha swala hili na ugomvi kati ya Lowassa na Sendeka. Some how, Millya lazima ataonekana ku "tumiwa" na mafisadi. Hii inadhihirisha kuwa vita vya tembo zinazoumia ni nyasi. Millya anaweza kukosa haki zake kwa kuwa "wakubwa" wanagombana. Yeye ni nyasi tu katika hili. Tusubiri tuone.
 
please mkuu,naomba unikumbushe ni wapi Mzee Mwanakijiji alipotoa huo utabiri!?

Mzee Mwanakijiji alimchambua Mengi kama karanga katika thread ya Anguko la Mengi kama Maxwel. Ilikaa for few days nilipotaka kuchangia sikuiona tena. Sikujua kama ilijifade out ama kulikuwa na mkono wa mtu. Kwa Tabia ya Mengi anavyopenda kusifiwa tuu na anavyofedheheka kuumbuliwa, nadhani angedhamiria kuishitaki JF lakini nadhani mwanasheria wake akamwambia hii ni forum tayari ina disclaimer.
 
Mkuu naona umechanganya madawa hapa.
Mwanakijiji alikua "mjumbe" tu na kuweka jamvini makala iliyoandikwa kwenye moja ya magazeti mapya yalioibuka na spidi ya kummaliza R. Mengi(wengine walisema ya Manji). Hayakua makala ya Mwankijiji mwenyewe.
 
Mzee Mwanakijiji alimchambua Mengi kama karanga katika thread ya Anguko la Mengi kama Maxwel. Ilikaa for few days nilipotaka kuchangia sikuiona tena. Sikujua kama ilijifade out ama kulikuwa na mkono wa mtu. Kwa Tabia ya Mengi anavyopenda kusifiwa tuu na anavyofedheheka kuumbuliwa, nadhani angedhamiria kuishitaki JF lakini nadhani mwanasheria wake akamwambia hii ni forum tayari ina disclaimer.

Pasco,

Hiyo makala unayoisema haikuandikwa na Mzee Mwanakijiji, yeye alisaidia tu kuanzisha hiyo thread. Makala ilikuwa ni ya mtu mwingine kabisa.

Mengi ameshambuliwa hapa JF mara nyingi sana, je mara ngapi ameshatushitaki?

Hata hiyo makala unayoisema, tumia search tool na utaipata. Huenda imeondolewa kwenye siasa na kupelekwa kule kwenye celebrities.
 
Kweli nimeamini kuwa "Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi". Hili swala ukilichunguza bila ushabiki na bila emotions utajifunza mambo mengi sana.

1.. Ole Sendeka hawaelewani na Lowassa. Kwa sababu hii kila mpinzani wake somehow anakuwa attached na Lowassa. Hata ugomvi huu usingetokea, Sendeka bado angeunganisha upinzani dhidi yake na "hujuma" za kufikirika za Lowasa.

2. Vita dhidi ya mafisadi inatumiwa vibaya na baadhi ya watu kuwaweka watanzania katika hali ya taharuki na kusahau kutafakari. Kila mtu anayekwenda kinyume na "Sendeka-Kimaro-Kilango-Mwakyembe" SEKIKIMWA Syndicate, hata kwa maswala binafsi, anaonekana kuwa mpinzani wa vita dhidi ya mafisadi, something which is untrue and very unfortunate. Inahitaji vyombo vya sheria visivyo endeshwa kwa emotions la sivyo haki haitakaa itendeke nchini. Kupambana dhidi ya ufisadi hakumpi mtu kinga dhidi ya uovu wake na uvunjaji wa sheria. Hata hivyo, katika hali ya taharuki iliyoikumba nchi (its quit natural, any historian will tell you so) ni vigumu kupata public opinion tofauti. Vyombo vya sheria visifuate public opinion, vifuate haki.

3. "Reigand Ole Mengi" amepata sehemu ya "kulipa fadhila" alizotendewa na Sendeka. Pia ni njia ya kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa hakuwa "pamoja" na Lowassa enzi za ufalme wake, something which only GOD can prove. Mengi ni mfanya biashara, just like any other businessman. Kusoma alama za nyakati ni moja ya mbinu za kubakia kwenye soko. Kwenda mahakamani in person ni ushabiki uliopita mipaka. Ni kujishushia heshima, ukizingatia Sendeka ana nguvu, umri, uzoefu na hata pesa nyingi kuliko Millya.

4. Hapa Millya ni Daudi anayepambana na Goliath. Ole Sendeka yuko na Mengi, (with his whole media) one one hand na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzanite, wabunge wenzake na "anti-Lowassa" network on the other. Millya ameshika "manati" ambayo ni haki yake kama Mtanzania huru anayetafuta haki na ukweli kuwa kapigwa kibao na kutishiwa kwa bastola. One does not need PhD in Quantum Physics to predict the results.

5. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari haiwezekani kwa sasa kutenganisha swala hili na ugomvi kati ya Lowassa na Sendeka. Some how, Millya lazima ataonekana ku "tumiwa" na mafisadi. Hii inadhihirisha kuwa vita vya tembo zinazoumia ni nyasi. Millya anaweza kukosa haki zake kwa kuwa "wakubwa" wanagombana. Yeye ni nyasi tu katika hili. Tusubiri tuone.

Mkuu Matejoo
Good analysis hakuna cha kuongeza wala kupunguza
 
Back
Top Bottom