Ole Sendeka amtwanga konde M/kiti UVCCM!

its very dissappointing hearing that.However we may not know whats behind the scene.These people might have long time conflict, who knows.Though we human being have got some emotions when it comes to some issues yet a public figure especially legislator is expected to have learnt well on how to control his/her emotions.
 
I think Ole Sendeka was just gesticulating with his arms. There are times when we can gesticulate vigorously. That is a sure way of hammering in our points.

Kama point ya Mbunge, ambayo ameisisitiza kwa konzi lake, imemwingia vizuri mwenyekiti na akaonyesha kukubali sana kwa kulala chini, basi kulikuwa na mafanikio makubwa. The point was well taken.
 
Nasisitiza tatizo la Sendeka ni shule tu. Hakuna anae m-set anaji set mwenyewe na ukihiyo wake.

Mbunge mzima unashindwa ku behave hadharani ovyo kabisa

Mkuu Masatu

Ditopile naye tatizo lake lilikuwa nini. Shule?
 
Polisi wamefikia wapi katika upelelezi wa suala hili? Nilisoma kama wanataka kulifikisha mahakamani... au wamekosa ushahidi?
 
Yees nilikuwa nagojea hili dokezo kama la Nyambala.
Ole Sendeka anapigwa vita na si ajabu the whole thing ni stage managed.
HINT 1:Ole hawaivi na Edo
HINT 2:Edo na "aliyepigwa ngumi" ni maswahiba
Conclusion..mwana JF jazaj mwenyewe!

Exactly si vibaya kuanza kufanya analysis kwa upande huu pia. It realy worth!!
 
Mzee Sendeka kateleza hapa.

Na mafisadi watamkamata kirahisi kwa kumvisha kesi ya jinai. Akiwa convicted na jinai, baadaye wanamuwekea pingamizi wakati wa kugombea ubunge.

Kawekewa ulimbo kanasa mwenyewe, it seems jamaa wanaijua short temper yake ilivyo pamoja na hulka yake ya kutiana mkononi....

Tusubiri tuone.

Something tells me that mafisadi wanafanya home work zao kikamilifu.

Wanaamua kumtenegezea Ole S against them and work him the whole range down...

Details za kutafuta ili kumuangusha?

Among all ....hizi

Attitudes when confronted... Emotional response/control....Mental capabilities.... and ...everything....Then inakuwa rahisi kumtengeneza wanavyotaka.

Wamenyanganya bastola yake na Leo au kesho wanampeleka mahakamani kwa kosa la kutishia kuua..!

Ninafikiri soon details za the whole issue zitatoka...

Lets wait and see!!
 
Wazee wa Kimasai wajitosa ugomvi wa Sendeka, Millya

WAZEE wa kimila wa kabila la Kimasai, maarufu kama Leigwanan, wamevunja sherehe zilizokuwa zikiendelea za kumpongeza James Milya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha (UVCCM), baada ya wazee hao kuwasili ghafla katika sherehe hizo kwa lengo la kusuluhisha mgogoro wao.

Tukio hilo lilitokea juzi, muda mfupi baada ya Millya kumaliza kuwashukuru wananchi waliofika kuhudhuria sherehe hizo na wananchi hao kuanza kupata chakula na vinywaji.

Wakati wageni waalikwa wakipata chakula na vinywaji, ghafla waliingia malaigwanan hao, na watu wa karibu na Millya kuona hivyo waliamua kumtoa ukumbini bila kuaga na kuanza safari ya kurudi Arusha, huku baadhi ya waliohudhuria sherehe hizo wakibaki wameduwaa.

Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa watu wa karibu na Millya aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema sababu iliyomfanya Millya aondoke ukumbini hapo ni hofu ya kulazimishwa suluhu ya ugomvi wake na Ole Sendeka nje ya mahakama, jambo ambalo hajaliafiki.

"Wazee hao wanataka suluhu ya ugomvi wa Millya na Sendeka, ipatikane nje ya mahakama wakati Millya anashinikizwa aende mahakamani, hali hiyo imemfanya atoke ukumbini kwani malaigwanan ni watu wanaoheshimika sana katika jamii ya wafugaji, hivyo hakutaka kuwapa nafasi," alisema mtu wa karibu na Millya.

Tukio hilo lilihitimisha sherehe hizo ambazo hapo awali zilitanguliwa na ibada maalumu ya shukurani iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Usharika wa Olkesimet, chini ya mkuu wa jimbo hilo, mchungaji Herman Kweka.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa niaba ya wenzake, Mzee Thomas ole Ngulupe, alisema wao kama wazee wa kimila, walikuwepo wilayani Monduli wakati Sendeka na Milya wakirushiana makonde, hivyo wamekuja Simanjiro kwa lengo la kufanya suluhu ya ugomvi huo, kwani ni sehemu ya majukumu yao.

Ngulupe alisema tukio hilo lilitokea katika kikao cha jadi cha jamii ya Kimasai, hivyo wao kama viongozi wakuu ndio wenye mamlaka ya kusuluhisha kijadi bila kufikishana mahakamani.

"Lakini kitendo cha Millya kutukimbia kimetufedhehesha sana kwani tulitaka kuanza naye, kisha kwenda kwa Sendeka na hatimaye tungewakutanisha wote," alisema Ngulupe.

Mzee mwingine, Yese Kamduli Lesimanga, alisema tukio hilo la kukimbiwa na Millya, limedhihirisha kuwa hata mila za Kimasai zinazoheshimiwa na jamii hiyo, zimeanza kudharauliwa, kwani Wamasai wenyewe hawaheshimu mila zao.

Sendeka na Milya walipigana kwenye kikao cha jadi juzi mjini Monduli katika ugomvi unaodaiwa kusababishwa na tamaa ya kutaka kuwania jimbo hilo linaloshikiliwa na Ole Sendeka.

Source:Tanzania Daima.
 
Tatizo la Sendeka ni shule. Wot do u expects from form 4 failure with Div 4.

kinachomsadia ni huo mzuka wake wa kimasai ambao sometimes unapanda sipo...
What matters ni results.The guy provides results, which we need for the good of country.
Either ni form 4 or form 9 it does not matter.Hao wenye form 20 wameifanyia nini nchi hii???????
Ifike mahali mtu apimwe kwa results anazoprovide sio hayo maform 17 yenu.
 
Ole Sendeka adai mafisadi wamempania
Jackson Odoyo
MBUNGE wa Simanjiro kwa tiketi ya CCM, Christopher Ole Sendeka amesema matatizo anayokabiliana nayo kwa sasa na yaliyomsababisha amtandike ngumi mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Arusha, James Millya ni mkakati maalum wa mafisadi unaolenga kumfuta katika uwanja wa siasa na kuonya kuwa wakiachiwa, chama kitakwenda pabaya.

Ole Sendeka alimtwanga ngumi Millya wakati wa mapumziko ya chakula ya semina ya kimila iliyohusu matumizi ya ardhi wilayani Monduli mwishoni mwa wiki iliyopita akidai kiongozi huyo wa vijana wa CCM mkoani Arusha alikuwa akimshambulia wakati akiwasilisha mada yake kuhusu Matumizi na Sheria ya Ardhi.

Ole Sendeka alidai kuwa Millya alidai katika mada yake kuwa wanasiasa wanadhulumu wafugaji ardhi kwa kutumia sheria na kutoa mfano wa Simanjiro, kitu alichotafsiri kuwa alikuwa akinangwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, mbunge huyo aliyejizolea sifa kwa jitihada zake za kupiga vita ufisadi, alisema watu hao wameanza kumwandama ili kudhoofisha jitihada zake za kuendelea kupiga vita ufisadi ndani ya CCM.

Alisema mafisadi hao walianza kumwandama kipindi kirefu ndani ya chama hicho na hivi sasa wamefikia hatua ya kumuangamiza kisiasa ndiyo sababu wameanza kutafuta kila sababu za kumshitaki ili afikishwe mahakamani.

"Wameanza kutafuta kila sababu ya kunifikisha mahakamani ili nikose sifa ya kugombea jimbo langu mwaka 2010 na nitoweke katika siasa," alisema Ole Sendeka na kuongeza:

"Moja ya njama hizo za mafisadi zilianza kuonekana siku moja baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa UV-CCM baada ya mtu asiyejulikana kuniandikia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa laini ya Tigo ukisema kwamba wameshaking'oa kisiki kimoja bado mimi na watafanikiwa kwa sababu hakuna haki hapa Tanzania na kwamba haki iko mbinguni."

Alisema Millya pia aliwahi kumuhakikishia kwamba amejitoa muhanga kwa ajili ya kumng’oa katika siasa.

"Nia ya mafisadi hawa inafahamika na leo hii wameanzia kwangu kesho watahamia kwa (mbunge wa Same, Anne) Kilango na baadaye watakwenda kwa (mbunge wa Kyela, Harrison) Mwakyembe ili waweze kufanikiwa katika jitihada zao za kulimaliza kundi linalopiga vita ufisadi ndani ya CCM na kama hawatashughulikiwa kikamilifu na haraka, hali ya chama itazidi kuwa mbaya," alisema.

Alifafanua kwamba Mafisadi hao wasipodhibitiwa kikamilifu hali itazidi kuwa mbaya ndani ya CCM kwani lengo lao ni kutetea ufisadi ndiyo maana alipozungumzia suala la ufisadi katika semina hiyo, Millya alisimama na kuanza kumshambuliwa.

"Shambulio hilo lilikuwa la maneno na hatimaye likawa la mikono kwa kuwa alinirushia ngumi ambayo niliikwepa... alikuwa akinitaka niwataje hao mafisadi ninaowasema na baada ya tukio hilo niliwasiliana na Lowasa akiwa kama kiongozi wa semina hiyo ya kimila, lakini akasema kwamba hawezi kuzungumzia siasa za Simanjiro," alisema Ole Sendeka.

Hata hivyo, Ole Sendeka alifafanua kwamba hana wasiwasi wowote kuhusu taarifa kwamba Millya ana mpango wa kugombea ubunge katika jimbo lake kwa sababu ana haki ya kikatiba kufanya hivyo. Lakini alidai kuwa Millya hajaandaliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo, bali kumchafua tu.

Aliongeza kuwa sakata lake na Millya ni ishara tosha kwamba safari hii mafisadi wameamua kumuangamiza.

Pia alidai haikuwa nia ya Millya kulifikisha suala lake mahakamani bali msukumo wa mafisadi, ambao bado hajawaweka hadharani.

Source: Mwananchi Read News
 
That's why I earlier asked, vp tumesikiliza upande wa pili????
 
MBUNGE wa Simanjiro kwa tiketi ya CCM, Christopher Ole Sendeka amesema matatizo anayokabiliana nayo kwa sasa na yaliyomsababisha amtandike ngumi mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Arusha, James Millya ni mkakati maalum wa mafisadi unaolenga kumfuta katika uwanja wa siasa na kuonya kuwa wakiachiwa, chama kitakwenda pabaya.

"Nia ya mafisadi hawa inafahamika na leo hii wameanzia kwangu kesho watahamia kwa (mbunge wa Same, Anne) Kilango na baadaye watakwenda kwa (mbunge wa Kyela, Harrison) Mwakyembe ili waweze kufanikiwa katika jitihada zao za kulimaliza kundi linalopiga vita ufisadi ndani ya CCM na kama hawatashughulikiwa kikamilifu na haraka, hali ya chama itazidi kuwa mbaya," alisema
.

"Wameanza kutafuta kila sababu ya kunifikisha mahakamani ili nikose sifa ya kugombea jimbo langu mwaka 2010 na nitoweke katika siasa," alisema Ole Sendeka na kuongeza:

AND yestarday I said.

Mafisadi wanafanya hpmework yao vizuri sana.

kunagezi limemtaja EL kabisa and na alimvyomchelewasesha kwenda kuungana na Ziara ya Raisi iliyokuwa inaendela minjingu ili tu...adhama yao ifikiwe.

Inaonekani ilikuwa ni total set up!!!
 
From Tanzania Daima 13 january 2009

WAZEE wa kimila wa kabila la Kimasai, maarufu kama Leigwanan, wamevunja sherehe zilizokuwa zikiendelea za kumpongeza James Milya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha (UVCCM), baada ya wazee hao kuwasili ghafla katika sherehe hizo kwa lengo la kusuluhisha mgogoro wao.

Tukio hilo lilitokea juzi, muda mfupi baada ya Millya kumaliza kuwashukuru wananchi waliofika kuhudhuria sherehe hizo na wananchi hao kuanza kupata chakula na vinywaji....

Maoni ya wasomaji.

Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.

Maoni 8 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Leigwanan, Mahakama za Kadhi, mambo bado! Ni vurugu tupu kuidhoofisha mahakama. Sishangai kuona AG,IGP,na Takururu wanaendesha kazi zao kwa kumhofu rais. Hawa walistahili kuwa huru.

na Biswalo, Mwanza/Tz, - 13.01.09 @ 10:13 | #7008

hiyo ndo adabu nzuri ya Millya? kama haheshimu wazee sasa atamuheshimu nani, Bashe? Wazee na wamasai wote msidhalilishwe na kafisadi kanakochipukia "Millya",haya CCM arusha kunani? pikipiki JK kakataa kugawa,mbunge na mwenyekiti wa UVCCM wametwangana,Millya kaandaa sherehe Manyara badala ya mkoa alioshinda? hii sishangai as long ni mkoa anaotoka fisadi Lowassa so lazima aanzie kuteka nyumbani,so la maana CCM muwe makini na Lowassa,kama vipi mumvue hata uanachama kabla mambo hayajazidi kuharibika.KKT manyara mnataka kuwa kimbilio la mafisadi, hatuwaelewi,kumbukeni wenzenu wa Kinondoni walirudisha hela za Rostam,nyie mlimtandikia kapeti Lowassa,tuwaeleweje KKT manyara? Tunaomba baba askofu Mwalasusa aimulike KKT Manyara

na jenga, tz, - 13.01.09 @ 14:20 | #7066

Huyo Millya anatumiwa tu na Lowassa na Kibaraka wake Kone ni mafisadi wanaoogapa kivuli cha sendeka bungeni kutikana na wizi wao.Sendeka hao wasikutishe watanzania wako nyuma yako kupinga ufisadi kwa nguvu zote.

na Busara, Danganyika, - 13.01.09 @ 16:40 | #7113

1.Mtu anatoka ARUSHA anakuja Manyara amekuja kwa ajili ya nini/nani.
2.Lowasa anahusika maana yeye pia sio Mmasai!!wameru wanamtawala nani kwa vipi?
3.NARUDIA KUSEMA KANISA WATOKE USINGIZINI.UKIINGIZA FISADI MAANA YAKE.MUNGU AONDOKE.HAO MAASKOFU WA K.K.K.T ARUSHA wanaanza kutumiwa na wanasiaa fisadi!!!

TUBADILIKE NCHI HII INAHITAJI WATU WATAKAO KULA KIAPO CHA KUMAANISHA ANAKUNYWA MWENYEWE.

na BARIKI, TANZANIA, - 13.01.09 @ 20:46 | #7140

ole sendeka si kiongozi bora. kiongozi bora hatumii ngumi na bastola kukabiliana na challenge! hapa anawapa credit mafisadi

na Deo, Dar es Salaam, - 13.01.09 @ 20:50 | #7141

Vinara wa kupiga vita ufisadi chungeni sana mitego la sivyo mtapoteza muda mahakamani

na yona matadi - 14.01.09 @ 04:09 | #7176

MAMBO YOTE HAYA YANAYOTOKEA SIMANJIRO CHANZO CHAKE LOWASSA!
MPANGO WAKE NI KULIPA KISASI KWA KUHAKIKISHA KUWA SENDEKA HARUDI TENA BUNGENI 2010. LOWASSA NI MTU HATARI SANA KWA NCHI.KADIRI YA HDETAILS NILIZO NAZO JUU YA LOWASSA, HUYU MTU NI CRIMINAL, YUPO TAYARI HATA KUUA MTU KWASABABU YA MASILAHI YAKE! SASA ANAMPANGO MKUBWA JUU YA WABUNGE WOTE WALIOCHANGIA KUMTOA UWAZIRI MKUU.

na Libwa wa Libwa - 14.01.09 @ 07:08 | #7181

KUMBE LOWASSA NI MTU HATARI SANA KWA AMANI YA NCHI TZ.
MUNGU AMUONDOE DUNIANI HUYU MFALME WA MAFISADI DUNIANI.

na ANNA - 14.01.09 @ 07:12 | #7183

Tanzania Daima - Sauti ya Watu.
 
What matters ni results.The guy provides results, which we need for the good of country.
Either ni form 4 or form 9 it does not matter.Hao wenye form 20 wameifanyia nini nchi hii???????
Ifike mahali mtu apimwe kwa results anazoprovide sio hayo maform 17 yenu.

Spot on! wot matters is the results... and he had one by throwing a knock out punch to his political "rival"
 
Watu wengine ovyoo kabisa yaani Mbunge mzima unavunja sheria kwa kupiga watu ovyo halafu unasingizia mafisadi! msamiati mafisadi umepoteza maana sasa..
 
Watu wengine ovyoo kabisa yaani Mbunge mzima unavunja sheria kwa kupiga watu ovyo halafu unasingizia mafisadi! msamiati mafisadi umepoteza maana sasa..

Haya, tayari Masatu alikuwapo Monduli na ana ushahidi kuwa Sendeka alipiga na sasa anasingizia na wala Masatu hajui kwamba Sendeka ndiye alikuwa mstari wa mbele kumng'oa Lowassa, kwa michango yao na kina Kilango.

KULIKONI la leo, limeandika hii:

Lowassa alimtosa
Sendeka Monduli
MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

MBUNGE wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka, amesema Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, amemtosa kwa kukwepa jukumu la kumdhibiti Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Arusha, James ole Millya, ambaye alikaidi ushauri wa wazee wa kimila waliokuwapo wakati ulipotokea ugomvi kati yao hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam alipo kikazi, Sendeka amesema Lowassa alikataa kuingilia suala hilo pamoja na kuwa ndiye aliyekuwa mwenyeji na kiongozi wa semina iliyofanyika wilayani Monduli.

Sendeka alisema Millya ndiye aliyemshambulia kwa maneno na baadaye kumvamia kabla ya yeye kujitetea kwa kumsukuma kitendo kilichosababisha mwenzake kuanguka, lakini walishauriwa na wazee wa jadi kutolipeleka suala hilo polisi lakini mwenzake alikadidi.

“Niliwasiliana na Mheshimiwa Lowassa kutaka kujua msimamo wake baada ya viongozi wa kimila kutaka kulisimamia, lakini yeye pamoja na kuwa ni kiongozi alisema hawezi kuingilia siasa za Simanjiro, nikashangaa wakati pale hatukuwa kwenye siasa za Simanjiro,” alisema.

Sendeka alisema kwa mazingira ya tukio na matokeo yake baadaye amebaini kuwapo kwa mkakati wa makusudi wa baadhi ya viongozi kummaliza kisiasa, mkakati ambao amesema unasimamiwa na kufadhiliwa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

“Mwaliko katika semina husika haukuwa na nia nzuri. Ulikuwa wa kuniingiza mtegoni. Ulikuwa na nia ya kutafuta sababu za kunishambulia pindi nitoapo hoja, na mashambulizi yaanzwe na aliyekwishaandaliwa. Aliyeandaliwa alikuwa ni Millya,” alisema Sendeka.

Alisema sababu kubwa ya kuamini hivyo ni kutokana na Millya kuulizia alipo kwa kumkashifu ikiwa ni pamoja na kumuita yeye fisi na hata katika mjadala alishambuliwa bila ya kupewa nafasi ya kujibu hoja zilizotolewa zikimlenga moja kwa moja.

Akielezea tukio zima la ugomvi ambalo anasema limepotoshwa kwa makusudi, Sendeka alisema Millya ndiye aliyemshambulia na kumgusa sehemu ya pua na katika mzozo huo bastola yake ilianguka.

“Alirusha mikono akanigusa sehemu ya pua, akarusha ngumi nikakwepa na katika kujihami nilimsukuma akaanguka chini. Wakati wa purukushani hii bastola yangu ikaanguka. Baada ya kuamuliwa nilifuata na kuiokota bastola yangu na kuihifadhi,” alisema.

Akifafanua Sendeka alisema Millya aliwakwepa baadhi ya viongozi wa kimila na viongozi wa dini ambao walimwendea kufuatilia suala hilo, ambalo amesema kwa sasa liko mikononi mwa polisi ambao nao ameshangaa kusikia linashughulikiwa na polisi mkoa wa Arusha badala ya wilayani Monduli ulikotokea ugomvi.

“Nilipotaka kwenda polisi kuripoti shambulio, viongozi sa kimila walinishauri nisifanye hivyo bali niache suala hili lishughulikiwe kimila ili kuepuka kulikuza mbele ya jamii pasipo manufaa yoyote. Nilifuata ushauri wa viongozi wa kimila. Wakati huo kutokana na ushauri wa watu waliokuwa na ajenda zao, Millya alienda kuripoti polisi kinyemela akaripoti nilimpiga na kumtishia maisha yake kwa bastola,” alisema.

Sendeka pia alishangazwa na hatua ya baadhi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kuingilia kati na kutaka kufanya maandamano wakidai kwamba wanapiga vita ukiukwaji wa maadili huku akisema anashanga vijana hao hawajawahi kuandamana wala kutoa kauli za kuonyesha kupinga ufisadi mkubwa ulioibuliwa na Bunge na kufanyiwa kazi na Rais Jakaya Kikwete.

“Vijana hawa hawajawahi hata siku moja kuandamana kupinga ufisadi wa Richmond, EPA ama mikataba minhgine tata ya madini, iweje leo wanakuwa waadilifu kiasi cha kuandamana dhidi ya Ole Sendeka bila hata ya kuwa na subira ya kupata maelezo ya pande zote?” alihoji.

Sendeka ambaye anakiri kuwa nje kwa dhamana, aliripotiwa katika kituo cha polisi cha Monduli Januari 9, mwaka huu tukio lililotokea wakati akiwa mmoja wa washiriki katika kikao cha kimila cha jamii ya Wamasai.

Millya alimfungulia Sendeka mashtaka dhidi ya tuhuma hizo katika Wilaya ya Monduli kwa kesi namba MON/RB/35/2009 akimtuhumu kumshambulia kabla ya kumtishia kumuua kwa bastola wakiwa eneo la mkutano.

Mkutano huo ulioandaliwa na Lowassa ulifanyika maeneo ya Chuo cha Ualimu Monduli, ambako kulifanyika mkutano mkubwa uliojadili suala la elimu hasa kwa watoto wa kike katika jamii za wafugaji; Wamasai na migogoro ya ardhi.

Millya ambaye anatajwa kuwania ubunge wa Simanjiro mwaka 2010, alielezwa kuchangia akielezea kukerwa na kauli ya Sendeka kupinga ufisadi. Millya anaelezwa kutoa sharti kwa Sendeka kujiuzulu ubunge kwanza ili aweze kufuta kesi polisi.

Wakati wa malumbano hayo, mkutano uliendeshwa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko ole Kone, ambaye ndiye aliyepokonywa ubunge na Sendeka, jambo ambalo limeelezwa kuwa sababu kubwa ya Sendeka kutopata nafasi ya kujibu mapigo.
 
What matters ni results.The guy provides results, which we need for the good of country.
Either ni form 4 or form 9 it does not matter.Hao wenye form 20 wameifanyia nini nchi hii???????
Ifike mahali mtu apimwe kwa results anazoprovide sio hayo maform 17 yenu.

Thanks Mkuu;

Kuna watu humu wanaua eti kwa sababu ya Elimu; Hata Mahalu si Professor? Katufanyia nini kikuu? Results matter more than anything else.
 
Haya, tayari Masatu alikuwapo Monduli na ana ushahidi kuwa Sendeka alipiga na sasa anasingizia na wala Masatu hajui kwamba Sendeka ndiye alikuwa mstari wa mbele kumng'oa Lowassa, kwa michango yao na kina Kilango.

Lets put this way, Halisi alikuwepo Monduli wakati mafisadi wana "mset" Sendeka!

Happy now?
 
Kuna watu mediocre sana humu nchini kwetu. Ndiyo maana ni rahisi kwa kila mbwa mwitu kuvaa ngozi ya kondoo na kupeta bila kushtukiwa na mtu yeyote. Yaani maneno tu yametosha kuwatongoza watanzania na akili zao kumuona Ole sendeka kuwa anapambana na ufisadi. Can any sensible person tell me why they regard him as such? Historia yake mnaijua? Huko Simanjiro mana fahamu umafia alioutenda in the past 3 years kiasi cha kuigawa wilaya katika makundi? Yeye alipokuwa mwenyekiti wa CCM wilaya alimfanyia vituko gani Parseko Ole Kone aliyekuwa Mbuge wa Simanjiro by then? Kwa kifupi chama kilichukua hatamu Simanjiro!

Elimu ndogo ya Sendeka si tatizo sana (kama alivyosema mchangiaji kuwa Mahalu ni Prof lakini kauibia) kama haitumii kumjengea infiriority complex na kuvuka mipaka ya utu yaani kufikiri. Kutokana na kielimu chake basi anaogopa kinvuli cha Millya.

Mimi nafikiri tuangalie kila jambo on its own case. Hii ya Sendeka kuijumlisha na uhasama wake na Lowassa ni kupoteza dira. There is nothing like mkono wa mafisadi in this particular thing. Ni kweli mheshimiwa Mbunge ana maadui wengi kutokana na maneno yake makali lakini hii haimpi kinga dhidi ya vitendo vyake viouvu na makosa ya jinai. Kwa mwendo huu itakuwa kila anayekemea ufisadi (kwa maneno) anajijengea aina fulani ya immunity against criminal actions iwe ujambazi, ubakaji, unajisi na kutishia kuua. Wake up my fellow Tanzanians!
 
Back
Top Bottom