Kaizer
Platinum Member
- Sep 16, 2008
- 25,320
- 17,822
Wakuu hii imekaaje kama wameanza kupigana wenyewe kwa wenyewe? Kuna watu wana hatimiliki ya majimbo?
Mbunge CCM amtwanga konde M'kiti UV-CCM
Na Mussa Juma, Monduli
MBUNGE wa jimbo la Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, jana alisababisha kizaazaa wakati alipompiga ngumi mwenyekiti mpya wa jumuiya ya vijana ya chama hicho, UV-CCM, mkoani Arusha wakati wa mapumziko ya semina iliyoandaliwa kuzungumzia matatizo ya ardhi.
Kilomita chache kutoka eneo hilo, mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alikuwa akizindua nyumba za wanajeshi wa kambi ya Monduli, akiwa ameongozana na viongozi wengi wa chama hicho na leo anatarajiwa kuja mjini hapa kuendelea na ziara yake.
Sakata hilo lilitokea wakati wajumbe wa semina hiyo wakitoka nje ya ukumbi kwa ajili ya kupata chakula cha mchana na ndipo Ole Sendeka, mmoja wa watu machachari bungeni, kumwendea mwenyekiti huyo wa UV-CCM, James Ole Milia na kumpiga konde lililompeleka hadi chini.
"Alitumia mada yake kunishambulia," alisema Ole Sendeka akizungumzia mada iliyowasilishwa na Ole Milya kwenye semina hiyo kuhusu matumizi ya ardhi na jinsi wanasiasa wanavyotumia Sheria ya Ardhi kudhulumu wafugaji iliyofanyika kwenye Chuo cha Elimu Monduli.
"Alisema waziwazi kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumia Sheria ya Ardhi kudhulumu wafugaji... kibaya zaidi ilifikia wakati akawa anatoa mifano ya Simanjiro wakati akijua mimi ndiye mbunge wa jimbo hilo.
"Huyu anatumiwa na mafisadi kunimaliza... najua ameshaeleza kuwa anataka kugombea ubunge wa Simanjiro ndio maana ameona aanze leo kunishambulia.
"Ninajua kuwa ameandaliwa mapokezi Simanjiro siku ya Jumapili kwa kisingizio cha kumpongeza kwa kuchaguliwa kuongoza vijana Arusha, lakini anataka kuwania ubunge."
Ole Milia, ambaye ni mwanasheria, alikanusha tuhuma hizo za kutumia mada yake kumshambulia Ole Sendeka, akisema alilenga kuzungumzia matatizo ya ardhi na Sheria ya Ardhi.
"Nitamchukulia hatua za kisheria," alisema Ole Milia wakati akipata matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Monduli. "Amenijeruhi na amenidhalilisha mbele ya watu, hivyo ni lazima nimchukulie hatua za kisheria.
Tayari mwenyekiti huyo wa UV-CCM amesharipoti tukio hilo polisi na sasa anasubiri kesi.
Source: Mwananchi Read News[/COLOR][/SIZE][/B]