Kitu kinaita hiki.
Mkuu jukwaa hili mbona umelitosa? Hebu rudi uwe unatusaidia kupunguza stress kwa kupata mavitu ya enzi zetu.
Siku hizi wanataja taja majina tu ndugu yangu na ukiwaambia jibu lao huu ni waqt wao. Utasikia wanaambizana mwanangu nimetoa bonge la pini ukija sikiza unabaki kukumbuka zile siku nzuri za zamani.Nimetoka kumsikiliza Ali Kiba - akimuita AJE,
Kisha nikamsikiliza Diamond - akimchombeza SALOME wa watu,
Halafu nikamsikiliza Chiriku, Hemed Maneti "Ulaya" na MARIA wake akiwa na Vijana Jazz, dah! nikatambua tofauti ya muziki na usanii.
Natamani nyakati zingerudi nyuma wallah!