Oksana akiwa hospitali baada ya kukatwa miguu yake na mkono wake wa kulia baada ya kuchomwa moto b

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
6320950.jpg

Oksana akiwa hospitali baada ya kukatwa miguu yake na mkono wake wa kulia baada ya kuchomwa moto baada a kubakwa
Thursday, March 22, 2012 4:01 AM
Mwanamke mwenye umri wa miaka 18 wa nchini Ukraine yuko mahututi hospitali baada ya kubakwa mtungo na wanaume watatu na kisha kuchomwa moto uliopelekea akatwe miguu yake yote miwili na mkono wake mmoja.
Oksana Makar, 18, alikuwa ni mrembo mwenye umbile na sura ya kuvutia lakini ghafla maisha yake yamegeuka juu chini baada ya kubakwa na wanaume watatu ambapo wanaume wawili kati yao ni watoto wa vigogo wa serikali nchini Ukraine.

Mbali ya kubakwa, Oksana alivalishwa matambara na kutelekezwa porini na kuchomwa moto ili afariki.

Lakini nusura yake ilitokea kwa mmoja wa wapita njia aliyesikia kelele zake za kuomba msaada na kwenda kumuokoa.

Kutokana na moto kumuunguza vibaya Oksana, madaktari wamelazimika kuikata miguu yake yote miwili na mkono wake wa kulia.

Katika VIDEO iliyorekodiwa na mama yake na baadae kurushwa kwenye mitandao, Oksana anasema kuwa wanaume waliomfanyia kitendo hicho wakikamatwa basi wakatwe makende yao na makende hayo wapewe mbwa wale.

Oksana alibakwa baada ya wiki iliyopita kualikwa kwenye mojawapo ya nyumba waliyokuwa wakiishi wabakaji hao. Watuhumiwa wa ubakaji ni pamoja na Maxim Prisyjnikov, 23, mtoto wa mkuu wa mkoa na Artyon Pogosyan, 21, mtoto wa mwanasheria wa mkoa.

Wabakaji hao walikamatwa na kuachiwa huru siku hiyo polisi wakisema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha.

Kuwekwa kwa VIDEO online kumepelekea wananchi wengi waandamane wakitaka haki itendeke.

Hatimaye rais wa Ukraine aliamuru uchunguzi wa kina ufanyike na ndipo wabakaji hao watatu walipotiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua.

Angalia VIDEO ya Oksana akitaabika kwenye kitanda cha hospitali ambako anatibiwa majeraha yake ya kuungua moto



VIDEO - Mwanamke Abakwa na Wanaume Watatu na Kisha Kuchomwa Moto

<tbody>
</tbody>
 
Last edited by a moderator:
hivi malaya hakuna mpaka mtu ukabake?
Nchi zingine kupata mwanamke inakuwa Big deal unafikiri kama hapo kwenu bongo wanawake wa kumwaga!!!!!!!!! Uarabuni au baadhi za nchi kama za vishoka Ukraine kupata mwanamke ufanye kazi kutongoza ama sivyo utakosa tu.
 
Back
Top Bottom