Okoa hii ndoa.

Halafu atarudi kanisani kulia. Haya makanisa yetu ya nyakati hizi ni hatari.

Ooooh Gosh!

Pengine niseme nina ufahamu na uelewa mzuri sana tena kwa vitendo kwa akina mama wenye imani kama hizi.
Hawa huwa hawatembeagi nje ya ndoa (kwa maana ya kutembea na wanaume wengine) hata wanaporudi nyumbani usiku
Hawa wamama wanakuwa wana tatizo kubwa la kiimani.
Mara nyingi huwa wamehama kutoka imani zao za awali za kikristo na kuingia hizo imani mpya huku wakiwa na matarajio makubwa ya kusikilizwa na Mungu kwa matatizo yao wakiwa huko kuliko imani zao za awali. Wenyewe wanasema wanasali KIROHO na sehemu zao za ibada wanaziita MAKANISA YA KIROHO na wanakusanyika hata chumbani na kuanza kusali kuanzia asubuhi mpaka usiku, huku seheu kubwa ya sala zao zikitawaliwa na watu kulia, kupiga-piga chini kama mtu mwenye hasira na kwa sauti kubwa.
Kunakuwa na kiongozi wa hayo makanisa ya kiroho ambaye huitwa Baba Mchungaji ambaye akikutana nao huwaeleza mambo ambayo ameoteshwa na Mungu, na kama kuna maagizo yoyote kutoka kwa Mungu ktk hizo ndoto basi Muumini aliyetajwa anapaswa atekeleze ndoto kwa vitendo. Ndoto nyingi zinakuwa ni fedha au mali.

Hutafutwa wamama ambao nyumbani kwao wana uwezo mzuri wa kiuchumi na kifedha ambao ni dhaifu kiimani kama nilivyoshuhudia mimi mwenyewe huku ninapokaa. Mchungaji huwaambia Mungu amemuotesha anapewa Mil 6 na huyo mama ili Mchungaji amalizie kujenga nyumba yake. Tena anasema wazi kwamba "NAJUA UNA UWEZO WA KUTOA KIASI HICHO, NA MUNGU AMENIAGIZA NIKUELEZE UNIPE"
Sasa kutokana na kuwa mtumwa wa imani hizo (yaani unakuwa kama umelishwa libwata fulani hivi) basi unampa kweli.

Nikirudi ktk ushauri
Kwanza fahamu ya kwamba waharibifu wakubwa wa imani ya huyo mama ni watu wamama wenzake anao ambatana nao, ambao ndio walimbadilisha imani yake ya awali.
Kwa sabau ya uzito wa tatizo lenyewe, nashauri waitwe ndugu wa pande zote, hasa wazazi na watu wazima wengine wanaoheshimika ktk hizo pande (mwanamke na mwanaume) wakae na walizungumze hilo suala kwa lengo la kulikomesha lisiendelee. Nina uhakika kwa busara za wazee na wazazi wa mwanamke watambana mwanao na ikibidi kumuonya au la watamwambia aseme kama amechoka kuishi maisha ya ndoa na huyo mwanaume aendelee na imani zake kwa uhuru ili ijulikane nini cha kufanya
 
Back
Top Bottom