Ogopa Mgomo Baridi: Muhimbili hakufai

attachment.php
 
Haya tuliyategemea serikali ya CCM ni bora serikali ya HITLER (NAZI), haina chembe ya huruma kwa watumishi achilia mbali wananchi wenyewe.
 
Tatizo la sis watanzania hatuna uzalendo hatakidogo . Madactari walivyo goma badala ya watanzania kuwasuport wakawa wana waponda na kuwaambia warudi kazini. Nafikiri pia inachangiwa na kutokwenda hospitalini tukaona yanayo tokea na madai yamadactori yalikua ni nini

wananchi wakamwamini sana liwalo naliwe

walahi tena tutateseka sana na kama nikulala chini tutalala chini sana tena hapo ni bado sana ngoja baada ya mwaka moja sasa utaniambia
 
Kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu,tunachekwa dunia nzima,the third largest beggar in the world after afghanistan and iraq,the question is can we really afford to fire all those medics? more than 300?this is outrageous!
 
Tatizo la sis watanzania hatuna uzalendo hatakidogo . Madactari walivyo goma badala ya watanzania kuwasuport wakawa wana waponda na kuwaambia warudi kazini. Nafikiri pia inachangiwa na kutokwenda hospitalini tukaona yanayo tokea na madai yamadactori yalikua ni nini

wananchi wakamwamini sana liwalo naliwe

walahi tena tutateseka sana na kama nikulala chini tutalala chini sana tena hapo ni bado sana ngoja baada ya mwaka moja sasa utaniambia
Na madokta nao wanasema liwalo na liwe
 
Hali kama hii wodi kujaa serikali inaitafsiri kuwa huduma zimerejea.
Wao watu kummiminika kwa wingi hospitali na wodi kujaa ndo indicator ya huduma nzuri.
Serikali ya Kikwete na Pinda wanajua QUANTITY tu, QUALITY kwao msamiati.

Walikuwa wakipita na kujisifu na shule za kata....sasa juzi juzi eti wanatoa tamko kwamba sasa wamesitisha ujenzi wa shule hizo kwani wamegundua hazikidhi kiwango. Si tunadanganyana.. yaani leo hii baada ya sisi kupeleka watoto wetu huko ndio wanaona hili??
 
Sijui wale madokta wa voda fasta wameishia wapi?
 
About 100 graduate doctor as Specialists in different medical disciplines are expected this August.
And about 80% of them are likely to walk away for greener pastures.
This is from one of their contained meetings following mgomo saga.
 
Ujinga wetu ndo umetufikisha hapa!
Na wajinga ndio waliwao. Si mnaishabikia serikali na kuwaponda madaktari? Ukitaka kujua kwamba hata wao wanajua umuhimu wa daktari kamuulize OCD-CID wa Wilaya ya Kawe alipoanza toba hata bila kuulizwa alipojikuta uso kwa uso na anaowaita maadui wa vigogo wake. Aisifuye mvua imemnyea.
 
About 100 graduate doctor as Specialists in different medical disciplines are expected this August.
And about 80% of them are likely to walk away for greener pastures.
This is from one of their contained meetings following mgomo saga.

I like this, mwe! Sijui kama message delivered and read to JK et al. Namtia moyo aendelee kunyanyasa noble professions lakini aongeze bidii kutrain ili wenye meno wale, yeye aendelee kucheza mchezo wa bao vijiweni na wapambe wake.
 
hivi waziri wa afya yupo?
Kuwapo kwake utakujua akiugua mafua na kwenda India Apollo Private Hospital, magazeti na TV na Radio vitacover Headings zao naye kupata umaarufu. Umesikia wapi tembo akijali sisimizi wakati anapobarizi?
 
Jamani waandishi wa habari,
Hebu thibitisheni habari hizi kwa umma wa watanzania.
Nendeni mpige picha zenu, video,
M-hoji wagonjwa,
ikiwezekana na ndugu zao
na uongozi wa Hospitali kwani tuliwashuhudia sikuchache kwenye TV wakijigamba kuwa huduma zimerejea kama kawa!
Tupate ukweli.
Watanzania wanakufa,
watanzania wanakuwa vilema.
Tutakuwa nchi ya misiba na vilema.

Waandishi wathibitishe nini wakati thread hii imeanika kila kitu? Pictures says more deeply than words. Kiziwi umpe nini asikie wimbo wa Rose Mhando "Jipange sawasawa"
 
Hii kiboko.
Ninachoona mimi hapa ni kuwa watanzania wameridhika na hali iliyopo na ndiyo maana serekali inawafanyia inavyotaka.
kulala chini ndo kawaida na inachukuliwa kama standard service kwa mtanzania.
Masikini sijui hata mtoa huduma atampaje huduma zaidi ya kumruka tu???
Kuna haja ya hizi hospitali za rufaa zilizotajwa na serikali zitumike maana hawa watu wanateseka sana jamani.Kuna Amana ,Temeke,Mwananyamala na Lugalo.
Nadhani viongozi wetu wangetibiwa hapa nchini haya mambo yasingetokea
 
Huduma mbovu za Afya zitatutafuna wote. Hili ni suala ambalo linaenda katika mapato na matumizi ya Serikali. Sisi kama Watanzania inabidi tusimamie hepo. Hivyo basi, tusijisahau tukachagua tu uongozi kwa ahadi, lakini ni lazima tuwe tuna mambo haswa tunayoyataka. Kukipigia kura chama, haijalishi cha rangi gani, ni jambo moja, na kukibana kitekeleze ni jambo jingine. Uzalendo wa utanzania lazima uwepo. Tuweke siasa pembeni, kwenye ukweli katika hili tuwe wazi, tumkosoe yeyote aliyekosea, na tusiunge mkono lolote ambalo si sahihi. Ikumbukwe kwamba madaktari na wagonjwa ni wanachama wa vyama vyote, na hivyo basi sioni sababu ya wanasiasa na sisi watanzania kuingiza siasa katika hili. Sasa Tanzania limekua tatizo, kila kitu tunaweka siasa na tunasahau real solutions.
 
Waandishi wathibitishe nini wakati thread hii imeanika kila kitu? Pictures says more deeply than words. Kiziwi umpe nini asikie wimbo wa Rose Mhando "Jipange sawasawa"
Ni kweli hii thread imeanika, lakini media pia ni ma-whistle blowers, magazeti, redio, TV husikika kwa wasiofika hapa Jamii Forums
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom