Ofisi za TCU zavunjwa, computers na nyaraka nyeti zaibwa!

Jamani ,hivi si kuna tukio kama hili lilitokea miaka miwili au mmoja uliopita na kukaibiwa benzi ya mkurugenzi, laptops na cmuputers, na walinzi tena wakampuni binafsi wakaleweshwa madawa ya kulevya? Hawakujifunza chochote?

walinzi wanapenda kula kula hovyo bila kuzingatia wanapokea chakula kutoka kwa nani
 
TCU haitoi vyeti uko Tanzania ipi??? wanahusika na kuchagua wanafunzi wa kwenda vyuoni tu.
namaanisha wao hufanya kazi kama za ku-verify waliosoma nje n.k, means kama rekodi zimepotea kutakua na udanganyifu mkubwa.
TCU haifanyi kazi ya kuchagua wanafunzi wa kwenda vyuoni tu, pamoja mkuu!!
 
Kama si UFISADI basi ujue kuna kitu hapo maana wezi hupoteza vielelezo kwa njia hio, sasa na wale waliojaza tayari sijui watawaambia wajaze tena? huku ni kutiana ulofa
 

Hizo ofisi za TCU zimevunjwa na Chadema. Wao ndiyo waliogiza wale vijana kuvamia ofisi hizo na kuiba nyaraka kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Rais wake Jakaya Kikwete, ni dhaifu.

Wananchi tutoke barabarani kukilaani chama hiki kwa hatua yake ya kufadhiri wezi: Vyuo vyote nchini vimeshikwa na Chadema – Nape Nnauye.
hata yale mabilioni ya epa na rada chadema ilifadhili hili ccm ionekane dhaifu
 
TCU nako kuna nini tena? Kuibiwa nyaraka muhimu si suala la kutisha maana nyaraka muhimu walizo nazo ni wanafunzi walioomba kujiunga na vyuo.

Kama vipi watawaomba ku-reapply ila 30,000/- ndo hivo wasiombe tena na vyuo vikuu ambavyo ndiyo vinavyotaka wanafunzi toka kwao wataviomba vitume tena entry qualifications kama hazipo.

Wewe unayesema ni CDM sijui kama nadharia hii itafanya kazi maana kazi ya kulinda usalama wa raia na mali ni kazi ya serikali kwa hiyo kama CDM ndiyo wenye dola watakuwa wamehusika vinginevyo hawahusiki na ulinzi wa ofisi za serikali.

Usifikiri TCU ni NGO ni ofisi ya serikali!
 
Hii ni katika harakati ya kuhalalisha PhD fake. Hapa sasa Ndugu Msemakweli atakuwa matatani kwa yatakayofuata.
 
Hivi ofic za TCU police huwa hawalindi? Mi naona kuna umuhimu office nyeti ma cop wapewe kulinda.
 
Ofisi za TCU zimevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi. Walinzi wake wamelewa kwa kinachaodhaniwa ni madawa ya kulevya waliyonyweshwa na hadi majira ya mchana huu hawajaamka. Eneo la ofisi liko chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Source: ITV.

Hiyo TCU ni Tanzania Commission for Universities au nyingine?
 
Hivi ofic za TCU police huwa hawalindi? Mi naona kuna umuhimu office nyeti ma cop wapewe kulinda.

Hao walinzi labda ndiyo polisi wenyewe! si mnajua wanavyopenda vya bure? watakuwa walipewa zawadi ya juice wakaanza kusherekea!
 
Ninyi CDM mnataka serikali hii isitawalike. Sasa ngoja tuwaonyeshe. Tutavamia ofisini zenu na kuiba kila kitu, kisha tutajibu mapigo kwa kusema, "Dk. Slaa naye ni dhaifu. Aruhusu wezi kuvunja ofisi yake." Nape Nnauye.
 
wewe kweli mwehu

Hizo ofisi za TCU zimevunjwa na Chadema. Wao ndiyo waliogiza wale vijana kuvamia ofisi hizo na kuiba nyaraka kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Rais wake Jakaya Kikwete, ni dhaifu.

Wananchi tutoke barabarani kukilaani chama hiki kwa hatua yake ya kufadhiri wezi: Vyuo vyote nchini vimeshikwa na Chadema – Nape Nnauye.
 
Back
Top Bottom