OFISI ZA TCU......Msaada please....!!

NGOSWE.120

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
219
233
Wakuu wana Jf,

Naomba kufahamishwa Ofisi za TCU zilipo hapa jijini DSM, I mean ni mitaa ipi/ maeneo gani.

Je nikitokea Ubungo nipande dala dala za wapi na nishukie kituo gani?

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Ngoswe.120
 
Panda basi mpaka mwenge halafu chukua basi kwenda kariakoo au posta teremkia kituo cha sayansi. Fuata njia ya mikocheni kwenda kwa mwalimu nyerere baada ya Rose Garden Bar kwenye kona ile kali utaziona zipo mkono wa kulia kama unakwenda kwa mwalimu.
 
Panda basi mpaka mwenge halafu chukua basi kwenda kariakoo au posta teremkia kituo cha sayansi. Fuata njia ya mikocheni kwenda kwa mwalimu nyerere baada ya Rose Garden Bar kwenye kona ile kali utaziona zipo mkono wa kulia kama unakwenda kwa mwalimu.
Mkono wa shoto kama watokea rose garden......
 
Nawashukuru sana wakuu hapo juu kwa kunisaidia kunipa hiyo ramani/maelezo ya kuniwezesha kufika hapo tcu!

Mungu awabariki sana!
 
Duh...nimegoogle hii mambo nikaletwa hapahapa nyumbani...shukrani sana wakuu! nadhani kibajaj kinanihusu maana hata huko kwa mwalimu Nyerere sipajui!
Hizo ofisi ziko upande huo huo wa sayansi ama ni lazima kuvuka barabara!??
 
Duh...nimegoogle hii mambo nikaletwa hapahapa nyumbani...shukrani sana wakuu! nadhani kibajaj kinanihusu maana hata huko kwa mwalimu Nyerere sipajui!Hizo ofisi ziko upande huo huo wa sayansi ama ni lazima kuvuka barabara!??
Umeambiwa kuelekea kwa Mwalimu Nyerere = the opposite side of COSTECH (SAYANSI). So Kibajaj atakufikisha
 
Ukishuka Sayansi, utakuta kuna bajaj/pikipiki waulize Office Tcu watakuelekeza! Ni umbali wa 600M! All the best!
 
Back
Top Bottom