Ofisi za CCM Pemba zachomwa moto, CCM walaani hicho kitendo

Habari za hivi punde zinasema kuwa ofisi za CCM Pemba zimechomwa moto na nyumba za wafuasi wa CCM kupigwa x.

Kiongozi wa CCM kutoka kisiwani humo amewataka wafuasi wa chama hicho wawe watulivu hadi tarehe 20 Machi ambapo watalipiza kisasi kwa kuipa CCM ushindi wa kishindo

Chanzo: Radio Uhuru

Nimeikuta hii : link CCM Militias Au (Mazombi) Yaingia Pemba Kwa Style Ya Kuweka X - Mzalendo.net
Inawezekana huo ni mkakati wa fisiem baada ya vyama 9 kukataa kushiriki uchaguzi wanatafuta njia ya kutokea.

CCM wana mbinu nyingi wakisaidiwa na vikosi vyenye vitu vya ncha kali.

Mengi tutayashuhudia. Kubaka demokrasia ina gharama yake na wanaoteseka ni walalahoi.
 
Mambo ya Zanzibar eti hayamuhusu Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilhali kura zilikuwa zinamuhusu.

Kichekesho cha namna yake hiki!!!
 
Yakhe, mimi si ishi Unguja wala Pemba, nimeuliza tu kwa nini Pemba?
Imeandikwa hivi:

Ama mimi sina budi ila kuwajuvya Yaliojiri Hapa Kwetu Pemba katika Wilaya ya Mkoani. Kama munavojuwa Ndugu Wazanzibari Tokea SEfu Ali Iddi Awe Makamo wa 2 Wa Raisi ameweza kufanikiwa Kutumia Pesa Nyingi sana za Serikali na Ruzuku Wanazopewa na SMT kwakuimarisha WAHUNI ambao Wamekuwa Wakila na Kulala Katika Kambi za MAJESHI.. Vikundi Hivo Vilitayarishwa Tokea 2012 pale Ilipokuja Suali la Wazanzibari Kutaka Mchakato Wa Katiba Uzungumzie Suali la Muungamo. Sina haja yakuwarudisha Nyuma naamini kila mmoja wetu anajuwa kwa Nini Sefu Ali Iddi ametumia pesa nyingi kwa Ajili ya Mazombi?.

Mazombi au CCM MILITIA wamefanikiwa sana kupiga, kuuwa na kujeruhi Wazanzibari wasio na hatia Hapa katika Kisiwa cha Unguja. Nakuweza Kupata Baraka zote za Viongozi wa Ngazi za Juu, POLISI na KMKM na hata kuhatarisha Hali za Raia Wa Kizanzibari hasa Wale wanaoaminiwa kama ni Wapinzani. Mazombo hayo ya CCM tayari yamepelekwa Pemba lakini wameambiwa Huko Waingie na Style Mpya na wasianze kupiga na kujeruhi Watu au Kutembea mchana kama Wanavowafanyia MIJIBWEGE ya MABADILIKO hapa UNguja. Pemba Wametakiwa Kwanza wawe na LAW PROFILe au kwa kingereza Tunasema ” They Should Keep Up Their Appearence” mpaka pale Kisiwa cha Pemba kitakapojazwa Askari Wa KIKURYA ambao Hawajawahi hata kusafiri. Hapo Ndipoo Mazombi hayo yataanza Kufanya Uharamia wa Ku-uwa, kupiga, kuiba, kuchoma moto mali na hata kunajisi Visima, Madrasa, Shule na Wanawake au Watoto WaDOGO.

Hata Hivo Mazombi waliokuja Pemba Wamekuja na Style yakupachika X katika Nyumba za MaCCM Wenzao. Huu ni mpango maalumu uliopangwa Ili CCM na Serikali ya Dictator ya Dr Sheni Ipate Sababu Yakuwaingilia Vijana NGANGARI WA PEMBA NA KUWAKAMATA NA KUWATIA NDANI ILI WAPUNGUZE KASI YA KUHOFIA HUJUMA KATIKA UCHAGUZI WAO.

BAHATI NZURI HABARI ZA KUTIWA NYUMBA X ZILIENEA KATIKA SOCIAL MEDIA NA HATA LICAL PLACES NA WENYEJI WA HAPO KWAVILE WENGI WAO HUISHI NA KUSAIDIANA NA WAPENZI WA CUF. WAMEAMUA KUKAA PAMOJA NA KUTAKA KUSOMA HALBADIRI YA YOYOTE YULE ALIEKUJA USIKU NA KUWEKA X KATIKA NYUMBA ZA CCM NILAZIMA AJULIKANE KWA KUNUILIA NA KUSOMA KISOMO CHA DUA YA MAAPIZO. vijana wa CCm waliposikia hivo Ilibidi Watoe Siri na waseme kwamba Wao CCM Ndio waliopita Usiku na Kutia X katika nyumba za CCM Wenzao ili Ionekane kwamba ni mpango wa Vijana wa CUF ambao wanapinga marudio ya uchaguzi.

Lila na fila huwa hazitangamana , kama tunakumbuka CCm walifanya mipango mengi yakutaka kuhujumu Uchaguzi na hata kununua T-Shirt za CUF kwa bei ya juu ili Wazitumie kwa hujuma yakuchafua Amani. Nashangaa Katika vitendo hivo vyote vya Kiharamia, Jaji na Polisi wamenyamaza kimya.

Jee Polisi na Jeshi munataka tuchukue hatua Wenyewe, Tunawambia CCM kwamba kila munalolifanya cc tunalijuwa tu na Inshallah hamufanikiwi hata kidogo na njama zenu zakutaka kunywa DAMU za Wazanzibari Wasio na Hatia..

Enough is Enough,, Sheni na CCM Must Go..
Source:mzalendonet
 
Kwa wale waliopewa dhamana ya nchi hii na wapo wanaangalia na hawachukui hatua,kuna siku wataulizwa kwa dhamana uliyopewa je ulichukua hatua gani kuzuia haya yasitokee,hata kama sio hapa duniani basi huko tuendako baada ya kifo.
Nawahurumia sana watoto na akina mama kwa kuwa ndio waathirika wakuu.
 
Habari za hivi punde zinasema kuwa ofisi za CCM Pemba zimechomwa moto na nyumba za wafuasi wa CCM kupigwa x.

Kiongozi wa CCM kutoka kisiwani humo amewataka wafuasi wa chama hicho wawe watulivu hadi tarehe 20 Machi ambapo watalipiza kisasi kwa kuipa CCM ushindi wa kishindo

Chanzo: Radio Uhuru
Haya ndiyo matatizo makubwa ya viongozi wetu.
Kuogopa ukweli.

CCM wapate wapi ushindi wa kishindo ilihali majuzi tu wameshindwa uchaguzi?
 
amani!amani! amani!
Mungu apishilie mbali uvunjifu wa amani na oampe hukumu ya haraka yeye anayesababisha haya yote!
 
Kama sisi-em walishinda uchaguzi inamaana wapo wengi ukilinganisha na CUF hii ina maana kwamba ukichukua CCM ukajumlisha na Police znbr ukajumlisha na serikali ya tanganyika watakao umia zaidi ni wapinzani.

walishinda uchaguz upi na wakat mmefuta matokeo au ndo mnaanza kutengeneza mazingira
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom