Ofisi ya Mbunge yavunjwa na kuibiwa kompyuta na nyaraka

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Habari nilizopata toka polisi Magomeni ni kwamba ofisi ya mbunge mmojawapo wa Manispaa ya Kinondoni imevunjwa na kuibwa kompyuta na nyaraka mbalimbali. Kwa mujibu wa chanzo hicho wizi huo umetokea juzi usiku. Hatahivyo, chanzo hicho ambacho hakikuta kutaja jina kimeeleza kuwa kituo chao kimeelekezwa kuwa taarifa za kina zitatolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari hapo kesho.
 
Hujawa na taarifa bado,sio busara kupost jambo usio na uhakika nalo! ILA
Ninasuspect watakuwa CDM hao ila sina ushahidi ninashuku tu! nawaomba polisi waanze na hiki chama maana kinatupa shida sana mitaani.
 
hii itakuwa operesheni ya kukamata mtandao wa wauza unga tu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Hujawa na taarifa bado,sio busara kupost jambo usio na uhakika nalo! ILA
Ninasuspect watakuwa CDM hao ila sina ushahidi ninashuku tu! nawaomba polisi waanze na hiki chama maana kinatupa shida sana mitaani.

Heri mimi sijasema kulikoni wewe unayeropoka tu. Una uhakika gani kama ni wa CDM; pale magomeni zipo ofisi za Mbunge wa Kawe (CDM), Mbunge wa Ubungo (CDM), na Mbunge wa Kinondoni (CCM);

Sasa una uhauhakika gani kuwa ni Mbunge yupi aliyeibiwa na pia ni wafuasi wa chama kipi waliohusika kama kweli itikadi za kisiasa zipo.

Acha kuropoka ndugu yangu usije valishwa SHANGA NA KHANGA MOJA MCHANA KWEUPE NA UKAPITISHWA UNASHANGILIWA BARABARANI

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hujawa na taarifa bado,sio busara kupost jambo usio na uhakika nalo! ILA
Ninasuspect watakuwa CDM hao ila sina ushahidi ninashuku tu! nawaomba polisi waanze na hiki chama maana kinatupa shida sana mitaani.

Akili za kuazima hizi.
 
Hujawa na taarifa bado,sio busara kupost jambo usio na uhakika nalo! ILA
Ninasuspect watakuwa CDM hao ila sina ushahidi ninashuku tu! nawaomba polisi waanze na hiki chama maana kinatupa shida sana mitaani.

Kuna mtu hapa jamvini alikuwa na kausemi kake kuwa " A silent fool is counted wise". Ungekaa kimya tu tungekosea kudhani kuwa una busara
 
Heri mimi sijasema kulikoni wewe unayeropoka tu. Una uhakika gani kama ni wa CDM; pale magomeni zipo ofisi za Mbunge wa Kawe (CDM), Mbunge wa Ubungo (CDM), na Mbunge wa Kinondoni (CCM);

Sasa una uhauhakika gani kuwa ni Mbunge yupi aliyeibiwa.

Acha kuropoka ndugu yangu usije valishwa SHANGA NA KHANGA MOJA MCHANA KWEUPE NA UKAPITISHWA UNASHANGILIWA BARABARANI

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Huyu akili zake zilifukiwa na Sheikh yule aliyekuwa anawaongoza.
Mtu anakurupuka utafikiri kashikiwa mtutu.
Akili za makada utaziona tu, hata signature yake.
 
Hujawa na taarifa bado,sio busara kupost jambo usio na uhakika nalo! ILA
Ninasuspect watakuwa CDM hao ila sina ushahidi ninashuku tu! nawaomba polisi waanze na hiki chama maana kinatupa shida sana mitaani.

Kama ulisuspect mbona hukuileta kama tetesi? Na hiyo notion yako kuwa ni CDM umeitoa wapi, na inakusumbua wewe na nani huko mtaani? Na hiyo signature yako, kipimajoto umeendesha lini na kwa vigezo vipi?
 
Back
Top Bottom