Ofisi ya CCM yafungwa na kugeuzwa ya CHADEMA:CCM yapoteza Mali na wanachama

Ole Sendeka akae mkao wa kufungasha virago.. namuona kabisa Ole Milllya akichukua jibo
 
Je kuchukua pango na samani za chama kingine na kuzigeuza kuwa za chama chako sio uvunjifu wa sheria na amani? Inabidi kuwaelimisha hawa wanachama wapya kuwa lazima wazingatie utawala wa sheria hata kama wana jazba ya kutaka kuhama chama cha mapinduzi. Naongea haya nikiamini kuwa CCM walipanga kwa mkataba na mmiliki wa nyumba yenye ofisi yao na pia samani zilizokuwa ndani ya ofisi hiyo ni mali ya CCM
Mwenye nyumba mwenyewe aliyewapangisha kahamia CDM na bado alikuwa anadai pesa ya pango na samani zilinunuliwa na hao hao waliohama, labda cha msingi ni CCM kudai bendera na muhuri wake, usikute hata hiyo bendera ilinunuliwa na hao hao waliohama.
 
Umenena vema sana mkuu......
 
Mkuu tata, unajua hizo mali zilipatikanaje mfano mimi nilichangea jengo mwingine akanunua viti kwa pesa yake je siku tukitaka kuhamia chama kingine kwa pamoja kwanini tusiondoke na vitu vyetu...Je masha alivyo ng'oa vitasa na mapazia kwenye ofisi ya bunge pale mwanza mlihoji kwanini alifanya hivyo..
Hahahaa Crashwise bana una kumbukumbuuuu!!
 
hapo patamu maana kila kitu waswahili wanasema haba na haba hujaza kibaba tutafika tu
 
Katika tukio ambalo halikutarajiwa na la kushangaza vijana zaidi ya 50 waliokuwa wanachama wa CCM Tawi la Cairo mjini Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameishusha bendera ya Tawi hilo na kuipandisha ya CHADEMA huku kila kitu ikiwemo ofisi,samani na wanachama wote kuhamia CHADEMA.

Wanachama hao wamesema wameamua kufanya tukio hilo la kushangaza kutokana na kudai kwamba CCm imepoteza dira na mwelekeo hadi kusababisha maisha kuzidi kuwa magumu na mfumuko wa bei.Pia wamesema wameamua kumuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya aliyejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA mwezi uliopita.

Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa CCM kata hiyo Sifael Saitore mbali ya kushtushwa na tukio hilo aliahidi kutafuta kiwanja sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya Tawi kwani awali Tawi hilo lililojiunga na CHADEMA halikuwa katika eneo linalomilikiwa na CCM.

Source:Mwananchi Ijumaa Uk.10

Ni HUZUNI KUBWA kwa vijana wanaoendelea kung'ang'ania Chama Cha Magamba, na kutokuona mbali...! Siku zinakuja watakaposema, afadhali na jana, 'tungewahi kutoka tusingekuwa ktk hali hii'. Hakika, kwa wanaoona mbali kidogo watagundua kuwa, kwa sasa kila Jimbo la Ubunge, Kata, Kijiji, Kitongoji na Mashina yanayoonekana mitaani dalili zote zinadhihirisha kuwa yapo ktk mpito, ni 'potential Chadema's' na hivyo wanaCCM waliopo mle 'wanaishi tu kwa matumaini'.
 
Katika tukio ambalo halikutarajiwa na la kushangaza vijana zaidi ya 50 waliokuwa wanachama wa CCM Tawi la Cairo mjini Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameishusha bendera ya Tawi hilo na kuipandisha ya CHADEMA huku kila kitu ikiwemo ofisi,samani na wanachama wote kuhamia CHADEMA.

Wanachama hao wamesema wameamua kufanya tukio hilo la kushangaza kutokana na kudai kwamba CCm imepoteza dira na mwelekeo hadi kusababisha maisha kuzidi kuwa magumu na mfumuko wa bei.Pia wamesema wameamua kumuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya aliyejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA mwezi uliopita.

Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa CCM kata hiyo Sifael Saitore mbali ya kushtushwa na tukio hilo aliahidi kutafuta kiwanja sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya Tawi kwani awali Tawi hilo lililojiunga na CHADEMA halikuwa katika eneo linalomilikiwa na CCM.

Source:Mwananchi Ijumaa Uk.10

Nape - na hawa tena walikuwa magamba na wenye ngozi nene tayari mlishawaandikia barua za kutaka kuwafukuza uanachama?
 
Kweli M4C, haina huruma!

Hadi jengo na samani??!!

Big up sana makamanda, Ole Sendeka aanze kujiandaa na maisha ya kustaafu sasa!!
 
Katika tukio ambalo halikutarajiwa na la kushangaza vijana zaidi ya 50 waliokuwa wanachama wa CCM Tawi la Cairo mjini Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameishusha bendera ya Tawi hilo na kuipandisha ya CHADEMA huku kila kitu ikiwemo ofisi,samani na wanachama wote kuhamia CHADEMA.

Wanachama hao wamesema wameamua kufanya tukio hilo la kushangaza kutokana na kudai kwamba CCm imepoteza dira na mwelekeo hadi kusababisha maisha kuzidi kuwa magumu na mfumuko wa bei.Pia wamesema wameamua kumuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya aliyejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA mwezi uliopita.

Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa CCM kata hiyo Sifael Saitore mbali ya kushtushwa na tukio hilo aliahidi kutafuta kiwanja sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya Tawi kwani awali Tawi hilo lililojiunga na CHADEMA halikuwa katika eneo linalomilikiwa na CCM.

Source:Mwananchi Ijumaa Uk.10

Vijana wameamua kuanza kurudisha mali za wananchi zilizotekwa na CCM. Mbio hazijashika kasi bado, kasi itakapoongezeka zaidi CCM watachanganyikiwa zaidi kuliko inavyotokea sasa kwani wanashikwa na kigugumizi cha kujibu mapigo hayo.
 
Absolutely Yes!!.....
 
Back
Top Bottom