Ofisi ya CAG yataka kuwa huru

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173

Ofisi ya CAG yataka kuwa huru

Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 7th February 2011 @ 15:11

LICHA ya ubora wa kazi za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutambuliwa kimataifa, bado imeshindwa kupanda daraja kwa muda mrefu kwa kuwa wafanyakazi wake wanaajiriwa na Serikali.

Kutokana na kikwazo hicho, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Ofisi hizo kwa nchi zinazozungumza Kiingereza barani Afrika (AFROSAI-E), ameitaka Serikali ilipatie ufumbuzi tatizo hilo.

Utouh amependekeza Serikali ifanye marekebisho ya sheria ya ajira ili kuipa ofisi yake mamlaka ya kuajiri wafanyakazi bila kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa Utouh, kitendo cha Serikali kuajiri wafanyakazi wa ofisi hiyo kunawafanya waonekane kama watumishi wa umma, jambo linalowaondolea sifa ya kupanda daraja katika AFROSAI-E na hivyo kubaki daraja la kwanza badala ya la tatu linaloistahili.

Aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kufungua mkutano wa wafanyakazi zaidi ya 600 wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) kutoka kanda zote nchini.

“Tuna vigezo vingi vinavyothibitisha uwezo wetu na kazi zetu zinathaminiwa na mataifa mengine kwa ubora, tunakamilisha ripoti zetu kwa usahihi ndani ya muda lakini haya yote hayajasaidia kutupandisha daraja kama wenzetu kwa kuwa wafanyakazi wetu wanaajiriwa na Serikali na kutambuliwa kama watumishi wa umma.

“Hii haitakiwi kwa sababu inaupa umoja wasiwasi kama tunafanya ukaguzi wa hesabu za Serikali na taasisi zake kwa uhuru unaotakiwa, inafaa tuwe taasisi huru, tuajiri wafanyakazi na kupanga mishahara yetu wenyewe,” alisema Utouh.

Kwa mujibu wa CAG, kitendo cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kuajiriwa na Serikali kinaleta wasiwasi kuhusu ukaguzi unaofanywa na mwajiriwa kwa muajiri wake.

“Tunawajibika kuwa na uaminifu mkubwa lakini kwa kuwa tupo kwenye umoja huo hatuna budi kufuata masharti yanayotakiwa, tumefikisha maombi yetu kwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma muda mrefu lakini hatujapata majibu...tunaomba Serikali iliangalie hili na kulifanyia kazi.” alisema.

Mbali na ombi hilo, Utouh aliilalamikia Hazina kwa kuikwamisha ofisi hiyo kuanzisha mfuko wa kuendesha shughuli zake na kumuomba Luhanjo aingilie kati kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo, Luhanjo alijibu kuwa Serikali ilikwishaelezwa kuhusu matatizo hayo na inaendelea kuyafanyia kazi.

Wakati huo huo, Luhanjo aliwataka wakaguzi hao kuwafichua wabadhirifu wa rasilimali za umma bila kujali kuchukiwa, kwa kuwa Mungu mwenye kutambua ukweli wao, atawasimamia na kuwaepusha na wabaya wao.

Luhanjo alisema anatambua kazi hiyo ina changamoto nyingi ikiwamo kuchukiwa kwa wakaguzi wa hesabu kiasi cha kutishiwa na kundi la watu wasiopenda kuwajibika, wanaoendekeza ufujaji wa mali na fedha za umma bila kujali athari wanazosababisha katika nchi.

“Msibabaishwe na wasiotaka kuwajibika na Mungu atawabariki, wafichueni wabadhirifu, ndio wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu...msikubali wawakatishe tamaa kwa sababu hilo ndilo lengo lao, wajibikeni kwa bidii na msiache mafanikio mliyoanza kuyapata yatoweke.”


 
PHP:
LICHA ya ubora wa kazi za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutambuliwa kimataifa, bado imeshindwa kupanda daraja kwa muda mrefu kwa kuwa wafanyakazi wake wanaajiriwa na Serikali. 
 
Kutokana na kikwazo hicho, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Ofisi hizo kwa nchi zinazozungumza Kiingereza barani Afrika (AFROSAI-E), ameitaka Serikali ilipatie ufumbuzi tatizo hilo. 
 
Utouh amependekeza Serikali ifanye marekebisho ya sheria ya ajira ili kuipa ofisi yake mamlaka ya kuajiri wafanyakazi bila kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Hoja ya muhimu siyo kufurahisha mataifa mengine ila kuimarisha taasisi za umma ziweze kufayna kazi bila hofu ya kuadhibiwa na Ikulu ambakoi ndiko chimbuko la rushwa zote.........................
 
not only independent but also must be seen independent in the public eyes..........................
 
ina make sense.....huwezi kuwa Mkaguzi wa Serikali halafu na wewe pia ni sehemu ya Serikali.....nchi FUMBO
 
Ingekuwa ishu ya kuiazibu chadema sheria hii ingeletwa bungeni mapema sana lakini kwa sababu ni ya kuwabana mafisadi ambao ndio wao watakwambia ombi limefika linafanyiwa kazi mara tuko kwenye mchakato na mambo mengi ili waendelee kulinda interest zao ila yana mwisho hayo
 
Back
Top Bottom