Ofisi ya Bunge: Mpendazoe bado ni mbunge wa Kishapu

Yes, Ofisi ya Bunge wanafuata utaratabu. Hatuwezi kuwalaumu.

Hili suala limeonyesha udhaifu wa huu utaratibu...ipo haja ya kuweka idadi ya siku (mfano 7 au 14) ambazo Chama chochote kinatakiwa kitoe taarifa Tume ya Uchaguzi kuhusu kujiondoa/kuondolewa uachama kwa kiongozi/ mgombea yoyote.

Udhaifu huo ndio unaoiwezesha CCM kukaa kimya kwa manufaa ya chama chao.

Lakini hata bila kupewa siku, mbona majimbo ambayo yalipoteza wabunge kwa sababu zozote zile yalitangazwa mara moja? Nadhani CCM hawana haraka kwa sababu hakuna uchaguzi mdogo huko Kishapu. Na kwa kudhania hivyo, wanajikuta katika mazingira ya ajabu kwa kushindwa kutoa taarifa kuwa mbunge wao amejivua uanachama na kupoteza sifa za kuwakilisha jimbo lake.

Labda wataalamu watusaidie, mwenye jukumu la kutaarifu tume ya uchaguzi/bunge kuwa Mbunge X amepoteza sifa za kuwa mbunge kwa sababu kadhaa (Y, X) ni nani? Na kama ni mbunge mwenyewe, hali inakuwaje katika mazingira ya kifo?
 
Kwangu mimi alichofanya Mpendazoe ni sahihi kabisa na amekifanya kwa umakini mkubwa sana. Ameitisha "press conference" na bila kumung'unya maneno akautangazia Umma kuwa anajiondoa katika chama kilichopoteza dira, kinachokumbatia majizi, kilichojaa mafisadi na kilichotekwa nyara na matajiri limbukeni. Akazidi kushindilia msumari kwa kusema ana mpango wa kujiunga na chama kipya cha CCJ ambacho hadi wakati huo kilikuwa tu na usajili wa muda - kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, CCM kimyaa.

Sasa shuhudia cha ajabu eti mpaka leo tunashuhudia CCM ikishindwa kabisa kulishughulikia hili swali kama katiba yake inavyotaka. Badala yake eti inasubiri awaandikie rasmi kuwa kweli kahama - ukisikia chama kukosa uongozi makini ndiko huku. Mpendazoe alichokataa ni kutanguliza maslahi ya CCM mbele ya wapiga kura waliomchagua ambao kwa asilimia kubwa si wana CCM. Mpendazoe kwa kufanya hivyo ametimiza wajibu wake, boli sasa lipo kwa CCM kupitia katiba yake na kwa ofisi ya Bunge kupitia katiba ya nchi.

Kupoteza Ubunge ni matokeo tu ya uamuzi wake wa kukataa kuendelea kushirikiana na wezi, period. Katiba ya nchi inaeleza wazi kabisa nafasi ya Ubunge inavyoweza kuwa wazi na hivyo hivyo katiba ya CCM iko wazi jinsi mtu anavyoweza kupoteza uananchama - hakuna sehemu hata moja inaposema mpaka urudishe kadi. Yaani uachane na genge la wezi halafu urudi kwao kuwataarifu kuwa umekoma kuwa mwananchama wao, duh ! - wakikukolimba je ? Mpendazoe kazi kamaliza, sasa wengine nao wahangaike na kama wanashindwa kumeza shauri yao.
 
Kupoteza Ubunge ni matokeo tu ya uamuzi wake wa kukataa kuendelea kushirikiana na wezi, period. Katiba ya nchi inaeleza wazi kabisa nafasi ya Ubunge inavyoweza kuwa wazi na hivyo hivyo katiba ya CCM iko wazi jinsi mtu anavyoweza kupoteza uananchama - hakuna sehemu hata moja inaposema mpaka urudishe kadi. Yaani uachane na genge la wezi halafu urudi kwao kuwataarifu kuwa umekoma kuwa mwananchama wao, duh ! - wakikukolimba je ? Mpendazoe kazi kamaliza, sasa wengine nao wahangaike na kama wanashindwa kumeza shauri yao.

hahaha.. Mag3.. this is what I missed kutomumunya maneno.. CCM wanataka wafanywe kuwa ni muhimu! Jamaa kimsingi kaamua kuwafanya CCM kuwa ni irrelevant!
 
Haisumbui sana akili kutokana na utendaji wa kazi wa wabunge wetu na bunge lenyewe.kitu muhimu hapa ni uchaguzi unakuja mpendazoe agombee kwa chama anachotaka yeye. Hilo swala kwamba yeye ni ccm bado pale bungeni sio tatizo hivyo vikao vichache havitaleta tofauti yoyote yale hata kama kuna kura zinapigwa kupitisha sheria bado ccm watapata kura za kutosha.
 
Mwanzo nilifikiri mwanasiasa mwenye papara ni Mrema peke yake, kumbe sivyo, avumaye baharini papa, kumbe wengine wapo!

Kwa taarifa yako, Mpendazoe sio mrema na kitu alichokifanya ni kielelezo cha mambo mengine yatakayofuatia!! Mpendazoe sio KIHIYO kama Mrema anajua anafanyanini na wale waliosema kuwa hatapata kiinuamgongo chake sasa wamefahamishwa na katibu wa bunge kuwa yeye wanamtambua kuwa bado ni mbunge halali wa Kishapu mpaka hapo yeye mwenyewe ATAKAPOWAALIFU KWA MAANDISHI KUWA ubunge wake umekoma kufuatana na taratibu za bunge!! Mpendazoe hana papara bali ni makini!!
 
Kasheshe,

Mpendazoe mpaka sasa hajaenda Kishapu kwa waliompigia kura kuwa mbunge wao 2005; huyu kweli anajua umuhimu wa wapiga kura?

Nakubaliana na wewe, alitakiwa apeleke barua bungeni na wakati ule ule barua inafika basi angewajulisha wananchi wa Kishapu juu ya uamuzi wake. Lakini kwa Tanzania viongozi wetu huwa hawawajali waliowapa madaraka ndio maana hata ambaye anataka kuwa mkombozi wao bado anafanya makosa yale yale.

Mpendazoe alitangaza kuwa si mwanachama tena wa CCM mbele ya byombo vya habari; hatukumsikia Makamba wa Tambwe Hiza wakimdai au kumuulizia barua ya kujivua Uanachama! Tena hatukuwasuikia CCM wakikanusha kuwa hawatambui kujivua kwake Uanachama; Bunge na Wakereketwa wengine mnadai kuwa ati bado ni Mbunge! Hizo ni porojo tu za kirasimu na zisizo na maana yoyote. Kama hamuamini kuwa Mpendazoe si M-CCM tena basi endeleeni kusubiri achukue fomu za kugombea Ubunge kupitia CCM. Tena tujiulize, hivi wakati Mpendazoe anakuwa Mbunge aliwaandikia Ofisi ya Bunge kuomba kazi ya Ubunge?

Suala la kuwajulisha watu wa Kishapu ni suala la wakati tu tena wakati wowote, mbona CCM huko Kishapu wameshaanza kumsema vibaya na kuandamana kwa kumbeza? Acheni hizo, Mpendazoe ana akili na anajua anachikifanya, tatizo ni ninyi wakereketwa wa CCM. Endeleeni kumtambua kama Mbunge nadhani baada ya muda uliowekwa kwa Mbunge kuvuliwa Ubunge kwa utoro Spika na Bunge watatoa taarifa ya kumtimua Ubunge! Just wait patiently.
 
Ndio mambo ya kienyeji enyeji hayo. Bunge lazima wawe waangalifu na mazingaombwe ya CCM. Huko tunakokwenda CCM watang'olewa tu wapende wasipende Tanzania ya jana sio ya leo. Wao waendelee kuwakumbatia wageni lakini siku zao zinahesabika.
 
kimsingi ndugu zetu hawa haamini kuwa Mpendazoe kweli kaondoka CCM; wanamng'ang'ania kama mchezaji ambaye ameshatoka kwenda timu nyingine na kuwapiga bao kawapiga, na jezi kavaa lakini bado mbona hajamwambia mmiliki.. sasa mmiliki haoni!? Kwa vile Bunge halijapata taarifa rasmi nina uhakika wataendelea kumpa posho yake kama kawaida hadi CCM itakapoamua kutoa taarifa rasmi.

Kasheshe et al wataendelea kupigwa mabao kwa kujitia wajuaji na kwa "jeuri ya chama"!
 
Mimi kwa upande wangu naona yote sawa. Na pengine hii itatusaidia kujua mapungufu katika sheria zetu, ukiangalia suala la mbunge huyu yeye ameamua kuanzia kwenye vyombo vya habari na kutangaza nia yake hiyo. Je kisheria hii inaweza kuchukuliwa ki uzito sawa na kupeleka barua bungeni? Au bado itachukuliwa kwamba ni uvumi hadi hapo atakapofanya hivyo? Na asipofanya hivyo bunge litaendelea kumchukulia kama mbunge bila kuhudhuria bungeni kwa muda gani? Na kama ataamua kuhudhuria bungeni kama mbunge wa CCM nani atamuwekea pingamizi kwa sasa tukirejea kauli ya Chiligati kwamba "yeye katuaga nasi tukamwambia asante" anaweza kuendelea kuwa muwakilishi wa jimbo lake hadi kuvunjwa kwa bunge?

Wajuzi wa mambo ya sheria na kanuni za bunge kwa faida ya wana JF na jamii kwa ujumla mtatusaidia sana kama mtatujibu maswali haya na mengine mengi ambayo nina hakika yatajitokeza.

Natanguliza shukurani.
 
Mimi kwa upande wangu naona yote sawa. Na pengine hii itatusaidia kujua mapungufu katika sheria zetu, ukiangalia suala la mbunge huyu yeye ameamua kuanzia kwenye vyombo vya habari na kutangaza nia yake hiyo. Je kisheria hii inaweza kuchukuliwa ki uzito sawa na kupeleka barua bungeni? Au bado itachukuliwa kwamba ni uvumi hadi hapo atakapofanya hivyo? Na asipofanya hivyo bunge litaendelea kumchukulia kama mbunge bila kuhudhuria bungeni kwa muda gani? Na kama ataamua kuhudhuria bungeni kama mbunge wa CCM nani atamuwekea pingamizi kwa sasa tukirejea kauli ya Chiligati kwamba "yeye katuaga nasi tukamwambia asante" anaweza kuendelea kuwa muwakilishi wa jimbo lake hadi kuvunjwa kwa bunge?

Wajuzi wa mambo ya sheria na kanuni za bunge kwa faida ya wana JF na jamii kwa ujumla mtatusaidia sana kama mtatujibu maswali haya na mengine mengi ambayo nina hakika yatajitokeza.

Natanguliza shukurani.

kwa kweli ndugu zangu mnakatisha tamaa..
 
Hapa ndipo huwa nasema watz tunapenda mambo mepesi mepesi; sheria inasema x, utaratibu unasema y sisi tunasema z tukiulizwa kwanini tunasema "kwa kweli sikutaka kujua x na y ni nini".. Kwenye masuala ya kisheria basi tujaribu japo kidogo kuegemea sheria. Mpendazoe amepoteza uanachama wa CCM kwa kujiunga na CCJ hivyo Ubunge wake kwenye Bunge la Muungano umekoma kwani amepoteza sifa ya kuwa mbunge. Hili siyo gumu kulielewa. CCM ndiye iliyepeleka jina la Mpendazoe kwenye Tume ya Uchaguzi kuwa ni mgombea wao na akagombea na kushinda; sasa kaondoka ni wao wanatakiwa waandike kwa Tume ya Uchaguzi na kuwaambia aliyekuwa mgombea wao kapoteza uanachama; tume ya Uchaguzi inatoa taarifa kwa Bunge. Hivi ndivyo hufanywa mbunge anapopoteza ubunge kwa kufariki au kuondoka kwenye chama chake. Hili siyo gumu hivyo.



Mfano wako haukaribiani na tunalolizungumzia kwani mtu akibadili dini imani yake iko huko kwingine, mengine yanaweza kubakia kuwa ni mapambo tu.. mbona wapo watu wengi tu wana vibuyu ndani ya nyumba zao na mikia ya ng'ombe lakini hawaamini ndumba na hivyo vibuyu.. we have to elevate our reasoning.. this is sad.

Bado nasimamia kuwa CCJ siyo chama rasmi na kama Mpendazoe hatarudisha Kadi yake CCM for sure akisimama kwenye Ubunge atawekewa pingamizi kuwa bado ni mwana CCM. Kwanini Njelu Kasaka hakuweza kugombea Ubunge kwa tiketi ya CUF?
 
Jamaa alitangaza mwenyewe na kwa sauti yake kuwa amehama sasa kipi ni kizibiti muhimu yeye mwenyewe au karatasi( inayoweza kuwa forged). Kwa mtizamo wangu n aona mbunge ndilo limechemka sana. Lini tutaacha mtizamo wa kusubiri kila kitu na siyo kuwa active. Bunge makini lilitakiwa badala ya kutoa maneno ya kijinga kama hayo lilitakiwa liwe limeshamwandikia barua ya kumweleza kuwa amepoteza ubunge wake.

Jamani naomba msaada, hivi kwenda maelezo kutoa msimamo ni sawa na kwenda uwanja wa fisi? Mimi nilidhani pale ni sehemu rasmi ya kutoa maelezao/msimamo na kwamba unaweza hata kufungwa kama mtu atatumia maneno uliyoyasema pale kama ushahidi. Hata mimi ningekuwa mpendazoe siagi uage nini wakati hata malipo yako hawakuripi ingalau pro rata? na kazi amefanya.
 
Bado nasimamia kuwa CCJ siyo chama rasmi na kama Mpendazoe hatarudisha Kadi yake CCM for sure akisimama kwenye Ubunge atawekewa pingamizi kuwa bado ni mwana CCM. Kwanini Njelu Kasaka hakuweza kugombea Ubunge kwa tiketi ya CUF?

huku kunaita kuhamisha magoli... ulisema mwanzoni "hakipo kisheria" nikaonesha kuwa kipo; unasema siyo "rasmi".. which is another way of saying "hakipo" na mimi nasema "kipo rasmi" kina usajili wa muda, uongozi wamuda, na kinafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria. Sasa unaweza kukataa kwa sababu inawezekana hupendi kuukumbatia ukweli hata ukikukodolea macho.
 
huku kunaita kuhamisha magoli... ulisema mwanzoni "hakipo kisheria" nikaonesha kuwa kipo; unasema siyo "rasmi".. which is another way of saying "hakipo" na mimi nasema "kipo rasmi" kina usajili wa muda, uongozi wamuda, na kinafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria. Sasa unaweza kukataa kwa sababu inawezekana hupendi kuukumbatia ukweli hata ukikukodolea macho.


Kuna watu hata ungewambia kwamba hakuna giza (na wakati huo jua liko nje nje kila mtu analiona) bado watakataa kwa sababu waliambiwa (na mtu fulani, labda Boss wao) kuwa usiku unaisha baada ya saa 12 alfajiri. Katika suala hili kuna watu wana hoja ambazo zinaweza kukufanya ukahisi kizunguzungu kwani hata aieleweki kama zinaelea au zimetua juu ya maji. Hili ni tatizo kubwa ambalo litatufanya tuendelee kubaki nyuma kwani bila kushughulika na vitu halisi maendeleo yaendelea kuwa ndoto milele. Inasikitisha kwamba watu wengi bado tunashughulika na vivuli.
 
Katiba ipo wazi kbs, mpendazoe ameshajivua ubunge na sidhani kama kuna haja hata ya kuandika barua kwani alitamka yeye mwenyewe mbele ya waandishi wa habari na kuijulisha tanzania nzima,ni juu ya ofisi ya bunge kutangaza kua jimbo la kishapu ni miongoni mwa majimbo vacant
 
Mpendazoe: Mimi bado ni mbunge
Habel Chidawali, Dodoma


FRED Mpendazoe ambaye hadi anajitoa CCM hivi karibuni walikuwa wa Kishapu, amesema kuwa anaweza kutinga bungeni muda wowote kuhudhuria mkutano wa bunge unaoendelea mjini Dodoma kwa kuwa yeye bado ni mbunge halali.


Mpendazoe aliyejiengua CCM na kujiunga CCJ hivi karibuni alisema kuwa kutokuwepo kwake mjini Dodoma ambako mkutano wa 19 wa bunge unaendelea hakumuondolei sifa yake ya ubunge, ndio maana bunge bado linamtambua katika nyaraka na kumbukumbu zake zote.


Unajua sio kwamba wabunge wote wa bunge hilo wapo katika vikao hivyo, wengine wapo katika shughuli mbalimbali kwa masilahi ya taifa, ndiyo maana na mimi niko mbali kwa ajili ya shughuli zangu. Lakini mimi ni mbunge halali kabisa wa Kishapu, alisema Mpendazoe.


Alifafanua kuwa bado kuna mambo mengi ambayo hayajakamilishwa, hivyo katika kipindi hiki yeye ni mbunge halali kama walivyo wabunge wengine na kwamba, kabla ya kukamilishwa kwa taratibu hizo ana uwezo wa kuingia bungeni.


Kauli hiyo ya Mpendazoe imetolewa siku chache baada ya Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel kusema Ofisi ya Bunge bado inamtambua Mpendazoe kuwa ni mbunge halali na kwamba akifika katika mkutano wa 19 wa bunge unaoendelea ana haki ya kukalia kiti chake.


Mkurugenzi huyo alisema bunge halijapata taarifa rasmi kutoka kwa wahusika kuwa mbunge huyo amejiuzulu nafasi yake au amehama chama chake, hivyo kabla ya kupokea taarifa hiyo wataendelea kumtambua kama mbunge.


Kauli ya Mpendazoe aliitoa kufuatia Mwananchi Jumapili kumtaka kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo kwa kuwa Ofisi ya Bunge imeonyesha kuendelea kumtambua kuwa ni mbunge hahali licha ya kujitoa CCM.


Juzi Ofisi ya Bunge mjini Dodoma, ilitoa kitabu chenye orodha ya wabunge wa bunge hilo ambapo katika ukurasa wa 22 kitabu hicho kimechapisha jina la Mpendazoe kuwa ni mbunge wa Kishapu, ingawa majina ya wabunge wengine waliopoteza sifa kwa sababu mbalimbali yameondolewa.


Katika kitabu hicho kipya, ambacho ni toleo la sita la Aprili mwaka huu, jina lake limo kwenye orodha ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, ukurasa wa 46.

Machi 30 mwaka huu, Mpendazoe alijitoa CCM na kujiunga na CCJ, tukio ambayo lilitikisa medani za siasa Tanzania
Hata hivyo, mbunge huyo alishakaririwa akisema kuwa ubunge si zaidi ya uhuru alio nao, na kwamba alipokuwa mbunge kupitia CCM alikuwa sawa na mtu aliyeko utumwani.
 
Huyu ndiye mpiganaji wenu, hajui wapi pa kujiuzulu? tutaendelea kuona mengi... credibility ya Mpendazoe at test!!! Maskini naona kama anajutia maamuzi yake.


Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Na Salim Said

OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi, inamtambua aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kishapu kupitia Chama hicho hadi hapo itakapopata taarifa rasmi kutoka CCM.

Mpendazoe ni mmoja wa wabunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi ambao walipachikwa jina la makamanda wa ufisadi, kutokana na msimamo wao mkali dhidi ya wanaotuhumiwa kwa kutafuna fedha za umma au kutumia madaraka yao vibaya.


Mbunge huyo alitangaza kukukiacha chama chake na kijiunga kwenye Chama Cha Jamii (CCJ) Machi 30 mwaka huu na kusisitiza kuwa CCM sio mama yake, hivyo hatajilaumu kukihama, kwa sababu alikuwa anaishi kwa matumaini muda wote ndani ya chama hicho.


Akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema,
"Ofisi ya bunge bado inamtambua Mpendazoe kuwa ni mbunge halali wa jimbo la Kishapu kwa sababu haijapata taarifa yoyote rasmi, kutoka kwake au chama chake cha awali."

"Kama Mpendazoe angekuja bungeni leo angekalia kiti chake kwa sababu hatuna taarifa yoyote ya maandishi ya kujiuzulu kwake," alisema Joel.

Joel alisema Ofisi ya Bunge inatakiwa kuwa na barua rasmi ya maandishi ya kuthibitisha kwamba Mpendazoe amejiuzulu nafasi ya ubunge au amekihama chake.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi taratibu na sababu za kuacha ubunge wa Bunge la Jamhuri.

"Sababu ya kwanza ni kwa mbunge mwenyewe kujinasua katika chama chake na kupata vithibitisho vyote, kuugua kwa muda mrefu na madaktari wakathibitisha kuwa hawezi tena kuwahudumia wananchi," alisema Joel.

"Mwisho ni kwa mwanachama kufanya vitendo vichafu na chama kikakunyang'anya uanachama," alisema Joel.

Alisema Ofisi yake haiwezi kukurupuka kwa vile kuna mivutano baina ya Mpendazoe na Chama chake, jambo linaloisababisha ofisi yake kusimamia taarifa rasmi itakayotumwa aidha kutoka chama chake cha awali au yeye mwenyewe binafsi.


Alisema kulingana na taratibu na sheria za bunge, Mpendazoe bado anatambuliwa na ofisi ya bunge kuwa ni mbunge wa Jimbo la Kishapu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Mpendazoe alisema,
"Mkurugenzi amejibu vizuri, ni kweli mimi bado ni mbunge, ila nilichofanya ni kutangaza kwa vyombo vya habari kujivua uanachama wa CCM."

"Ubunge wangu utakoma pale nitakapowasilisha taarifa ya maandishi kwa katibu wa bunge, nakusudia kufanya hivyo siku yoyote kuanzia sasa. Nina mambo yangu binafsi yakikamilika nitakwenda," alisema.
"Siku ile niliyokutana na waandishi Machi 30, sikupata muda wa kwenda ofisi za bunge kupeleka taarifa yoyote, lakini kikatiba natakiwa niwasilishe taarifa kwa katibu wa bunge," alisisitiza Mpendazoe.

"Nitakwenda kwa katibu wa bunge, lakini sikwambii lini hiyo ni taratibu zangu, mimi sio rais wala waziri mkuu. Lakini kikatiba na kisheria natakiwa niwasilishe taarifa ya maandishi katika ofisi ya bunge," aliongeza Mpendazoe.

Alipoulizwa iwapo ataingia bungeni katika mkutano huu wa 19, Mpendazoe alisema hayo ni mambo yake ya faragha (private).


“Unataka nikuambie naenda bungeni halafu kesho muandike Mpendazoe aingia bungeni, mbona mlikuwa hamuniulizi kabla sijahama CCM, mimi ni mtu mdogo bwana sipaswi kutangaza safari zangu,
" alisema Mpendazoe.

Alipoulizwa kwa sasa yuko katika mji gani wa Tanzani, Mpendazoe alikataa kuweka wazi na kujibu tu kwa ufupi.


"Nipo Tanzania, nipo Tanzania bara lakini kukusaidia zaidi ndugu mwandishi."

Kwa upande wake Katibu wa Kamati Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chilgati alisema suala hilo haliwahusu wao kwa kuwa, Mpendazoe aliwambia kwa heri na wao wakamwambia asante.


"Hilo ni suala lake binafsi na mamlaka ya bunge, sisi hatujamfukuza ila yeye ndiye alituaga na sisi tukamwambia asante, hatuna ugomvi na wewe," alisema Chiligati.

"Kama tungemfukuza uanachama sisi ndio tungelazimika kuiandikia ofisi ya bunge kuwa huyu si mwanachama wetu tena, lakini kwa vile yeye mwenyewe ndiye amehama chama, suala hilo ni la kwake na mamlaka ya bunge watajua namna ya kulimaliza,
" aliongeza Chiligati.


kwani yeye ndo kawaambia wamlipe mshahara? CCM haijaitaarifu ofisi ya bunge kuwa mpendazoe sio mwnachama wao tena sasa yeye ana kosa gani...wanachofanya bunge ni kufuata taratibu sio ukichwa maji wa akina makamba kutofuata taratibu na kudhani kuwa bunge litafanya kazi kwa mamabo ya kusikia magazetini...shame kwa makamba na ofisi yako kama mtendaji mkuu wa CCM
 
Bado hadi leo hii mpendazoe anakula pesa za ubunge huku ccm haijawasilisha barua bungeni kama si mwanachama wake. jee ccm haimtegi na baadae kutangaziwa kuwa fisadi kwa kulipwa pesa asizozitumikia?
Leta uthibitisho wa pesa zipi za BUNGE ambazo Mpendazoe anakula.
 
Back
Top Bottom