Ofisi ya Bunge: Mpendazoe bado ni mbunge wa Kishapu

Alipotangaza alikuwa amemaliza Ni mweshimiwa makamba tu kama kawaida yake inawezekana alikuwa hajasoma katiba ya CCM ili atoe taarifa bungeni.

bingo!!. .. badala ya watu kuelezea kwanini CCM haijatoa taarifa Bungeni kuwa imezidiwa kete na Mpendazoe.. watu wanataka Mpendazoe atafute, ameze.. na ashibe. Makamba na Kikwete kwanini hawajatoa taarifa Bungeni kuwa aliyekuwa mbunge wao amepoteza uanachama..? hili ndilo swali... wengine hawataki kuuliza swali sahihi na hivyo wanapata majibu yasiyo sahihi.
 
Huyu Mbunge inaonekana alitangaza kujiuzulu kwake kwa vyombo vya habari,
hajakiankikia barua chama chake na Ofisi ya Bunge ndio kwa maana Bunge bado
linamtambua kuwa ni Mbunge. Clever Guy!!!!!

Katiba ya CCM inasema mtu akijiunga na chama kingine anapoteza unachama. Mpendazoe kajiunga na chama kingine bado mnataka na aandike barua ya kuwaaga? Aweke na terehe?
 
Katiba ya CCM inasema mtu akijiunga na chama kingine anapoteza unachama. Mpendazoe kajiunga na chama kingine bado mnataka na aandike barua ya kuwaaga? Aweke na terehe?

Mkuu! nakusoma.........watu wako intoxicated, hawataki kufungua macho, wanasikia lakini wanagoma kuona!!.....kuona ni muhimu, huwezi kusikia alama za nyakati, unatakiwa kuziona. Nao wamegoma katu katu kuziona.
 
Kwa upande wake Katibu wa Kamati Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chilgati alisema suala hilo haliwahusu wao kwa kuwa, Mpendazoe aliwambia kwa heri na wao wakamwambia asante.

"Hilo ni suala lake binafsi na mamlaka ya bunge, sisi hatujamfukuza ila yeye ndiye alituaga na sisi tukamwambia asante, hatuna ugomvi na wewe," alisema Chiligati.

"Kama tungemfukuza uanachama sisi ndio tungelazimika kuiandikia ofisi ya bunge kuwa huyu si mwanachama wetu tena, lakini kwa vile yeye mwenyewe ndiye amehama chama, suala hilo ni la kwake na mamlaka ya bunge watajua namna ya kulimaliza," aliongeza Chiligati.

mtani wangu hapa kachemsha tu...
 
Mimi nawatakia kila la kheri wanaona Mpendazoe alivyofanya ni sahihi, lakini msimamo wangu ni kwamba alikurupuka kama alivyokurupuka Augustion Lyatonga Mrema.
Na historia hiyo haitafutika daima...

Hayuko makini period.
 
watu wengine wanaamini kabisa kua mwezi umetengenezwa kwa cheese na watabisha milele ukiwaambia kuwa ni miamba mitupu tu kule na hakuna uhai! Sasa kwa vile umeshaamua kuwa Mpendazoe ndio abebe lawama basi hata hutaki kuangalia katiba ya nchi, katiba ya CCM, na taratibu za CCM. Kwani Mrema alipojiuzulu aliandika barua kwa nani, lini?
 
Ni kuwa bunge linamtambua kwa sababu hajapeleka taarifa za kimaandishi, kwa hiyo hakuna jambo la ajabu hapo.

I am not a politician, but because JF is an open forum, let me give out my views on this motion (floated before us all). MPendazoe left his former party because he does not support the way the party and its government behave. He does not support the way the former party implements its election manifesto and the way the economy of the nation is handled. That was his priority one. He defects the government of the ruling party but not the Parliament. The question of his parliamentarianship is rather a consequence of the above priority as stated in the Union Constitution. He did not quarrel with the House of Representatives (Bunge?). He has no reason to hurry up submitting the resignation letter to the Bunge as if he hated ‘em! If the constitution could allow him to exercise representing his people, in a new party, we could be surprised to see him remain a faithful member of the Bunge. So MPendazoe has a big conundrum to resolve, thank God this is not ours. So let us, as educated ones, be CCM or CCJ & CHADEMA etc be slow to being offensive to Mr MPendazoe, because we may end up being regarded as fanatics of egoism which is a negative picture to us.
 
Unaongea vitu ambavyo ni rahisi sana mkuu sio kwamba hatuelewi vya katiba zote kama unavyodhani, and you are doing this not b'se hauna uwezo no... only because umefungwa kitambaa na huoni mkurupuko wa Mpendazoe shujaa wako.

Kuna wakati utaona kitambaa kikiondolewa kwa sasa it won't happen. I feel sorry for you...

Wakati ule Mrema akitoka CCM wengi tulijua kwamba alichemka process... kosa sio kutoka... na Mpendazoe hana kosa kutoka... but process ya kutoka... he got it wrong... na history itakuwa hivyo tu mkuu...

Pole sana... I know it hurt you... lakini ukweli ndio hivyo shujaa amechemsha... na angekuwa makini asingefanya hivyo... atachemka tu hata huko mbeleni....
 
Kasheshe.. unafikiri CCM wangetoa taarifa Bungeni kuwa Mpendazoe kajiunda na CCJ na hivyo amepoteza uanachama wake kwenye CCM kwa sababu alikuwa ni Mbunge kupitia chama chao?
 
Mzee Mwanakijiji,

Kuna njia mbili za kuisha kwa ubunge wa Mpendazoe:
1: Yeye mwenyewe kulijulisha bunge kwa maandishi kuhusu kujiuzulu kwake kwasababu amehama CCM
2. CCM kulijulisha bunge kwamba Mpendazoe sio mwanachama wao tena

Mpendazoe ndiye katangazia umma kuhama chama na kuachia ubunge; anashindwa nini kuliambia bunge? CCM hawajamfukuza, hivyo hawana haraka ya kujadili kuhusu kujiuzulu kwake.

Ni sawa na ndoa, wewe umeamua kumwacha bwana, badala ya kwenda kuomba talaka, unataka bwanako ndiye akaombe. Akiamua na yeye kukaa kimya, hiyo ndoa haijavunjwa.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kuna njia mbili za kuisha kwa ubunge wa Mpendazoe:

Hapana.. Ziko njia zaidi ya moja ya kupoteza ubunge wake katika mjadala huu amefanya hivyo kwa kupoteza uanachama wa chama chake cha siasa. Amepoteza uanachama wa CCM siyo alipotangaza hadharani bali pale alipoamua kujiunga na chama kingine. Ukiondoa njia hiyo nyingine ni kufukuzwa, kuvunja masharti ya katiba na hata kufa.

1: Yeye mwenyewe kulijulisha bunge kwa maandishi kuhusu kujiuzulu kwake kwasababu amehama CCM

Hakuna mahali popote kwenye Katiba panaposema Mbunge anapoteza Ubunge kwa kulijulisha Bunge!

2. CCM kulijulisha bunge kwamba Mpendazoe sio mwanachama wao tena

Hiyo ni kutoa taarifa tu; atakuwa ameshapoteza ubunge kwa kujiunga na chama kingine.

Mpendazoe ndiye katangazia umma kuhama chama na kuachia ubunge; anashindwa nini kuliambia bunge? CCM hawajamfukuza, hivyo hawana haraka ya kujadili kuhusu kujiuzulu kwake.

Kama Mpendazoe kashatangaza kuwa ameacha CCM na tayari amejiunga na chama kingine, kwanini awaandikie na barua ya kuwajulisha wakati jukumu hilo ni la chama kilichompoteza. Vinginevyo Mpendazoe hatowaambia na watamlipa kwa muda ule na anaweza akatokea siku moja moja Bungeni kukusanya posho.. CCM ndio wanatakiwa kutoa taarifa kwa Bunge kuwa Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wao kajiunga na chama kingine na hivyo siyo mwanachama wao tena.

Ni sawa na ndoa, wewe umeamua kumwacha bwana, badala ya kwenda kuomba talaka, unataka bwanako ndiye akaombe. Akiamua na yeye kukaa kimya, hiyo ndoa haijavunjwa.[/QUOTE]
 
Jibu: Hapana.

Mzee Mwanakijiji, post zako zote za katiba ziko right!!! Tatizo hapa ni umakini tu wa Shujaa Mpendazoe katika ku-execute hayo anayosema... ni vyema tuendelee kumshangilia ili aendelee kuona alichofanya ni sahihi... Lakini moyoni mwake anapata shida sana... angekuwa shujaa barua kwanza kwa Bunge then Shinyanga kwa Wapiga Kura wake... then habari maelezo.

Hata hivyo tunamtakia kila la kheri lakini lets wait and see, yuko wapi Mrema, yupo wapi Njelu Kasaka.

mpaka sasa watoto wachache wameshaona kwamba mfalme hajavaa nguo muda si muda mtoto atapiga makelele kwa umati unaomshangilia mfalme ambaye hajavaa nguo.
 
Kasheshe,

Mpendazoe mpaka sasa hajaenda Kishapu kwa waliompigia kura kuwa mbunge wao 2005; huyu kweli anajua umuhimu wa wapiga kura?

Nakubaliana na wewe, alitakiwa apeleke barua bungeni na wakati ule ule barua inafika basi angewajulisha wananchi wa Kishapu juu ya uamuzi wake. Lakini kwa Tanzania viongozi wetu huwa hawawajali waliowapa madaraka ndio maana hata ambaye anataka kuwa mkombozi wao bado anafanya makosa yale yale.
 
Hapana.. Ziko njia zaidi ya moja ya kupoteza ubunge wake katika mjadala huu amefanya hivyo kwa kupoteza uanachama wa chama chake cha siasa. Amepoteza uanachama wa CCM siyo alipotangaza hadharani bali pale alipoamua kujiunga na chama kingine. Ukiondoa njia hiyo nyingine ni kufukuzwa, kuvunja masharti ya katiba na hata kufa.

Hakuna mahali popote kwenye Katiba panaposema Mbunge anapoteza Ubunge kwa kulijulisha Bunge!

Hiyo ni kutoa taarifa tu; atakuwa ameshapoteza ubunge kwa kujiunga na chama kingine.

Kama Mpendazoe kashatangaza kuwa ameacha CCM na tayari amejiunga na chama kingine, kwanini awaandikie na barua ya kuwajulisha wakati jukumu hilo ni la chama kilichompoteza. Vinginevyo Mpendazoe hatowaambia na watamlipa kwa muda ule na anaweza akatokea siku moja moja Bungeni kukusanya posho.. CCM ndio wanatakiwa kutoa taarifa kwa Bunge kuwa Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wao kajiunga na chama kingine na hivyo siyo mwanachama wao tena.

Ni sawa na ndoa, wewe umeamua kumwacha bwana, badala ya kwenda kuomba talaka, unataka bwanako ndiye akaombe. Akiamua na yeye kukaa kimya, hiyo ndoa haijavunjwa.

Mzee Mwanakijiji,

Kwenye kila jambo ukishaanza kuingia kwenye technicalities utaishia kulalamika kila siku.

Mambo mengine sio magumu kiasi hicho; ni kutumia common sense tu na unapata jibu sahihi.

Hizo technicalities tuwaachie mahakimu na mawakili mahakamani maana ndio wanalipwa kwa hayo mambo.

Kama Mpendazoe kweli aliamua kuachana na CCM na kuachia ubunge; kwanini asubiri CCM ndio wapeleke barua bungeni?

Huko mbele sitshangaa CCM na upinzani wakisema huyo ni mtu wa CCM maana hata kadi hajarudisha. Yatarudia yale yale ya Mrema.
 
Nafikiri kama CCM hawana haja ya kufanya hivyo hata Mpendazoe hana haja ya kufanya hivyo.

Hivi ni nani anasimamia katiba ya chama cha mapinduzi? Au ndiyo yale yale chama hakina mwenyewe.

Huyu ndiye anapaswa kuangalia katiba ya chama inasemaje.

Mpendazoe ameonekana wazi wazi akipewa kadi ya CCJ hilo ni tosha kwa chama kuangalia katiba yake na kumuondoa ktk orodha ya wanachama hivyo kupoteza ubunge.
 
Mpendazoe: Mkombozi wa Wanyonge... Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote.
 
Kosa lake alikurupuka, angetafuta walau mwanasheria mmoja akamuuliza nini hatima ya kujitoa CCM na mustakbali wa ubunge wake, basi angengoja.

Milioni 45 si mchezo kuzikosa, na ubunge ndio keshaukosa maisha yake.
Uamuzi wake ni wa kishujaa kwa kuwa aliamua kukacha mahela yote hayo ili kupigania ustawi wa demokrasia.

Pesa siyo msingi wa maendeleo, sana sana fitna na uzandiki hujengwa na fedha
 
wabongo bwana.....mnapenda kweli thread za kujadili watu
Ndo manake best hapa si kwamba tunajadili watu tu bali kila kitu. Tunajadilili bila kificho. Kimsingi huwezi kuongelea maisha na maendeleo yoyote bila WATU. So dude unless it's a forum people must and should be discussed!
 
Msanii,

Tafuta njia nyingine ya kumsifia, sio hii mkuu; mshiko anakamata kama kawaida kwa utaratibu wa sasa. hivyo kama ulimpa ushujaa kwa kuwa ameacha mihela nakushauri ufikirie mara mbili.

Pension; ni malipo ya makato yako... huwa unapewa mpaka pale ulipofika mwisho wa kuchangia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom