Ofisi ya Bunge: Mpendazoe bado ni mbunge wa Kishapu

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Huyu ndiye mpiganaji wenu, hajui wapi pa kujiuzulu? tutaendelea kuona mengi... credibility ya Mpendazoe at test!!! Maskini naona kama anajutia maamuzi yake.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Na Salim Said

OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi, inamtambua aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kishapu kupitia Chama hicho hadi hapo itakapopata taarifa rasmi kutoka CCM.

Mpendazoe ni mmoja wa wabunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi ambao walipachikwa jina la makamanda wa ufisadi, kutokana na msimamo wao mkali dhidi ya wanaotuhumiwa kwa kutafuna fedha za umma au kutumia madaraka yao vibaya.

Mbunge huyo alitangaza kukukiacha chama chake na kijiunga kwenye Chama Cha Jamii (CCJ) Machi 30 mwaka huu na kusisitiza kuwa CCM sio mama yake, hivyo hatajilaumu kukihama, kwa sababu alikuwa anaishi kwa matumaini muda wote ndani ya chama hicho.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema,
"Ofisi ya bunge bado inamtambua Mpendazoe kuwa ni mbunge halali wa jimbo la Kishapu kwa sababu haijapata taarifa yoyote rasmi, kutoka kwake au chama chake cha awali."

"Kama Mpendazoe angekuja bungeni leo angekalia kiti chake kwa sababu hatuna taarifa yoyote ya maandishi ya kujiuzulu kwake," alisema Joel.

Joel alisema Ofisi ya Bunge inatakiwa kuwa na barua rasmi ya maandishi ya kuthibitisha kwamba Mpendazoe amejiuzulu nafasi ya ubunge au amekihama chake.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi taratibu na sababu za kuacha ubunge wa Bunge la Jamhuri.

"Sababu ya kwanza ni kwa mbunge mwenyewe kujinasua katika chama chake na kupata vithibitisho vyote, kuugua kwa muda mrefu na madaktari wakathibitisha kuwa hawezi tena kuwahudumia wananchi," alisema Joel.

"Mwisho ni kwa mwanachama kufanya vitendo vichafu na chama kikakunyang'anya uanachama," alisema Joel.

Alisema Ofisi yake haiwezi kukurupuka kwa vile kuna mivutano baina ya Mpendazoe na Chama chake, jambo linaloisababisha ofisi yake kusimamia taarifa rasmi itakayotumwa aidha kutoka chama chake cha awali au yeye mwenyewe binafsi.

Alisema kulingana na taratibu na sheria za bunge, Mpendazoe bado anatambuliwa na ofisi ya bunge kuwa ni mbunge wa Jimbo la Kishapu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Mpendazoe alisema,
"Mkurugenzi amejibu vizuri, ni kweli mimi bado ni mbunge, ila nilichofanya ni kutangaza kwa vyombo vya habari kujivua uanachama wa CCM."

"Ubunge wangu utakoma pale nitakapowasilisha taarifa ya maandishi kwa katibu wa bunge, nakusudia kufanya hivyo siku yoyote kuanzia sasa. Nina mambo yangu binafsi yakikamilika nitakwenda," alisema.
"Siku ile niliyokutana na waandishi Machi 30, sikupata muda wa kwenda ofisi za bunge kupeleka taarifa yoyote, lakini kikatiba natakiwa niwasilishe taarifa kwa katibu wa bunge," alisisitiza Mpendazoe.

"Nitakwenda kwa katibu wa bunge, lakini sikwambii lini hiyo ni taratibu zangu, mimi sio rais wala waziri mkuu. Lakini kikatiba na kisheria natakiwa niwasilishe taarifa ya maandishi katika ofisi ya bunge," aliongeza Mpendazoe.

Alipoulizwa iwapo ataingia bungeni katika mkutano huu wa 19, Mpendazoe alisema hayo ni mambo yake ya faragha (private).

“Unataka nikuambie naenda bungeni halafu kesho muandike Mpendazoe aingia bungeni, mbona mlikuwa hamuniulizi kabla sijahama CCM, mimi ni mtu mdogo bwana sipaswi kutangaza safari zangu,
" alisema Mpendazoe.

Alipoulizwa kwa sasa yuko katika mji gani wa Tanzani, Mpendazoe alikataa kuweka wazi na kujibu tu kwa ufupi.

"Nipo Tanzania, nipo Tanzania bara lakini kukusaidia zaidi ndugu mwandishi."

Kwa upande wake Katibu wa Kamati Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chilgati alisema suala hilo haliwahusu wao kwa kuwa, Mpendazoe aliwambia kwa heri na wao wakamwambia asante.

"Hilo ni suala lake binafsi na mamlaka ya bunge, sisi hatujamfukuza ila yeye ndiye alituaga na sisi tukamwambia asante, hatuna ugomvi na wewe," alisema Chiligati.

"Kama tungemfukuza uanachama sisi ndio tungelazimika kuiandikia ofisi ya bunge kuwa huyu si mwanachama wetu tena, lakini kwa vile yeye mwenyewe ndiye amehama chama, suala hilo ni la kwake na mamlaka ya bunge watajua namna ya kulimaliza,
" aliongeza Chiligati.
 
Patamu hapo.

Binafsi sioni tatizo lolote. Yeye atakapopata muda atawaandikia barua ili kuwapatia taarifa rasmi na kwa ajili ya kumbukumbu. Ningeshangaa kama angekuwa amekwenda kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendelea. Sina hakika suala la kulitaarifu bunge kwamba yeye si mbunge tena lina uharaka kiasi gani (level of urgency). Nadhani ni kukamilisha taratibu tu ila kimsingi yeye siyo mbunge tena!
 
Weweeee.... naomba nikupe mfano ukiajiriwa unapewa barua, ukijiuzulu unafanya nini? Lipi ambalo lingekuwa la urgency kwenda habari maelezo au kupeleka barua bungeni... alafu ipi ingekuwa uungwana kuwaaga wapiga kura, meaning kutangaza ukiwa jimboni au ukiwa mzizima...

I now understand the guy hana vision... we shall see...
I hate viongozi wasiokuwa makini ... this is... basi ...
 
''Huyu ndiye mpiganaji wenu, hajui wapi pa kujiuzulu? tutaendelea kuona mengi... credibility ya Mpendazoe at test!!! Maskini naona kama anajutia maamuzi yake''.

walengwa ni nani hapo kwenye red CCJ au JF members, halafu mi pia sioni tatizo kwani ni lazima upeleke barua siku hiyo hiyo, huo ni utaratibu tu atapeleka barua ya kujiuzuru siku yoyote akipata muda na si kuwa hajui wapi pa kujiuzuru
 
Weweeee.... naomba nikupe mfano ukiajiriwa unapewa barua, ukijiuzulu unafanya nini? Lipi ambalo lingekuwa la urgency kwenda habari maelezo au kupeleka barua bungeni... alafu ipi ingekuwa uungwana kuwaaga wapiga kura, meaning kutangaza ukiwa jimboni au ukiwa mzizima...

I now understand the guy hana vision... we shall see...
I hate viongozi wasiokuwa makini ... this is... basi ...
Mwanzo nilifikiri mwanasiasa mwenye papara ni Mrema peke yake, kumbe sivyo, avumaye baharini papa, kumbe wengine wapo!
 
Ni kuwa bunge linamtambua kwa sababu hajapeleka taarifa za kimaandishi, kwa hiyo hakuna jambo la ajabu hapo.
 
nadhani pale habari maelezo alitangaza nia ya kuhama CCM na kujiunga na CCJ, taratibi zingine zinafata
 
Weweeee.... naomba nikupe mfano ukiajiriwa unapewa barua, ukijiuzulu unafanya nini? Lipi ambalo lingekuwa la urgency kwenda habari maelezo au kupeleka barua bungeni... alafu ipi ingekuwa uungwana kuwaaga wapiga kura, meaning kutangaza ukiwa jimboni au ukiwa mzizima...

I now understand the guy hana vision... we shall see...
I hate viongozi wasiokuwa makini ... this is... basi ...

Ni kweli kwamba inaleta wasi wasi au kutia doa umakini wake katika kushughulikia mambo muhimu kama hili.

Ila katika mfano ulioutoa, siyo lazima kuandika barua mara moja ndo uonekane umeacha kazi. Hilo ni suala la uungwana na kufuata taratibu. Unaweza kuacha kazi kwa kutokuwepo mahali pako pa kazi kwa muda fulani ambao umewekwa na ofisi, mfano siku 7 mfululizo na mwajiri akachukulia kuwa umeacha kazi. Kwa hiyo suala la kuandika barua linaweza kufanyika wakati wowote (kwa maoni yangu).
 
mnaniangusha jamani!! CCM ndio walitakiwa watoe taarifa kwa Bunge!! Katiba ya CCM inasema hivi (msisitizo wangu):

13. (1) Uanachama wa mwanachama utakwisha
kwa:-
(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na Chama kingine chochote
cha siasa.

Badala ya kumuuliza Makamba kwanini hajatoa taarifa kwa Bunge.. mnashangaa kwanini Mpendazoe hajaandika kwa Spika. HAITAJI.
 
Likishindikana la MGOMBEA BINAFSI tuhangaike na hili la Mbunge aliyechaguliwa na watu wote bila kujali uanachama wao kunyang'anywa Ubunge kwa kuhamia chama kingine. Tuna mengi ya kufanya kwenye katiba zetu za vyama na hasa katiba ya JMT.
 
Ala kumbe siku hizi bado lazima barua upeleke mwenyewe? tuwe makini kidogo tuache kucheza sindima... kama alijua kwamba lazima ujiuzulu rasmi alienda maelezo kufanya nini?
 
CCM ilitakiwa kuandika barua kwa bunge kusema kuwa Mpendazowe sio mwanachama wake tena kwa hiyo afutwe ubunge au bunge lenyewe lilitakiwa kujua kuwa mpendazoe amehama chama kwa hiyo limfute?

maana hiyo sheria haisemi wazi nani anatakiwa kuandika barua ya kuonyesha uhamaji wake wa chama
 
Ala kumbe siku hizi bado lazima barua upeleke mwenyewe? tuwe makini kidogo tuache kucheza sindima... kama alijua kwamba lazima ujiuzulu rasmi alienda maelezo kufanya nini?

Sijui gumu ni lipi hapa. Huwezi kuwa mbunge hadi uwe umesimamishwa na chama cha siasa; ukijiunga na chama kingine cha siasa unapoteza ubunge wako (haijalishi kama umetoa taarifa mbinguni!); Mpendazoe alikuwa mbunge aliyesimamishwa na chama ha siasa - CCM.. akaamua kujiunga na CCJ hadharani na kwa kauli yake - hivyo amepoteza uanachama wake wa CCM.. lakini kuna genius wa bongo asiyejua katiba anayeng'ang'ania kuwa Mpendazoe ni Mbunge!! Na magenius wengine wanaonekana kukubali hivyo.. !!
 
Kosa lake alikurupuka, angetafuta walau mwanasheria mmoja akamuuliza nini hatima ya kujitoa CCM na mustakbali wa ubunge wake, basi angengoja.

Milioni 45 si mchezo kuzikosa, na ubunge ndio keshaukosa maisha yake.
 
a. huwezi kuwa mbunge hadi usimamishwe na chama cha siasa
b. kwa mujibu wa chama chako ukijiunga na chama kingine unapoteza unachama
c. Kwa vile umepoteza uanachama huwezi tena kuendelea kuwa mbunge!

Na hili mnahitaji mwanasheria kuwafafanulia? Ugumu hasa uko wapi?
 
Alipotangaza alikuwa amemaliza Ni mweshimiwa makamba tu kama kawaida yake inawezekana alikuwa hajasoma katiba ya CCM ili atoe taarifa bungeni.
 
Weweeee.... naomba nikupe mfano ukiajiriwa unapewa barua, ukijiuzulu unafanya nini? Lipi ambalo lingekuwa la urgency kwenda habari maelezo au kupeleka barua bungeni... alafu ipi ingekuwa uungwana kuwaaga wapiga kura, meaning kutangaza ukiwa jimboni au ukiwa mzizima...

I now understand the guy hana vision... we shall see...
I hate viongozi wasiokuwa makini ... this is... basi ...

We Kasheshe, alipokuwa kwenu alikuwa mzuri, akiondoka hana vision!!! LOW man, tena sana.
sina uanachama wa chama chochote, but i can feel you r too intoxicated to open your eyes! and they all r.
 
Kosa lake alikurupuka, angetafuta walau mwanasheria mmoja akamuuliza nini hatima ya kujitoa CCM na mustakbali wa ubunge wake, basi angengoja.

Milioni 45 si mchezo kuzikosa, na ubunge ndio keshaukosa maisha yake.

Mkuu,
masilahi ya taifa siyo milioni 45 tu, Mpendazoe bado ananguvu kabisa hata angepewa hizo pesa zingeisha tu .
 
Huyu Mbunge inaonekana alitangaza kujiuzulu kwake kwa vyombo vya habari,
hajakiankikia barua chama chake na Ofisi ya Bunge ndio kwa maana Bunge bado
linamtambua kuwa ni Mbunge. Clever Guy!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom