Ofisi hii Kila Ijumaa Wafanyakazi Wake Wanamwaga Radhi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani umezua jambo nchini Uingereza. Kampuni moja nchini humo ambayo baada ya kuona inapata hasara na inapoteza wafanyakazi wake wengi, iliamua kuwa kila siku ya ijumaa wafanyakazi wake wafanye kazi wakiwa uchi wa mnyama Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza, Baada ya kuona kazi haziendi vizuri katika kampuni hiyo, mmiliki wa kampuni hiyo Sam Jackson aliwashawishi wafanyakazi wake kuwa kila siku ya ijumaa wafanye kazi wakiwa uchi wa mnyama ili kuongeza morali wa kazi na kuwafanya wafanye kazi kwa uwazi zaidi. Kampuni hiyo inayojulikana kwa jina la Onebestway inashughulika na utengenezaji wa website, logo na matangazo ya kwenye luninga na ina makazi yake katika mji wa Newcastle. Wakati bosi wa kampuni hiyo alipotoa wazo hilo, wafanyakazi wake walipigwa na bumbuwazi lakini baadae walikubalina na bosi wao na kuamua kila ijumaa watakuwa wakifanya kazi wakiwa uchi. Mmiliki wa kampuni hiyo amedai kwamba kwa kutumia njia hii wafanyakazi wake wameweza kufanya kazi bila kuoneana aibu na uelewano kati ya wafanyakazi umeongezeka. Sam Jackson amedai kwamba hivi sasa shirika lake limeweza kujikwamua kwenye mtikisiko wa uchumi nchini Uingereza na wafanyakazi wake wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Habari za wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya kazi uchi kila siku ya ijumaa imevivutia vyombo vingi vya habari nchini Uingereza na kupelekea kutengenezwa kwa documentary kuhusiana na kampuni hiyo itakayorushwa kwenye televisheni ya Virgin 1 ya nchini humo julai 9 mwaka huu.

nifahamishe.com
 
Last edited by a moderator:
Du! Haya makubwa. Hakika duniani kuna mambo. Kumbe nguo tunazovaa ni kikwazo katika kufanya kazi kwa morale na uwazi zaidi! Ni elimu mpya.
 
mmmh,huyo bosi kweli ana akili sana!.....Ngoja ni kawashawishi mabosi wa Zain nao wafanye hivyo.Sipati picha nimuone nanhiii yupo uchi,teh teh teh,ila kwa bongo nadhani itafanya watu wasiende makazini kabisa, maana kuna watu unatakiwa uwaone wakiwa wamevaa nguo tu,maana unakuta mtu jimwili lake limevimbiana manyama hovyo.
 
Last edited:
Yaani hiyo style ikija hapa tutashuhudia vidudu vidogo kama vya watoto wachekechea.
Natasha nani kakuambia hivyo? ujui Bongo watu wamebarikiwa hivyo vifaa? utakimbia mwenyewe.Ukitaka kuona vidudu vidogo nenda India na China.Bongo ni balaa tupu usiombe.
 
rate ya kuzaliana bongo itaongezeka kwa 80% kwa muda wa miaka miwili tu ijayo. kama sasa tuko kati ya 42 hadi 46 em, ni wazi kabisa baada ya miaka miwili two tutakuwa kati ya watu 75.6 na 82.8m (em). umenihamu mkubwa eeh!
sasa nakupa blogwork, tafuta uwiano kati ya uzaliano huu na rasilimali tulizonazo halafu gawanya kwa wasomi tulionao ambao wataweza kuzi utilize hizo rasilimali.

wabongo kwakupenda nanilihiiiiiiiiiiii! ni noma.
 
Its a psychological approach of inviting more clients..... nadhani niliwahi kuhudhuria course flai ya mambo ya E-Marketing na mkufunzi alitoa hii hadithi wakati akielezea strategies mbalimbali za kuwavutia wateja kwako! Kama sikosei
 
mmmh,huyo bosi kweli ana akili sana!.....Ngoja ni kawashawishi mabosi wa Zain nao wafanye hivyo.Nipati picha nimuone nanhiii yupo ushi,teh teh teh,ila kwa bongo nadhani itafanya watu wasiende makazini kabisa, maana kuna watu unatakiwa uwaone wakiwa wamevaa nguo tu,maana unakuta mtu jimwili lake limevimbiana manyama hovyo.
teh teh ...kaka wazo zuri tena mi ntawai siku hiyo nakaa zangu pale reception najifanya nasoma magazeti nione watu wanavoingia uchi..jamaa yuko very innovative
 
kwa hivyo leo hii yote wako tupu tupu........weweweeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!
 
teh teh ...kaka wazo zuri tena mi ntawai siku hiyo nakaa zangu pale reception najifanya nasoma magazeti nione watu wanavoingia uchi..jamaa yuko very innovative

'yuk!'...uchafu tu!

...imagine wale vibonge wenye vitambi na manyama uzembe wakiwa uchi, na wale wenye malapa vifuani, au wenye cellulites na wenye michirizi chirizi utadhani michuruziko ya mchuzi...au wale nguo zinazowastiri 'mapori' ya nywele mwilini,... kuna mijitu inatisha ikiwa uchi, utasema masokwe!
 
Back
Top Bottom