Ofisa wa Serikali atishia kumloga mwandishi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]Monday, July 23, 2012[/h]Na Gustaphu Haule, Kisarawe



MWANDISHI wa habari wa kituo cha Televisheni ya Channel Ten, Marietha Nsembele juzi alitishiwa kulogwa yeye na familia yake na Ofisa Uhamiaji kutoka makao makuu, Eric Mwakiusa, baada ya kupiga picha nyumba ya ofisa huyo anayedaiwa kujiunganishia umeme kwa njia za panya.


Vitisho dhidi ya mwandishi huyo vilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati akiwa katika kampeni maaalum ya ukaguzi wa umeme iliyoanzishwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoani Pwani kwa lengo la kubaini watu wanaolihujumu.


Kutokana na kampeni hiyo, timu ya wataalamu kutoka mkoani wakiongozwa na Meneja wa Shirika Mkoa wa Pwani, Johnson Mwigune, walifika katika nyumba ya ofisa huyo na kugundua mita yake inatumika kinyume, hali ambayo inasababisha kuonyesha matumizi ya chini.


Mbali na kuchezea mita hiyo, ofisa huyo alikutwa na kosa la kuingiza umeme kwenye nyumba yake kwa njia za panya, ambayo amepangisha wapangaji kitendo ambacho kilisababisha awekwe kiti moto na watalaam wa TANESCO.


Wakati mahojiano yakiendelea, mwandishi alitumia nafasi yake kutimiza wajibu wa kupiga picha mbalimbali katika nyumba na kurekodi mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika, lakini jambo hilo lilisababisha ofisa kuja juu.


“Mwandishi picha ulizonipiga zinatosha, naomba usiendelee tena kwani kwa kufanya hivyo utanidhalilisha …maana mimi ni ofisa wa Serikali,…kosa la umeme mimi nimeliona nipo tayari kuwasikiliza wataalamu naomba uache kabisa mambo ya kupiga picha,” alisema ofisa huyo.


Wakati mwandishi huyo akiendelea kupiga picha hizo ndugu wa ofisa huyo, walianza kuja juu na kutaka kumshambulia mwandishi, huku wakisema wanachota mchanga wa nyayo zake ili wakamloge na ashindwe kutoa picha hizo katika luninga.


“Chota mchanga alipokanyanga huyu mwandishi, kwani hatuwezi kuacha shemeji yetu akadhalilishwa kiasi hiki… picha alizopiga zinatosha,” walisikika shemeji wa ofisa huyo wakisema.


Hatahivyo, pamoja na vurugu zilizokuwepo katika maeneo hayo Meneja wa TANESCO Mkoa wa Pwani, Johnson Mwigune, aliwaambia askari waliokuwepo katika eneo la tukio kumpeleka ofisa huyo kituoni, ili aweze kutaja watu waliomfanyia vitendo hivyo.

Chanzo: Mtanzania
 

Katika wa Nyerere hata wa Mwinyi hatukuwa na Viongozi wakiwa na Nguvu za kutishia kama kusema nitakuloga au

Kueneza UDINI ndani ya Jamii; Sasa Hivi UDINI ni nguzo hauwezi kupambana na viongozi wa kijamii waliotanguliza UDINI,

kila mtu anawaogopa na hata kuongea nao angalia Zanzibar eti UNAWALIPUA kwa MABOMU sio kutatua matatizo

Unawaongezea Umaarufu; Sasa hapa huyu sasa anasema atamloga Mwandishi... Inamaana waandishi wataanza

kukimbia kuandika masuala mabovu? kama UDINI?
 
Nitakuloga we nichezee@nngu007(utani). Duh! watu tutashindwa kufanya kazi sasa kwa kuogopa kulogwa.Hivyo vilikuwa ni vitisho ili kupooza tatizo.
 
Hata mimi leo nimetishiwa kulogwa nikampuuzia tu maana hawezi kuniloga!
Siabudu miungu wanaougua na kulazwa hospitali, wanazeeka, wanakufa.

Tujiwekeze imani kwa Mungu anayeishi milele, hii ndiyo kiboko ya wachawi!
 
Vitisho vya kawaida tu hivyo.................harogwi mtu km hana kosa
 
Serikali hii imejaa washirikina watupu, huoni jinsi wanavyovyaa mipete ya kishirikina wakiongozwa na mkulu, mchezee mkulu kama hujalogwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom