Ofisa Usalama wa Taifa atumbukia ufisadi BoT

Ninaamini hiyo report imepita mikononi mwa zaidi ya watu kumi. Wasipoitoa kuna siku tutaiona hapa JF.

JK inabidi awe mwangalifu sana, asije akawa kama Karamangi. Karamangi angetoa ile contract yake mapema wala yasingempata haya yanayompata sasa ya kwamba ni fisadi namba moja.

JK ikijaweza kuibua hiyo report na ikaonekana mbaya kuliko JK alivyotuambia, ajiandae 2010 kwa lolote.

Asante mkuu Halisi kwa hilo la Ngowi. Hakukuwa na hata mtu mmoja JF ambaye
alimwelezea huyu jamaa na kazi anazofanya kabla ya wewe leo kuandika majukumu yake.

Mimi kwa kufuata hizo habari nilihisi Ngowi ndiye anasemwa lakini sikuwa na uhakika kama kweli ndiye pia kigogo wa usalama wa taifa. Hapa umesaidia kutupatia the last piece in the jigsaw.
 
Kwa kiasi fulani naanza kupata mwangaza jinsi Thom Apson alivyopata hizo tenda za Ikulu na Benki kuu Zanzibar.

Mafuchila,

Kumbe na wewe ulikuwa gizani kama mimi? Yaani sasa picha imefunguka kweli kweli. Wakuu wamesaidia kutegua mtego uliokuwepo, sasa ni kukaa chini na kuongeza popcorns zetu kusubiri hili lipicha mwisho wake utakuwaje.
 
Wabongo hatuwezi kulala. Ina maana hawa jamaa kwa nguvu na network waliyonayo, kama sheria ikichukua mkondo wake wana uwezo mkubwa wa kutuingiza kule ambapo jirani zetu wanajuta kuwepo.

Mafuchila hatulali. Ndio kwanza kumekucha ILA INAUMA. Nawatakia kila la kheir JF, kama NIKIWA HAI (maana INATISHA), tutaendelea kuchangia baadaye.
 
Mafuchila hatulali. Ndio kwanza kumekucha ILA INAUMA. Nawatakia kila la kheir JF, kama NIKIWA HAI (maana INATISHA), tutaendelea kuchangia baadaye.

Mzee tunakuombea uzima ili uweze kutufukulia zaidi huu uozo
 
Mtanzana yule kijana alipewa ulaji ule na JK baada ya Mama yake kumpa Tom siri moja ambayo Baba yake alishiriki kucheza na kurudi usiku home late na ilikuwa mipango ya kumpiga chini JK kutokugombea kabla ya majina kule Dodoma kufika . Ndipo Tom alikuwa mpenzi wa JK akamtafuta na ku spill the beans JK akaona Mwanga ndiyo maana yuko naye . Sasa sijui kama ilikuwa ni strategy ama vipi lakini Mzee alizoza home late night ndip Tom akaipata .

Apson kafanya mengi na JK na Elisifa akiwa shemeji yake Mkapa basi lazima tukazane . Lile jumba la Tom pale kwake lilikuwa linalindwa na Jeshi na wala si FFU nikawa nashangaa why mtoto alindwe na Jeshi .Yaani kumbani kwa Tom si kwa Apson.Toma ana makashfa kibao lakini hakuguswa na hajaguswa .
 
Kulingana na habari hapo juu, jina linalotokea kwenye kampuni hizo zote mbili ni la Elisifa Ngowi, je huyu ni usalama wa taifa?ali siwa

watu humu ni wakali...si ajabu kila mara jk anahamaki kuwa mitandao ni UVUMI..ukweli wa mambo ni kuwa humu watu wanasema ukweli ndio maana anahamaki!!!.....ukirusha jiwe gizani atakayelia limempata!!!!
 
Heri yenu... lakini mwenzenu bado niko Gizani kwenye Kagoda Agric...

At least hayo mawili Excel.. Service etc.. nimeona Mwanga!!!
 
Sasa, Balali alipoenda kwa Bi. Meghji na kumuambia malipo ya Kagoda ni kwa ajili ya "Usalama wa Taifa" inawezekana alikuwa anasema kweli?

Kwa maneno mengine, inawezekana walichelewa kumtaarifu Bi. Meghji kuhusu mambo hayo na hivyo hakuwemo kwenye loop.

Ndio maana wanasema hakuna perfect crime, mara nyingi unaweza kujikuta unafanya kosa la kizembe na siri inafichuka.
 
watu humu ni wakali...si ajabu kila mara jk anahamaki kuwa mitandao ni UVUMI..ukweli wa mambo ni kuwa humu watu wanasema ukweli ndio maana anahamaki!!!.....ukirusha jiwe gizani atakayelia limempata!!!!

Huo usemi kiboko Mkuu, na kweli jamaa jiwe limempata. Atupe ukweli wa fununu hizi, ama svyo tutaendelea kuamini daima kwamba hizi tetesi ni za kweli
 
Sasa, Balali alipoenda kwa Bi. Meghji na kumuambia malipo ya Kagoda ni kwa ajili ya "Usalama wa Taifa" inawezekana alikuwa anasema kweli?

Kwa maneno mengine, inawezekana walichelewa kumtaarifu Bi. Meghji kuhusu mambo hayo na hivyo hakuwemo kwenye loop.

Ndio maana wanasema hakuna perfect crime, mara nyingi unaweza kujikuta unafanya kosa la kizembe na siri inafichuka.

Hili ndilo swali ambalo wengi hapa wanajiuliza sasa. Kwa muda sasa baadhi yetu tuliweka cover hapa JF ili hii story ya wana usalama kuhusika na wizi wa BoT irushwe kwenye vyombo vya habari nyumbani na finally the music is getting out!

Nimechukua popcorn zangu tayari kabisa kushuhudia part two ya hii movie.
 
Hii sio hoja tena ya wapinzani sasa wamegeuka watetezi wa mafisadi
 
Back
Top Bottom