Ofisa Mipango Chamwino ajiua.... baada ya kumshika mke na lijamaa

Ngabu,u cant be serious,women?"they are warry transgrassors"thats why they look so inocent

Women are so innocent, so pristine, and so wholesome to even think of cheating on their men. I refuse to accept that proposition.
 
ebwana huyu bwana tunaishi nae jilan hapa kitaani, magorofa mengi kikuyu! Huyo mwanamke huyu ni mume wake wa 3 kati ya wa4 kufariki tena kwa kupigwa au kujipiga risasi. Mmoja aliyenusurika mpaka sasa ni chizi, mwili wa jamaa keshasafirishwa kwenda tabora kwa mazishi. Mungu ampumzishe mahala pema!

............aiseee!! Kama ni kweli inawezekana huyo mama ana nguvu flani za giza, hii ni kiimani zaidi maana haingii akilini waume wote kuishia na risasi.
 
we we weeee,ishia hapo hapo,ndo unavyojidanganya hivyo,mimi tu hapa mke wa mtu kaniganda mbaya,huwa nachakachua kiaina,sasa hawachiti vp?au waolewe kabisa mara mbili?

Kaa mkao wa kujutia
 
Kwa kweli ni tukio la kushangaza sana, hata huyo aliekuwa chizi wanadai ni baada ya risasi kumparaza! Hapa Dodoma hizi ndio habari yilizoteka mji! Kijana alikuwa mtu wa watu sana!
 
Kaombwe miaka 28 .Vicky miaka 34????? ... Huyu kaombwe alikuwa bado ana mambo ya kitoto maana hata umri wake unaonyesha....we wife anapiga kazi za nje na wewe unajipindua kama huna akili nzuri....mamabo ya kujiuwa ya kijinga sana hayo...
 
OFISA Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Fred Kaombwe (28), amejiua kwa kijipiga risasi kichwani baada ya kumkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine katika baa mojawapo mjini Dodoma.

Baada ya hapo, Kaombwe inadaiwa alimkimbiza mkewe huyo Vicky Kaombwe (34) na baadaye alimpiga risasi na kumjeruhi sehemu za mbavu.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Elizabeth Masiaga alisema ,Kaombwe alijipiga risasi juzi saa 3.00 usiku katika mtaa wa Madole eneo la Kigamboni mjini Dodoma.

Kamanda Masiaga alisema, Kaombwe alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kupatiwa matibabu wakati mkewe Vicky amelazwa katika hospitali hiyo.

Hata hivyo, hali ya majeruhi huyo anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana mjini Dodoma bado si nzuri na Kamanda Masiaga aliahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Akizungumza na gazeti hili, mkwe wa marehemu, Thadei Nghwaya, alidai kulikuwa na ugomvi wa kifamilia na kwamba, Kaombwe alijipiga risasi kifuani na si kichwani baada ya kuhisi kuwa amemuua mkewe.

Nghwaya alisema, baada ya vipimo, ilibainika na wataalamu kuwa risasi aliyojipiga Kaombwe ilipitiliza na haikubaki mwilini.

Akizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina, mmoja wa mashuhuda alidai kuwa, kabla ya mauaji hayo Kaombwe alimkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine katika baa.

Alidai kuwa, baada ya hapo, Vicky alikimbilia katika gari lake na kuondoka nalo huku akifukuzwa na mumewe katika gari lingine hadi walipofika nyumbani kwao eneo la Kigamboni.

Shuhuda huyo alidai kuwa, Vicky aliposhuka katika gari kwa lengo la kufungua geti, Kaombwe alikuwa ameshafika akatoka ndani ya gari lake na kumpiga risasi mkewe.

Kaombwe alisafirishwa jana kwenda Tabora kwa maziko.

source: habari leo

MAONI; sasa hapa kuna nafuu gani?
anyway wamama na wadada jamani kuna wanaume ni dhaifu sio vizuri kuchakachua
mali zao, wanaume kujiua kwa ajili ya penzi, inaingia akili kweli
Neno la Mungu linasema kuwa mpende Bwana Mungu wako kwa nguvu zako zote, akili zako zote na uwezo wako wote na umpende jilani yako kama unavyo jipenda. Kwa mawaidha hayo nasema kuwa watu wanahitaji darasa au counseling, maana kama unampenda Muumba wako utamuogopa saana na kama unajipenda huwezi kujiuwa kwa ajili ya jilani. Kwa sababu mke si Nduguyo wala hukuzaliwa naye.Lakini neno la Mungu linasema ''Matthew : 19: 9 Kama mwanamke ametenda kosa kubwa la uzinzi unayo haki kumuacha na kumpatia talaka.Hapo mtu hafungwi kuoa au kuolewa tena. Kwa hiyo katika kumpenda mkeo hata kama mna watoto uwe na kiasi kukosa kiasi ni ujinga. Mungu amekupa akili na utashi ndio maana wewe ni mtu si mnyama. Kwa mwanamke vivyo hivyo uwe na kiasa Umpende saana Mungu wako, usitoe moyo wako wote kwa jilani yako, uwe na hekima na maarifa.Fikiria sasa maisha ya hiyo familia????????? Watu tuwe waaminifu kwenye ndoa zetu, madhara ya kukosa uaminifu ni makubwa saana kwa familia zetu!!!!!!!
 
Sasa ndio itakula wazi wazi kama kweli ilikuwa inampenda, nilishawahi kushuhudia kama hii jamaa lijinyonga kisa mke analiwa nje,
ndugu zake walikuwa wakali kwa mama hasipewe urithi lakini mama alikuwa jasiri hakawaburuza mahakamani na kushinda kesi
kwa kukosa ustaarabu yule mtuhumiwa alianza kwenda kuchakachulia hapo hapo kwa marehemu


Hii habari ya kufumania isikie tu kwa watu,
usilogwe ikakukuta,
mara nyingi maamuzi yake huwa ni magumu sana!!!!
 
we we weeee,ishia hapo hapo,ndo unavyojidanganya hivyo,mimi tu hapa mke wa mtu kaniganda mbaya,huwa nachakachua kiaina,sasa hawachiti vp?au waolewe kabisa mara mbili?
Acha hiyo tabia utakufa, fikiria maisha yako ndugu yangu bado una future yako, achana na mijimama. Panga maisha yako ya baadae, pata mke mwema uoe, jifunze neno la Mungu mtangulize Mungu kabla ya chochote katika maisha yako!!!!!!!!!!
 
ebwana huyu bwana tunaishi nae jilan hapa kitaani, magorofa mengi kikuyu! Huyo mwanamke huyu ni mume wake wa 3 kati ya wa4 kufariki tena kwa kupigwa au kujipiga risasi. Mmoja aliyenusurika mpaka sasa ni chizi, mwili wa jamaa keshasafirishwa kwenda tabora kwa mazishi. Mungu ampumzishe mahala pema!

mh!!! anakitu gani huyu mwanamke? mh iko namna si bure
 
Hii haiwezekani bana! Toka lini wanawake wameanza kuchiti? Wanawake huwaga hawachiti bana. Huyo jamaa maisha tu yamemshinda na akaamua kujiua sasa wanamsingizia infii mkewe.

Mi bado nakataa bana. Wanawake huwaga hawachiti.

Wanawake hawachiti bana. Huo ndo ukweli wenyewe. Jamaa alikuwa na wasiwasi wa bure tu.

Sijawahi kabisa mimi kuona mwanamke anayechiti. Hata hapa uliza hawa akina dada waliopo hapa JF watakwambia.

Women are so innocent, so pristine, and so wholesome to even think of cheating on their men. I refuse to accept that proposition.
Wanawake huwa hawachitiki kabisa wanasingiziwa, they are so innocent like angles in the heaven.
 
wivi ni compulsory content ya mapenzi ila ukizidi ni hatari
siongezi neno kwenye hii sredi
 
Kaombwe miaka 28 .Vicky miaka 34????? ... Huyu kaombwe alikuwa bado ana mambo ya kitoto maana hata umri wake unaonyesha....we wife anapiga kazi za nje na wewe unajipindua kama huna akili nzuri....mamabo ya kujiuwa ya kijinga sana hayo...

hapa hapasemwi ukweli watu watakuona mkosaji
zuga unampa pole marehemu ili usisemwe vibaya
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom