Önly fans of Hiphop

Mfuatilieni mtu anaitwa chief ramso ambaye kwa sasa anajiita zavara ndo mtajua nani anastahiki kuitwa mc wa bongo,nash emcee anaonekana anaijua hip hop kwa kuwa anapita anapopita zavarra na hata ukisikia nash anavyochana na mitambao utaona kuna mfanano kati yake na zavvara

Ramadhani Mponjika aka Cheef Rhymson aka Zavala uyu ni mwalimu wa Hiphop kwa Tanzania..jamaa anaijua Hiphop na anaiishi bila kujistukia,unajua kuishi Hiphop usifanye nako mchezo..ukimwona na midevu yake na pamba zake unaweza mchukulia poa ila usimpimie ata kidogo jamaa ni wa ukweli haswa,ameishi State na Ukerewe(UK) maisha tofauti tofauti tena sio ya kuungaunga...nilishawai mtembelea home kwake kabisa uko Iringa ana bangaloo lake maeneo ya Gangilonga kuna hadi studio umo ndani na mkewe ni Injinia wa kimataifa ni mjamaika...ana swaga zake flani za kutumia maneno ya kiingereza yasiyo na tafsiri rasmi ya kiswahili ila yeye anayatafutia tafsiri ya kiswahili mfano Mixtape=kandamseto,punchlines=mistarikonde,link=kiunga,rapper=mchanaji nk nk nk...jamaa ni Godfather wa Fid Q,Sterio,One,Philly Techniques,Songa,Niki mbishi,Maalim Nash,Para The Mc na wengi tu..

Back to the topic MC Wa kweli kwa sasa Bongo ni Mr II Sugu.
 
kwa waliopo kwenye game now anaefaa kuitwa MC ni FID Q peke yake ila tukiongeza na wasiokuepo ndo wenge sana..

Wabongo ni wavivu wa kusoma ndio maana tunawaona watu kama Fid Q na Mrisho mpoto ni watu wakali sana katika aina ya miziki wanayoimba.

Mfano kama Mpoto, kwa mtu anayefahamu haswa nahau, tenzi, misemo ya Kiswahili na vurumai kama hizo hawezi kumsifia eti anajuwa Muziki.
Kazi anayofanya Mpoto ni kupitia vitabu vyenye mafumbo, methali, nahau na misemo ya Kiswahili kisha anachomeka chomeka kwenye mashairi yake machache then anatoa Single na wabongo tulivyo wavivu wa kujisomea basi tunampigia makofi tukiamini ameumiza kichwa ile mbaya.
Kumbe maneno yoote anayotumia yalishatungwa na akina Andanenda enzi hizo.

So ni the same na Fid Q, huyu jamaa anapenda sana kutumie misemo na Methali za kiswahili ambazo wenzake walishaumiza kichwa na kuzifanyia kazi, then yeye anakuja kupita mulemule.

Wasanii wengi wa Bongo fleva walikuwa wanaiba Mashairi katika kipindi kilichokuwa kinarushwa hewani Redio Tanzania Dar es Salam, kipindi cha Malenga wetu.

nahisi kile kipindi kwa sasa hakipo tena kutokana na mijitu kufaidika na mpangilio wa mashairi ya wenzao ile hali wenyewe wanachoweza ni kukimbizana kwa waganga kila kukicha na kutumia pesa pasipo kukumbuka kuwekeza
 
Nilishawahai muuliza ili swali Geronimo Prat (If I spelled the name right), pale UAACC akabaki hana jibu ila alinipa majina niyape namba mwenyewe

1. Faza Nelly R.I.P
2. Sugu
3. J.C.B Jacob Makala
4. Jay Moe
5. EMP2 Boyoloco

Hao wapange uonavyo. Hao ndio MCs wa sasa. Japo Faza Nelly hatunae lakini daily lazima umsikie, either Rappers wamkumbuke, au uisikie "Nini Haramu" On Air
 
- Ukishakuwa maarufu lazima ukubali skendo...
- sio kila siku watasifu lazima watapiga dongo...
- Kuna Wengine hawapitishi hata wiki wamefanya jambo...
- Na wengine wakiona hawaskiki watajifanya wana skendo...
- Jay Moe ni yuleyule umaarufu haujanibadilisha...
Kipara hakuna nywele style ya kiduku itapita...

Am so Famous...
 
Ramadhani Mponjika aka Cheef Rhymson aka Zavala uyu ni mwalimu wa Hiphop kwa Tanzania..jamaa anaijua Hiphop na anaiishi bila kujistukia,unajua kuishi Hiphop usifanye nako mchezo..ukimwona na midevu yake na pamba zake unaweza mchukulia poa ila usimpimie ata kidogo jamaa ni wa ukweli haswa,ameishi State na Ukerewe(UK) maisha tofauti tofauti tena sio ya kuungaunga...nilishawai mtembelea home kwake kabisa uko Iringa ana bangaloo lake maeneo ya Gangilonga kuna hadi studio umo ndani na mkewe ni Injinia wa kimataifa ni mjamaika...ana swaga zake flani za kutumia maneno ya kiingereza yasiyo na tafsiri rasmi ya kiswahili ila yeye anayatafutia tafsiri ya kiswahili mfano Mixtape=kandamseto,punchlines=mistarikonde,link=kiunga,rapper=mchanaji nk nk nk...jamaa ni Godfather wa Fid Q,Sterio,One,Philly Techniques,Songa,Niki mbishi,Maalim Nash,Para The Mc na wengi tu..

Back to the topic MC Wa kweli kwa sasa Bongo ni Mr II Sugu.

daah kweli kaka umenipa shule tosha watu kama hiye ndo mfano wa kuigwa sio mtoto mitozi ya siku hizi eti mi Mc i hate dat!
 
Nilishawahai muuliza ili swali Geronimo Prat (If I spelled the name right), pale UAACC akabaki hana jibu ila alinipa majina niyape namba mwenyewe

1. Faza Nelly R.I.P
2. Sugu
3. J.C.B Jacob Makala
4. Jay Moe
5. EMP2 Boyoloco

Hao wapange uonavyo. Hao ndio MCs wa sasa. Japo Faza Nelly hatunae lakini daily lazima umsikie, either Rappers wamkumbuke, au uisikie "Nini Haramu" On Air

Huwezi mtaja Faza Nelly kama real Mc, pasipo kuwataja K-Single, Faza Nelly anaanza game K-Single, D-Rob, Adili(Nigga One), tayari walikua wana run game hii kwa bongo.
Bamiza inamtoa Faza Nelly 99 lakini Kwanza Unit walikua tayari wanafanya game, na nina uhakika hata Faza Nelly wali muinsnpire!
JCB bado hajafiki level hiyo ya real MCs
Jay Moe wakawaidaa sana
Pia hahis haujaelewa maana ya MCs, sio kuaaandika mashairi tu zingatia nguzo 5 za hip hip
Maana kama MCs ni kuandika mashairi hata FA atakuwemo!
Na MCs sio kukaza sauti kama JCB maana hata Chindo Man, Kala Pina na Msema Kweli watakuwemo!
Kifupi MCs wa ukweli Bongo
1.Sugu - bado yupo
2.Faza Nelly - R.I.P
3.Adili(Nigga One) - R.I.P
4.Kibacha(K Single) - bado yupo
5.Hashim Dogo -bado yupo
6.D-Rob - R.I.P
7.Chief Ramso - bado yupo
 
nini maana halisi ya MC..
wana hip hop?

Mbona JOH MAKINI..hamjamtaja hapa.
Jembe langu hlo.
 
nini maana halisi ya MC..
wana hip hop?

Mbona JOH MAKINI..hamjamtaja hapa.
Jembe langu hlo.

hahahahaha hamna kitu pumba tupu soft sana siku hz huyu kaka ndo maana wana mponda sana kina Nikk Mbishi
 
Kwa sasa kwa upande wangu, vijana walio katika Tamadun Muzik akina Nash Mc na P the Mc bila kuwasahau One the Incredible na Niki Mbishi pamoja na Stereo.
 
Tukiongelea Hiphop kama vilivyo vitu vingine, nayo imeshindwa kuhimili upepo wa mabadiliko nayo pia, imemegwa na baadhi ya ladha zake zimekua diluted kiasi sisi tuliokuwa tunapenda Hihop za way back, tumeshindwa ni wapi pa kushika hivi sasa, nkiimaanisha ni nani wa kizazi hiki anaweza kuvishwa crown, Ila kwa sasa Kibongobomgo FId Q
 
Kama tukiwa makini, Hashim Dogo me nadhani anastahili kua m1 ya real mc hapa bongo nje ya Zavara, K-single, D rob, na Faza nelly.
Kwasababu ukimsikia Fid, Nikki Mbishi, Sterio, Songa, P The Mc na Maalim Nash wote ni Copy ya Hashim Dogo.
Pia wengine wanacopy hata style za state mfano Nikki Mbishi haswa alipokua anaanza game nyimbo kama Punch Line kuna sehemu anasound kama Common.

FID Q anacopy sana baadhi ya punch line zake state mfano kwenye nyimbo yake ya Professional kuna punch anasema " Natokea mwanza home of greatest rapper mtoto wa dandu comes first then i am a professional" alichukua kwa Lil Kim kwenye nyimbo ya Lighters up Kim alisema "Am from brooklyn home of greatest rappers BIG comes first and Kim comes after" pia kama una album ya Enter the Wutang ya mwaka '93 ya Wu tang clan kuna punch line nyingi Fid anazitumia hata jina la One man army au jeshi la mtu mmoja alikua analitumia Ol' diry bastard kwenye nyimbo ya "Shame on you" kifupi wasanii wengi wa sasa ni wezi wa mistari konde.
 
Mc wa ukweli ni CHINDO MAN mbwa mzee a.k.a Jombii
tafuteni nyimbo za huyu generali wa WATENGWA FAMILY.He is an awesome mc,from arusha the high court of Hip Hop
 
Mc wa ukweli ni CHINDO MAN mbwa mzee a.k.a Jombii
tafuteni nyimbo za huyu generali wa WATENGWA FAMILY.He is an awesome mc,from arusha the high court of Hip Hop
 
Back
Top Bottom