OCD, Zuberi Mwombeji afunguliwa jalada kwa kuwaita panya wana A TOWN

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.“Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote,” alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya. Akizungumzia madai hayo jana kwa njia ya simu, OCD Mwombeji alikana kutoa kauli hiyo na kusema hizo ni propaganda zinazoenezwa kuhalalisha uhalifu au kutafuta huruma ya umma kwa makosa yaliyotendeka. “Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri,” alisema OCD Mwombeji.

chanzo: mwananchi
 
"Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri," alisema OCD Mwombeji.

Huu utetezi wa malezi mema kutoka kwa familia naona sasa umekuwa wimbo wa kawaida wa wakurupukaji serikalini na kwingineko.
 
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita."Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote," alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya. Akizungumzia madai hayo jana kwa njia ya simu, OCD Mwombeji alikana kutoa kauli hiyo na kusema hizo ni propaganda zinazoenezwa kuhalalisha uhalifu au kutafuta huruma ya umma kwa makosa yaliyotendeka. "Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri," alisema OCD Mwombeji.

chanzo: mwananchi
polisi wanamchunguza polisi mwenzao hapo kuna haki itatendeka kweli kwanini wasitafute independent entity kuchunguza issue nzima. we need an independent eye to look into it and not someone who has a dog in the fight.
 
Panya niyeye na mabwana zake wanao mtumia kuwachanganya watu. Nyambaf nguvu ya umma itawaangusha tu
 
Filing a case is one thing but observation of justice is another important yet difficult thing to happen given bad record of our legal authorities. They probably have to launch an independent committee to investigate into the allegations but not relying on same corrupt organs to expect fairness and justice.
 
Mapanya ni wale wahuni. Lugha.Jf hapa kuna matusi yakutisha, mbona hakuna kesi.
 
Mapanya ni wale wahuni. Lugha.Jf hapa kuna matusi yakutisha, mbona hakuna kesi.
Hiyo lugha unayotumia ndiyo Zuberi aliitumia na wewe kesho ikiambiwa umewaita binadamu panya utakataa kama anavyokataa OCD, anajifanya eti amelelewa vizuri familia gani inafundisha kuwaita binadamu wenzake panya kumbe hata tanzania tuna kina Gaddafi shame on him ngoja nitafute wanasheria niinunue hiyo kesi.
 
Ufunguaji wa jadala kumchunguza mkuu wa kituo cha polisi Arusha ni kutokana na tishio la wananchi wa Arusha kuweka mgomo wa vyombo vya usafiri, na kama hatua hazichukuliwi maana yake kizaazaa kikubwa kitafumuka, hii ni ishara wazi ya nguvu ya umma isivyoshindikana.
 
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji.

Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.“Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote,” alisema Kamanda Mpwapwa.....................................

chanzo: mwananchi

Walifikishwaje mahakamani kama uchunguzi ulikuwa haujafanyika sawa sawa na kupata ushahidi ili haki itendeke? Je, ina maana watafuta mashitaka yaliyoko mahakamani sasa? Na kama mahakama itandelea na kesi, polisi watatoa ushahidi upi ikiwa uchunguzi ndiyo kwanza unafanyika?

Na je, kama uchunguzi ukifanyika na kukosa ushahidi dhidi ya hiyo kesi ambayo tayari iko mahakamani, je POLISI watachukua hatua gani dhidi ya POLISI ambao wamefungua kesi ya uongo, ya kubambikiza?

Hili sakata la Lema na Mwombeji aidha litampa Mwombeji u-RPC mahali fulani au litamrudisha kijijini kama Zombe. Time will tell.

Simfahamu vizuri sana RPC Mpwapwa, ila wanaomfahamu vizuri wanasema ni mtu makini na anaijua kazi yake, japo wakati mwingine anayumba kidogo kuchukua hatua.
 
Ufunguaji wa jadala kumchunguza mkuu wa kituo cha polisi Arusha ni kutokana na tishio la wananchi wa Arusha kuweka mgomo wa vyombo vya usafiri, na kama hatua hazichukuliwi maana yake kizaazaa kikubwa kitafumuka, hii ni ishara wazi ya nguvu ya umma isivyoshindikana.

Arusha inaweza kuanzisha kama Bengazi kisha wengine wanaitikia hadi ukweli uenee nchi nzima.
 
asimsingizie mama.... Kwani mama ndie aliemfundisha ukatili na dharau?
 
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.“Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote,” alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya. Akizungumzia madai hayo jana kwa njia ya simu, OCD Mwombeji alikana kutoa kauli hiyo na kusema hizo ni propaganda zinazoenezwa kuhalalisha uhalifu au kutafuta huruma ya umma kwa makosa yaliyotendeka. “Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri,” alisema OCD Mwombeji.

chanzo: mwananchi

Mimi ningependa kutoa maoni yangu kama ifuatavyo,huyu OCD aliyewaita wananchi panya ni kuwa tayari ameshatuhumiwa kama alivyotuhumiwa Lema,hivyo basi kua huyu ni boss wa polisi ili aachie uchunguzi ulio huru anatakiwa ajiuzulu apishe nafasi ya uchunguzi huru,akishajiuzulu akamatwe awekwe ndani apelekwe mahakamani na apewe nafasi ya kupata dhamana vilele kama alivyopewa lema manake ni haki yake ya kimsingi na kesi iendelee mpaka hukumu itakapotoka.
Zaidi ya hapo kama ataendelea kuwa madarakani uwezekano mkubwa wa kuvuruga ushaidi upo.
Inatakiwa ieleweke kwamba raia yoyote akitenda kosa lazima sheria ichukue mkondo wake hata akiwa hakimu.
 
Inauwaje mtu anafunguliwa jalada wakati akiendelea kushika wadhifa ambao kwa namna moja ana nyingine utazuia uchunguzi huru?. Ilitakiwa ajizulu kwanza wadhifa huo ili kupisha uchunguzi huru. Anything short of that is tactic to calm the public anger on one man who thinks his authority can be used to punish those who are opposing him. He abuses the power.

Historia inaonesha kuwa chunguzi kama hizi huwa hazina effect kwa mchunguzwaji. Hapo ni IGP kuangalia chini na kumuhamisha kituo cha kazi huyu mbabe ambaye uwepo wake Arusha una negative effect kwenye mahusiano kati ya polisi na wananchi. Polisi wanatakiwa kuwa rafiki wa raia wema na si adui. Maamuzi hayo yatakuwa ni ya busara zaidi kuliko polisi kuanzisha uchunguza wa kisanii kama huu.
 
Mimi ningependa kutoa maoni yangu kama ifuatavyo,huyu OCD aliyewaita wananchi panya ni kuwa tayari ameshatuhumiwa kama alivyotuhumiwa Lema,hivyo basi kua huyu ni boss wa polisi ili aachie uchunguzi ulio huru anatakiwa ajiuzulu apishe nafasi ya uchunguzi huru,akishajiuzulu akamatwe awekwe ndani apelekwe mahakamani na apewe nafasi ya kupata dhamana vilele kama alivyopewa lema manake ni haki yake ya kimsingi na kesi iendelee mpaka hukumu itakapotoka.
Zaidi ya hapo kama ataendelea kuwa madarakani uwezekano mkubwa wa kuvuruga ushaidi upo.
Inatakiwa ieleweke kwamba raia yoyote akitenda kosa lazima sheria ichukue mkondo wake hata akiwa hakimu.

mtaongea sana zaidi ya kasuku! Mbona akina Lowassa, Chenge na wengineo wengi waliochota mabilion na kuhifikisha nchi hapa ilipo kwa madeni ya mabilion ya kesi mbona wanapeta barabaran na mavogo lakn hawakuwekwa ndani sembuse mtu ku2humiwa kusema neno panya! Mie sio tatizo kwa jinsi 2lpofikia na kaneno hako. Hayo mambo ya siasa mwisho wake ni vurugu tu.
 
Kwa hiyo tuhuma ya OCD imebaki moja tu sasa ya kuwaita wananchi panya ambayo ikikosa vielelezo ocd hatapatikana na hatia yoyote, na kauli yake ya malezi mema ya familia yake itakuwa kweli.
 
palalisote;2748838 “Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu said:
Utetezi wa aina hii kwa mtu anayeshughulika na maswala ya usimamiaji wa sheria inadhihirisha udhaifu mkukwa kwa watu wanaoteuliwa kuzisimamia sheria nchini. Ndio maana kesi nyingi zinazofunguliwa na polisi kwa niaba ya serikali zinaishia kutupiliwa mbali kwakuwa wanapeleka mashaidi wenye utetezi wa aina hii.

Kweli safari bado ni ndefu!
 
polisi wanamchunguza polisi mwenzao hapo kuna haki itatendeka kweli kwanini wasitafute independent entity kuchunguza issue nzima. we need an independent eye to look into it and not someone who has a dog in the fight.

Nilitegemea huyo ocd angesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi lakini hawajazungumzia jambn hilo. Na hapo ndio uchunguzi unapotiliwa shaka!
 
Back
Top Bottom