Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
Obama aanza kusaka raia wa kigeni Marekani Send to a friend Wednesday, 11 May 2011 21:25 0diggsdigg
WASHINGTON, Marekani
RAIS Barack Obama wa Marekani,ameamua kuimarisha ulinzi wa nchi yake na tayari ametangaza mageuzi makubwa na ya haraka, katika mfumo wa uhamiaji.Hatua hiyo, inakuja wiki moja baada ya Kikosi Maalumu cha Jeshi la Marekani, kumuua aliyekuwa akiongozi wa Kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden, katika mji wa Abbottabad, nchini Pakistani.
Akizungumza katika Jimbo la Texas juzi, Rais Obama alilitaka Bunge la nchi hiyo, kuwachambua raia wanaoishi Marekani kwa kuhamia, ili kujiridhisha na uhalali wao.Inasemekana kwa sasa Marekani ina watu milioni 11 wanaoishi kama raia wa kuhamia.Hata hivyo, Rais Obama ametaka watu hao wafuatiliwe upya na kuthibitishwa uraia wao.
"Tuna nguvu na ulinzi wa kutosha katika mipaka ya nchi yetu hata watu wengi wanaamini hivyo. Kilichobaki ni kuwaoatia vibali wahamiaji wanaoishi hapa nchini kwetu,"alisema kiongozi huyo wa Marekani.
Rais Obama alisema mageuzi katika mfumo ya uhamiaji, pia yataleta manufaa ya kiuchumi kwa watu wa tabaka la kati na katika nyanja ya biashara.Alisema mageuzi ya mfumo huo, yataimarisha pia usalama wa kitaifa.
Alisema kwa sasa sera ya uhamiaji ya Marekani si nzuri na kwamba inapaswa kufanyiwa marekebisho ya haraka hasa ikizuingatiwa kuwa Marekani ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya wageni wanaotaka kupewa uraia wa kudumu.
Obama alisema hiki ni kipindi cha kila mtu kuangalia uchumi na kwa msingi huo, sera ya uhamiaji lazima izingatie hilo na kwamba kuwanyima watu vibali, ni kuzorotesha uchumi wa nchi.Alisema sekta ya uhamiaji ni ya muhimu katika kila nchi inayowajali watu wanaohamia wakiwa wana kila sifa ya kupewa vibali.
Wakati huo huo, Marekani imeimarisha msimamo wake wa kuikosoa vikali China kuhusu rekodi yake ya haki za binadamu kwenye mkutano uliofanyika jana mjini Washington.Akizungumza mwishoni mwa mkutano huo wa siku mbili wa kila mwaka kati ya nchi hizo mbili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema nchi hizo zinapaswa kuzungumzia wazi wazi tofauti zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Clinton aliilaumu China kwa ukiukaji wa haki za binadamu na kwamba nchi hiyo, itakuwa inafanya makosa ikifikiri inaweza kuzuia mageuzi huku maandamano ya kupigania demokrasia yakiendelea katika mataifa ya kiarabu.
Katika mkutano huo, Marekani pia ilisaini mkataba na China kuhusu uchumi unaonuiwa kuboresha uhusiano kati ya dola hizo kuu kiuchumi duniani.