Obama: Tulikosea kuivamia Libya na kumuondoa Gaddafi

Mtu anavamia nchi huru anaipiga na kuisambaratisha anakiri alifanya unyama kuliko mnyama ameua mamilion ya waafrika wenzetu kule Libya...bado anakiri ameua hakamatwi wala hauwawi kama wenzie wote aliowaua ni aibu sana na fedheha kwa Afrika
 
Ndio mana nachukia wale wajinga wanaoitwa ICC wanataka nn tena kama ameshakiri mwenyewe kwann asikamatwe kwa mauaji ya Kiongozi wa Nchi na kuiharibu nchi huru ya Libya..Obama i ni muuaji mbaya sana sana..yeye na sakozy na mla rushwa Cameroun wanatakiwa kukamatwa
Teh teh hajasaini mkataba wa kuwa member wa hiyo mahakamani kwahiyo huwezi kumkamata.
 
Walibya wadai fidia ya $ trilion 900 kuirudisha Libya!
Wamdai nani kwa upumbavu wao! Majitu yamelishwa sumu na watu wa magharibi eti wapate true democracy, wakamuua Gaddafi kwa kumuonea tu, acha wachinjane na ma ISL na ISIS yao huko. Nchi imebaki magofu matupu.
 
Hapo sasa ndio amemualibia Clinton kwasababu kwa namna yoyote lazima nayeye clinton alihusika kwenye hilo kosa kwasababu wote walikua wanafanya kazi pamoja kwa kushirikiana.
 
Obama mwenyewe amekiri kuwa walifanya kosa kubwa Libya lakini cha kushangaza kuna watu humu wanajifanya wao ni zaidi ya Obama.
 
Usichojua ni kwamba, vita nyingi zinaanzishwa na makampuni makubwa yanayotaka rasilimali kwenye nchi husika.

Tafuta kitabu kinachoitwa "Fuel on the fire" cha Greg Muttitt. Kitakupa mwanga ni nani hasa alitoa wazo na alianzisha vita ya Iraq.
 
anachofanya Obama ni kwa maslahi ya Wamarekani..sasa wewe endelea tu kuhoji ''UAFRIKA'' ama 'UCHOTARA'' wake...
 
Ni kweli uliyosema kuhusu Gadaffi, Pia kumbuka Obama kuwa rais wa marekani sio kwamba atafanya kila kitu kwa mamlaka yake hapana kuna vingine anaambiwa afanye hata kama hapendi bali ni kwa interest ya nchi anayoiongoza (Marekani) atalazimika kuvitekeleza. Ni wazi Gadaffi hakupewa support na waafrika kama alivyoamini ni ndugu zake wakati wa vita nchi zote za afrika zilinyamaza kimya isipokuwa Zimbabwe tu Mugabe alilaani vikali kitendo cha Marekani kumvamia Gadaffi hivyo lawama zisiishie kwa Obama tu bali hata sisi waafrika viongozi wengi ni wanafiki na vibaraka kwa wazungu
 
Usichojua ni kwamba, vita nyingi zinaanzishwa na makampuni makubwa yanayotaka rasilimali kwenye nchi husika.

Tafuta kitabu kinachoitwa "Fuel on the fire" cha Greg Muttitt. Kitakupa mwanga ni nani hasa alitoa wazo na alianzisha vita ya Iraq.

Hapa sijaongelea kuhusu Iraki, bali nimeongelea kuhusu Obama kumuua Kiongozi wa Kiafrika M.Gadafi!
 
Ni kweli uliyosema kuhusu Gadaffi, Pia kumbuka Obama kuwa rais wa marekani sio kwamba atafanya kila kitu kwa mamlaka yake hapana kuna vingine anaambiwa afanye hata kama hapendi bali ni kwa interest ya nchi anayoiongoza (Marekani) atalazimika kuvitekeleza. Ni wazi Gadaffi hakupewa support na waafrika kama alivyoamini ni ndugu zake wakati wa vita nchi zote za afrika zilinyamaza kimya isipokuwa Zimbabwe tu Mugabe alilaani vikali kitendo cha Marekani kumvamia Gadaffi hivyo lawama zisiishie kwa Obama tu bali hata sisi waafrika viongozi wengi ni wanafiki na vibaraka kwa wazungu

Kwanza siyo kweli kwamba nchi za K iafrika hazikutoa msaada kwa Gadafi, J.Zuma wa AK mpka alituma South African Air force kumchukuwa gadafi lkn Gadafi alikataa na aliamua kufia kwenye ardhi aliyozaliwa, hata nchi yetu pia ililaani mashambulizi yaliyofanywa na Obama dhidi ya Gadafi lkn zaidi ya kulaani nchi kama yetu Uganda au sijui Swaziland na wangefanya nini kuzuia makombora ya Obama dhidi ya Gadafi?
 
View attachment 336567

Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.

Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.

Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.

Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.

Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.

Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.

Chanzo: BBC
I SEE INAKUWAJE KWA UHARIBIFU HUU NA PIA KWA MAISHA YA RAIA YALIYOPOTEA WAWALIPE AISEE
 
kwa
Usichojua ni kwamba, vita nyingi zinaanzishwa na makampuni makubwa yanayotaka rasilimali kwenye nchi husika.

Tafuta kitabu kinachoitwa "Fuel on the fire" cha Greg Muttitt. Kitakupa mwanga ni nani hasa alitoa wazo na alianzisha vita ya Iraq.

KWANI IKULU YA OBAMA NI KAMPUNI? NATAKA NINUNUE SHARE
KWANINI AOMBE RADHI KAMA VITA VILIFANYWA NA MAKAMPUNI NA SIO IKULU YAKE?
 
kwa

KWANI IKULU YA OBAMA NI KAMPUNI? NATAKA NINUNUE SHARE
KWANINI AOMBE RADHI KAMA VITA VILIFANYWA NA MAKAMPUNI NA SIO IKULU YAKE?

Yeye anafuata proposals za makampuni. Makampuni yakipata faida na nchi yake inapata faida.
 
Back
Top Bottom