Obama: Tulikosea kuivamia Libya na kumuondoa Gaddafi

You are as stupid as your thoughts. what is good about this stupid Trump who only dreams of building walls between him and other people? If not creating barriers, his other main dream is colonizing Africans. To hell with Trump and whoever supports him.

Huna haja ya kutukana!
Kama hujui kusoma unaweza kuomba kusomewa.
Trumph anawakilisha Msimamo thabiti na halisi wa Marekani tofauti yake na kina Hilary Clinton ni igizo la kuwapumbaza wepesi wa kuwaza kama wewe! Mwisho wa siku mkisikia Trumph kaangushwa mnashangilia Wamarekani hawapendi ubaguzi kumbe ...
 
Ndio mana nachukia wale wajinga wanaoitwa ICC wanataka nn tena kama ameshakiri mwenyewe kwann asikamatwe kwa mauaji ya Kiongozi wa Nchi na kuiharibu nchi huru ya Libya..Obama i ni muuaji mbaya sana sana..yeye na sakozy na mla rushwa Cameroun wanatakiwa kukamatwa
 
You are as stupid as your thoughts. what is good about this stupid Trump who only dreams of building walls between him and other people? If not creating barriers, his other main dream is colonizing Africans. To hell with Trump and whoever supports him.
Kwani Africa hatutawaliwi? Kuna kitu kinaitwa ukoloni mambo leo. Huu ni mbaya kuliko ule wa direct. Maana tunajiona tupo huru, kumbe hakuna kitu
 
Kosa kubwa zaidi ni kule kudhani walilokosea Libya ni kutoandaa Mazingira mazuri baada ya kuivamia na Kumuondoa Ghadafi.

Kama Libya ingekuwa inatawalika leo kwao Uvamizi ule ungekuwa halali.
Namkubali sana Donald Trump kwa kuwa Mungu kamuwezesha kutokuwa Mnafiki ana ujasiri wa kueleza hisia zake za kweli
Nakubaliana nawe kabisa ktk maoni yao kuhusu huo uvamizi. Kosa siyo matayarisho. Kosa ni lile lile linalorudiwa na viongozi wa Marekani tena na tena la kuvamia nchi za watu na kudhani watatengeneza visattelite vyao (natumia euphemism hapo).
Na Donald Trump ndiyo atakuwa worse then even Bush. You see, jamaa anasema kabisa kwamba atavamia Iraq na kulipua kila kitu kwanza. Trump ni more impulsive, inconsistent, na kwa jumla haoneshi uelewa wa kutosha wa historia, jiografia, siasa za nje, na hata utamaduni wa nje. Hiyo ni recipe ya kiongozi kilaza ambaye ataleta madhara makubwa. Ni muhimu kabisa aifahamu dunia vizuri zaidi. Watu walipuuzia umbumbumbu wa GWB na matokeo yake wanayajutia hadi leo. No, friend, Trump will definitely be worse than anything you have seen.
 
barafu
Hawa jamaa sijui Mashetani???
Iraqi walikosea kumuondoa SADAM
Libya walikosea kumuondoa Col: Gaddaffi
Afghanistan walikosea kuwaondoa TALIBAN
Somaliya walikosea kumuonda SIAD BARRE !!!
Iraki,sirya,libya,na nchi nyigine zinazozalisha wakimbizi ulaya ndo majuto yatakapo zidi baada ya watu hao kuzaliana na kuondoa vizazi vyao
 
View attachment 336567


Rais wa Marekani Barrack Obama amesema katika mambo anayoona alifanya vibaya katika uongozi wake ni ule uamuzi wa kuivamia Libya na kumuondoa Rais wa nchi hiyo Muamar Ghadafi.

Obama amesema hayo wakati akihojiwa na kituo cha Luninga cha Fox News cha nchini Marekani.Amasema kosa kubwa ktk uongozi wake ni kuivamia Libya huku akiwa hajajiandaa kuweka mazingira mazuri ya utawala baada ya kumuondoa Ghadafi.

Msome zaidi hapa Obama ajutia makosa ya Marekani nchini Libya - BBC Swahili

Hapo kwenye red, sio sahihi. Ukimsikiliza Obama mwenyewe na hata ukipitia article ya BBC utapata ujumbe tofauti na ulichoandika. Alichosema Obama ni kwamba Marekani haikuwa na mpango wa nini cha kufanya mara baada ya kumuondoa Ghadafi, lakini kumundoa Ghadafi bado wanaona walikuwa sahihi.
 
Hapo ndipo utajua kwamba hawa ni wanyama


US President Barack Obama says his “worst
mistake” in the past eight years has been the
mishandling of the crisis in Libya after the US-
backed ouster of former Libyan dictator
Muammar Gaddafi in 2011.
Speaking to Fox News on Sunday, Obama said
his “worst mistake” was “probably failing to
plan for, the day after, what I think was the
right thing to do, in intervening in Libya.”
This is while in a BBC interview two weeks ago,
Obama had raised a similar point, adding
"that's a lesson I now apply when we are asked
to intervene militarily. Do we have a plan for
the day after?"
In March 2011, a coalition of US-backed Western
countries, including the UK and France,
launched missile and air strikes on Libya in a
bid to help oust Gaddafi following a national
uprising.
Gaddafi was deposed later that year shortly
after the fall of the capital Tripoli on August
20.
But the ensuing power vacuum allowed various
militant groups, including a Daesh affiliate, to
gain power in the country and exploit its
natural resources.
Both Obama and then US Secretary of State
Hillary Clinton keep arguing that Gaddafi’s
overthrow did not incite the Libyan crisis and
the chaos was rather caused by the coalition’s
failure to prop up a stable government in the
days following.
Obama has also put part of the blame on two
traditional US allies, France and the UK, saying
he was wrong to believe they would be
"invested in the follow-up" to Gaddafi’s ouster.
“When I go back and I ask myself what went
wrong, there’s room for criticism, because I had
more faith in the Europeans, given Libya’s
proximity, being invested in the follow-up,”
Obama said in March.
Obama slammed British Prime Minister David
Cameron, in particular, for getting “distracted
by a range of other things” rather than focusing
on Libya.
He also censured France’s ex-president Nicolas
Sarkozy for being “too eager” to take credit for
the Western military intervention against
Gaddafi.
Meanwhile, back in March a six-member UN
panel published their report, stating that Daesh
had “significantly expanded” its territory in
Libya and was posing a severe threat to the
country’s oil installations.
“Libyans have increasingly fallen victim to the
terrorist group's brutalities, culminating in
several mass killings,” the report added.
 
Obama ni mnafiki sana kuliko marais waliopita , Bush aliivamia Iraq na kumng'oa Saddam Hussein kwa kisingizio cha umiliki wa silaha za maangamizi ili hali hazikuwepo Bush akutoa unafiki wake kwakuwa alikuwa anajua anafanya vile kwa maslahi ya taifa lake. 2011 Obama kafanya vilevile lakini kwa unafiki wake anajutia leo wakati Syria anataka kufanya kama Libya na ametumia miaka 5 sasa ila kwa msaada wa urus anaelekea kushindwa.

Kwakuwa amekubali kinafiki kuwa walifanya kosa kuivamia Libya na kuangusha utawala wa Gaddafi basi waache haraki zao za kumuondoa Assad ili wasifanye kosa lingine maana waswahili wanasema kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa, akifanya hivyo nitaona kuwa yeye sio mnafiki.
Nimeona kuna wadau wanasema Obama apelekwe ICC kufunguliwa mashtaka, ni kweli lakini USA sio mwanachama wa ICC alafu yeye ndio kiranja wa dunia hivyo yupo juu ya maamuzi yote ya kimataifa UN ilikataa uvamizi wa Iraq lakini Bush akaagiza majeshi yavamie. Blair mwenyewe alihojiwa na mamlaka za UK kwa kutoa uamuzi wakupeleka vikosi Iraq na ikaonekana kuna ukiukwaji wa sheria za kimataifa lakini hakuna wa kumpeleka ICC, Hilary Clinton naye aliwekwa kitimoto juu ya uvamizi wa Benghazi lakini sasa anagombea nafasi ya kuwakilisha chama chake urais 2017. ICC haina meno kwa maovu yanayofanywa na nchi za magharibi, uvamizi wa Iraq na Libya ni uhalifu wa kijeshi lakini ICC haiwezi kemea kwa kuwa kuna double standards.

Marekani katika historia yake haijawahi kuikalia nchi nyingine pasipo kuiacha ikiwa haitawaliki, haigawanyiki na kuibuka vikundi vikundi vinavyohasimiana . Hebu angalia tangu waivamie Afghanistan na Iraq hizi nchi hazitawaliki hadi sasa utasikia Taliban, al Quida mara IS sijui Al Nusra Front. Kila siku ni mabomu tuu na serikali walizoziweka zinakosa ushawishi na uungwaji mkono na raia hivo kuleta vikundi vya kigaidi vinavyojaribu kutengeneza dola kwakuteka na kukalia ardhi.

Free Syrian army (FSA) kabla ya kujaribu kung'oa utawala wa Assad kwa msaada wa marekani wajitafakari sana huku wakiangalia kilichotokea Libya kama case study ya kitu wanachojaribu kufanya dhidi ya serikali halali ya Syria, badala ya kujuta baadaye kama wenzao walibya.

Naikubali sana ile kauli ya Donald Trump aliposema dunia na mashariki ya kati ingekuwa salama kama Gaddafi na Saddam Hussein wangekuwepo. Alisema ukweli mtupu bila kuficha kitu wala kuleta unafiki wa kimarekani katika amani ya mashariki ya kati na dunia kwa ujumla, maana kila mtu anaona kinachoendelea huko mashariki ya kati. Libya na Iraq.
 
Hapo kwenye red, sio sahihi. Ukimsikiliza Obama mwenyewe na hata ukipitia article ya BBC utapata ujumbe tofauti na ulichoandika. Alichosema Obama ni kwamba Marekani haikuwa na mpango wa nini cha kufanya mara baada ya kumuondoa Ghadafi, lakini kumundoa Ghadafi bado wanaona walikuwa sahihi.
Walimuondoa Col:G lakini na waLibya wakamuondoa Balozi wao kwa kumteketeza ndani ya jahanamu hapohapo ubalozini !!!
 
Sera zake za Mambo ya Nje hazikufanikiwa ata Syria pia wamekosea sana lakini Busara za Putin angalau Mwanga unaonekana.
 
Hapo kwenye red, sio sahihi. Ukimsikiliza Obama mwenyewe na hata ukipitia article ya BBC utapata ujumbe tofauti na ulichoandika. Alichosema Obama ni kwamba Marekani haikuwa na mpango wa nini cha kufanya mara baada ya kumuondoa Ghadafi, lakini kumundoa Ghadafi bado wanaona walikuwa sahihi.

Sasa kama walikuwa SAHIHI iweje huo USAHIHI ulete instability.
Nijuavyo mimi USAHIHI wa jambo au hatua hupelekea MATOKEO sahihi (Kwa maana ya manufaa)
 
Ndio mana nachukia wale wajinga wanaoitwa ICC wanataka nn tena kama ameshakiri mwenyewe kwann asikamatwe kwa mauaji ya Kiongozi wa Nchi na kuiharibu nchi huru ya Libya..Obama i ni muuaji mbaya sana sana..yeye na sakozy na mla rushwa Cameroun wanatakiwa kukamatwa

Hiyo ICC imeundwa kwa ajili ya sisi waafrica tusiojitambua and not for the white devils i mean (wazungu) na bado tunaendelea kuwanyenyekea washenzi hawa...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom