Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wazo la Kufikirisha: Hakuna Rais wa Marekani aliyefanya mengi kwa ajili ya Bara la Afrika na kuyanusuru maisha ya Waafrika wengi kama Rais George W. Bush. Uamuzi wake wa kuongeza kwa kiasi kikubwa fedha za kupambana na maambukizi ya HIV katika Bara la Afrika unasifiwa kwa kuokoa maisha ya watu wengi ambao madawa ya ARVs yalikuwa kwao ni kama anasa na hivyo walipoambiwa wako (+Ve) basi ilikuwa ni kama hukumu ya kifo. Leo hii mamilioni ya Waafrika wanafurahia maisha na kuendelea na majukumu yao mbalimbali kwa sababu ya uamuzi wa Rais Bush kuanzisha PEPFAR. Na kwa Tanzania ni Rais Bush aliyetoa msaada mkubwa zaidi na kufanya mengi zaidi kuliko marais wengine wote waliomtangulia na hata aliyemfuatia.
Cha kushangaza ni Rais ambaye Serikali yetu na Watanzania wengi hawajaoneshi ile shukrani anayostahili kwa mchango wake huo mkubwa. Cha kushangaza zaidi hata jina la kijimtaa kimoja kwa heshima yake hakuna!
Ila kaja Rais wa Marekani mweusi; well.. you know what happened!.... yote ambayo Obama alifanyiwa simply ni kwa sababu ya rangi yake si kwa sababu ya mengi aliyoyafanya...
"Sisi tunatukuza watu bwana, hatutukuzi rangi" alisema J. K. Nyerere