Obama Adaiwa Kuisaliti Ndoa Yake

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,408
Obama Adaiwa Kuisaliti Ndoa Yake
4423798.jpg

Vera Baker Monday, May 03, 2010 3:47 AM
Rais Barack Obama wa Marekani amekumbwa na skendo la kuisaliti ndoa yake kwa kujivinjari na mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele kwenye kampeni zake za uchaguzi wakati alipokuwa akigombea useneta miaka sita iliyopita. Rais Barack Obama wa Marekani anadaiwa kuisaliti ndoa yake na Michelle Obama kwa kujirusha na mrembo wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Vera Baker.

Mwaka 2004 wakati Obama akipiga kampeni za useneta ilidaiwa kuwa alijivinjari chumba kimoja hotelini na mrembo Vera Baker ambaye wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 29.

Wakati huo Vera alikuwa mdau wa karibu wa Obama kwenye kuchangisha fedha za mfuko wa kampeni na alifanikiwa kuchangisha mamilioni ya dola.

Miaka sita ikiwa imepita bila ya ushahidi hata wa picha kutolewa, jarida maarufu la Marekani National Enquirer limeliibua upya soo hilo likisema kwamba lina ushahidi wa video kuthibitisha kuwa Obama aliisaliti ndoa yake.

Jarida hilo ambalo lilijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya kuibua skendo la mgombea urais John Edwards kuwa anajivinjari kwa siri na mrembo Rielle Hunter na kwamba amezaa naye mtoto mmoja.

Skendo hilo lilipoibuliwa wakati huo, Edwards alikanusha vikali lakini ilipogundulika kuwa ni kweli, jarida la National Enquirer lilijipatia umaarufu mkubwa sana na kugeuka kuwa chanzo cha habari kwa vyombo vingine vya habari.

Hivi sasa National Enquirer linasema kwamba lina ushahidi wa video za kamera ya ulinzi kwenye hoteli ya jijini Washington D.C ambayo Obama na Bi Vera wanadaiwa kupumzika kwenye chumba kimoja.

Jarida hilo limesisitiza kuwa iwapo watu wataziona video walizo nazo basi wataamini kuwa rais Obama aliisaliti ndoa yake na Michelle Obama.

Obama hajasema chochote tangia National Enquirer lilipoliibua tena skendo hili ingawa Vera alishawahi kukanusha kuwepo kwa uhusiano wowote wa kimapenzi kati yake na Obama.
 
Hakuna kipya hapa, hii issue iliibuliwa 2004, ikakosa proof ikaja tena kwenye kampeni za uchaguzi 2008 ikakosa proof, sasa Ma wingnut wameona waiibue tena baada ya kuona jamaa anachanja mbuga na mikakati yao yote imekuwa useless. Kitakachofuata sasa watatengeneza video bado jamaa atawapiga bao. Ni kama vile wale birthers. Wanajua kuwa jamaa 2012 atawa-beat tena baada ya mbinu za kumkwamisha kushindwa. Hahahaha kweli Rightwingnuts wamefulia, bado action moja tu ya kujaribu bunduki nayo watashindwa.
 
hakuna mbaya Obama mwenyewe ni binadamu kama sisi ,haya mambo yapo kama kweli au si kweli ni yeye na life yake
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom