Zulqarnayn
Senior Member
- Oct 17, 2011
- 107
- 50
Mkuu ni Nzega sio Igunga
Tuweni makini na watu wasiyo raia wa nchi yetu, sasa mtu anaenda kuzuia watu wasilime zao la biashara, anataka nini mtu huyu? Yeye anagawa pesa, wali na nyama basi! Mwenzake anahamasisha maendeleo ya kilimo cha pamba!
Ila Kigwangalah kweli ni jembe la mapinduzi, mpaka Bashe hakukaliki Dar, ameona aanze kampeni mapema ili kushindana na spidi ya Kigwangalah! Saidi Bagaile achana na siasa za FB, endelea kupeleka maendeleo kwa wananchi tu hawatokusahau wakati ukifika kama utaendelea hivi!
Suala la Bashe na uraia wake tunalifahamu vizuri na wala lisikukoseshe usingizi...huyo atauona Ubunge kama uchi wa mtoto, maana ili awe Mbunge ni lazima JK atoke madarakani kwanza na yeye aweke sawa ishu ya Uraia wake (kitu kitakachochukua miaka 10!)Mara ya kwanza alilazimika kugushi nyaraka zake za Uraia (jinai hii) na sisi tunao ushahidi, ili agombee Uenyekiti wa UVCCM na pia alilazimika kufoji cheti chake cha kuzaliwa (jinai nyingine hii) ili apate fursa ya kugombea UVCCM. Pia alilazimika kugushi cheti cha kuzaliwa cha Mama yake mzazi ili kuhalalisha uraia wa Mzazi wake mmoja na kurahisisha utaratibu wa kupata Uraia kwa njia ya kuukana Uraia wa Baba yake na hapo kukwepa kuingia kwenye utaratibu wa kusubiri miaka 10 ipite kabla hajafikiriwa kuwa raia! Yote haya tunayajua, Kigwangalah acha kuhangaika na huyu Al-shabaab, fanya kazi bhana!
Zul