Nyumbani wamemkataa mchumba wangu. sababu: mhaya!

tunashuriwa tuwasikilize wazazi wetu na kamwe tusiwadharau eti kwa sababu wamepitwa na wakati kaa chini wakupe sababu zao kwanini wamemkataa mhaya kila mtu anasababu zake yawezekana wanasababu ya msingi kuliko kuanza kulalamika sawa siku hizi kila mtu ana uhuru wa kuchagua anavyotaka ila usije ukasema bora ningewasikiliza wazazi kwanza ukaja ukajuta. ushauri kaa na wazazi wako wakupe ushauri na kamwe usifanye mambo kibabe hakika utajajuta ingawa hatuombei hayo,
 
King'asti umenifanya nicheke,wangoni wana tabia gani kwani?nijuze
 
Last edited by a moderator:
za magono wa kunyumba.
mimi pia mngoni na kuna kaka yangu kaoa mhaya, yaani tunampenda yule wifi kupita maelezo, ana tabia nzuri sana....... kabila siyo tatizo kabisa kama alivyosema kaka yangu hapa, angalia tabia zake tu na uwe na sababu nzuri ya ku-convince wazazi

Kabwina!
nimefurahi kusikia wewe wa kunyumba lkn mbona sina bahati ya kukutana na watoto wa kingoni hivi wapo kweli, kila nnapogeuka ni watoto wa kichagga tuuuuu!!
 
hayo yalipitwa nawakati kuchaguliana wachumba kama unampenda shikilia msimamo wako jiamini unapofanya maamuzi yako nahiyo ndio sifa yamwanaume.oa unayempenda hatakama wao hawampend badae watamkubalitu hata kishingo upande.mke niwako si wawazazi
ni kweli unachosema ila baraka za wazazi pia zahitajika kwenye hiyo ndoa...........mimi nadhani mhusika anabidi ajitahidi kuwaelezea wazazi wake kuhusu tabia nzuri ya huyo mchumba wake............ili kuwatoa kwenye huo mtazamo wa kuwa wahaya wanatabia mbaya.
 
Mh hapa kazi kwelikweli, ila kumbuka ni dhambi kubwa sana kumzania mtu kwa kitu fulani, mapenzi ya dhati ndio kitu cha muhimu sana katika ndoa mkuu. Maamuzi yako na maamuzi ya Wazazi yote ni muhimu.....Jitahidi kuwaelewesha wazazi.


Tafakari chukua hatua
 
Ila hata mimi napenda sana wanawake wa kihaya na wa kisukuma, yani sijui kwa nini jamani
 
Wadau
nipeni ushauri nipo njia panda. ni kweli sababu waliyonipa kuwa wahaya wana tabia mbaya?

mi ni mngoni, nishauri!!

hata mimi nnakushauri usimuoe huyo mwanamke maana hyo product mtakayotoa itakua balaa maana wangoni pia kwa ngono hamjambo,hadi mmetunga ule wimbo wenu sijaushka vizuri hla nnakumbuka chorus ile nnapotaka mimi ni hapo tu.
 
sikia,ndoa unaoa wewe,kuchaguliwa mke kubaya mdogo wangu,mkianza kasheshe ndani ya ndoa wao watakuwa kando na sanasana watakuona mkorofi kamwe hawatakumbuka kama wao ndo chanzo cha matatizo.nakushauri tafuta wazee kwenye ukoo,waombe wakueleze baadhi ya ndoa ambazo zina utata ndani ya ukoo,angalia zipi zinaweza kuwa msaada kwako katika kujieleza,nina maanisha kuwa lazima utakuta za wangoni kwa wangoni,wangoni na kabila jingine ambazo zina shida,then waambie je wale ni wahaya,hapo utasimamia msimamo kuwa ndoa sio kabila,pia waeleze kuwa siku hizi ni zama za magonjwa,waambie wazi kuwa je ukimwacha unayempenda ukaoa usiyempenda ukianza kuiba nje ukapata magonjwa wajue wazi wanahusika!hawa wazazi wetu wana nafasi ktk maisha yetu lakini wasituchagulie wenza kama walivyokuwa wanatuchagulia shule!nakwambia ukiwa soft utaacha umpendae hivihivi!
 
Unatafuta MKE WENU au MKE WAKO??????????????????

Unatafuta Kabila au Mke wako????????????????????????

Ndoa yako ni kwaajili ya satisfication ya ukoo wenu????????????

MUOMBE MUNGU AKUPE MKE WAKO

kumbuka WAZAZI ni wawakilishi wa MUNGU hapa Duniani! mara nyingi Mungu unena nasi kupitia kwao!

Ukidharau mwiba, utakuchoma, na mguu tatoa Usaha!
 
kumbuka WAZAZI ni wawakilishi wa MUNGU hapa Duniani! mara nyingi Mungu unena nasi kupitia kwao!

Ukidharau mwiba, utakuchoma, na mguu tatoa Usaha!

Acha uongo kila mtu anamwakilisha Mungu hata yeye (mungu) alisema kulingana na maandiko ya kikristo amemuumba mtu kwa mfano wake lakini kuna wazazi wengine wameumbwa kwa mfano wa mungu lakini wanamwakilisha Shetani hapa Duniani!

 
tupo timemi ngo!........................... jova kingi

nongiiiiii!mimi hapo kwenye bold tu nimecheka karibu niumwe,hapo mngoni kasisitiza kitu kwelikweli!na saiuti inakuwa ya mkazo balaaa.dah!u made mya day mlongo wangu,ngati kaka mwenyee huyu ababii mchaga sijuiiiii!ah gangi nene agha! wengo!
 
Back
Top Bottom