Nyumba za mbezi beach zageuka mabwawa ya samaki

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Wanandugu waishio tankibovu na pembezoni,

Kama hujafika nyumban jitahdi ununue ma buti ya plastic kama yanapatikana.

Huku karibu kila nyumba maji yameingia ndani ukipata bahati ndio unaweza kuingia lakini wengi wametoa magodoro na kwenda nyumba wanazojua kusitiri maisha yao.

Hakika ni mvua ambayo atkuwahi kujua yaweza kufikia kiasi hiki

Ukishuka Tanki bovu kuingia Barabara ya BILLS LODGE kila nyumba pembezoni zinatoa maji kuna ambazo walikuwa ndan wanasubiri usiku kuzoa maji ...kuna ambao waliamua kukodisha water pump na sasa ukipita sehemu hizo ni makelele utasema mitambo ya DOWANS pale UBUNGO kumbe ni water pump zinatoa maji.

Bado najiuliza ni miundombinu ama ni nini kinafanya nyumba zote hizi kuingia maji

Tunawaomba wenye uwezo wa kukodisha water pump wafike TANKI BOVU HARAKA KUOKOA watu waweze kuingia nyumbani kwao kwa amani!
 
Askari wa zima moto si kazi yao? Pia JWTZ si waje waokoe?

Kama wananchi, kama viongozi.
 
poleni jamani..karibuni huku vikindu mambo safi hakuna mambo yenu ya mjini hayo eti maji yanajaa ndani badala ya shamba
 
tatizo lenu hamhusishi miundo mbinu yenu na utawala ulioko madarakani, mnadhania ni mapenzi ya Mungu! Ogeleenii tu yatakauka na kesho itakuwa kama jana.
 
ni kweli mwana kj
naona mama mmoja anadai hapa yoote ni maoenzi ya mungu...duh sasa sijui mapenz ya mungu godoro kuelea juu ya maji yananikumbusha mambo ya petro kule baharin
 
huu ndio muda wa kutafuta viwanja na nyumba za kupanga mbezi beach.
Poleni lakini pia mnaweza mkahamia huku kwetu Yombo vituka kwa muda,,,,
 
Halafu ukiuliza bei ya nyumba au kiwanja, unaambiwa $300, 000! Haya bwana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom