Nyumba za Mawaziri - nani amehamia kule?

sasa nani wanaishi kwenye hizo nyumba jamani; we have established kwamba mawaziri na manaibu wao wengi hawaishi huko. Je ziko tupu?

Duuh Mkuu Mwanakijiji........hebu tuachie tupumue kidogo.....maana ile hoja ya kuuza nyumba za kule O'bay....tuliipitisha kwa taabu sana.......je unafikiri tulimaanisha kile tulichojengea hoja?....shoot!
 
kwa sababu tumekubali kuwa watawala wao wanastahili maisha ya heri. HIvi mnakumbuka zile nyumba za mawaziri zilijengwa kwa kiasi gani kila moja? Ni mawaziri wangapi wanaishi kwenye nyumba zile? Je Mawaziri wote wanaishi kwenye nyumba zile?

Nilikuwa natafuta specs zake...

Mwanakijiji nadhani swali rahisi liwe nani anaishi nyumba tofauti na zile dedicated kwa mawaziri. Say wanaokaa kwenye nyumba zao, Mimi naanza kuorodhesha:

1. Prof Mark Mwandosya - Kunduchi

2. Hussein Mwinyi - Mbezi Beach

3. Batilda Burian - Mbezi beach

4. Anna Makinda - Sinza

5. Makongoro Mahanga - Segerea

6. Magufuli - Ada Estate

7. ..........

8...............

9.....................
 
Mwanakijiji nadhani swali rahisi liwe nani anaishi nyumba tofauti na zile dedicated kwa mawaziri. Say wanaokaa kwenye nyumba zao, Mimi naanza kuorodhesha:

1. Prof Mark Mwandosya - Kunduchi

2. Hussein Mwinyi - Mbezi Beach

3. Batilda Burian - Mbezi beach

4. Anna Makinda - Sinza

5. Makongoro Mahanga - Segerea

6. Magufuli - Ada Estate

7. ..........

8...............

9.....................

asante..
 
Huenda zimefanywa getho za watoto wao


Zile nyumba sio mbaya kama wengi wanavyodhani ..ni za ghorofa ....na room nne juu kuna master ..ofisi./study etc..na garage...tatizo la zile nyumba kubwa ni Maji....kuna wakati walikuwa wanasombewa maji na malori.....simnajuwa maisha ya masaki..labda huu mradi mpya wa maji utasaidia...

Tatizo la pili na ambalo ndilo kubwa[kwani mawaziri wengine nyumba wanazoishi uswazi hazifikii zile]....wanasema kule ni kama STAFF QUOTERS ...wanakosa privacy...na kumbukeni mara ya kwanza hata fence zilikuwa hazijashika vema ...wengi hasa kutokana na siasa....hawataki nyumba yake iwe wazi kiasi jirani anajuwa nani amemtembelea???...simnajuwa mambo yetu yale...iwe kwa mwanamume au mwanamke[import and export].....au simply kwa wenzake kujuwa tu aina ya wageni wake ....wanaweza moja kwa moja wakamjuwa ...na ku connect dots!!

Kuna mawaziri zile nyumba hawakai lakini wanazitumia[na ni wengi tu]....hasa wanapokuwa na mambo yao wanayoitaji kufanya karibu na mjini...kwa maana hiyo wanaweka wanafamilia au walinzi kuwaangalizia....??
 
Kuna mawaziri zile nyumba hawakai lakini wanazitumia[na ni wengi tu]....hasa wanapokuwa na mambo yao wanayoitaji kufanya karibu na mjini...kwa maana hiyo wanaweka wanafamilia au walinzi kuwaangalizia....??

Hapa yawezekana umetoa jibu nililokuwa ninashuku.. kama kuna watu wengine wanaishi kule.. na mawaziri bado wanaishi kwingine.. nani analipa? Isijekuwa serikali inawalipa posho upande huu.. halafu na wenyewe wanalipwa na watu waliowapangisha upande ule.. halafu mambo yanakuwa juu ya mambo..
 
...Lakini wazee watumishi nyeti wa serikali kuwa na nyumba karibu na mjini ni muhimu...wewe fikiria kama waziri anakaa Tegeta ....na foleni hizi ,muda anaopoteza njiani ni mkubwa sana yet hata ikitokea dharura inakuwa tabu..kuwahi mjini...

Nafikiri nyumba za viongozi miaka ile kujengwa kilometa 3 toka ikulu it was very strategic...kufanya utawala uwe rahisi.......sasa tumeamua kuwauzia na wao karibu zote wameshaziuza kwa wahindi......siku hizi ukienda Oysterbay kumekuwa soo crowded ...its like high density area..soon patafanana na siza ..kila nyumba imejeuka duka/baa ili mradi ipo road side..aibu ni wazi wanaoishi pale hawastahili...tangu lini seheme ya house grade A wakaruhusu upuuzu huo..sheria ya planning...haisemi hivyo...it was not supposed to be like that...ina maana hata kama wameuza watu wa Ardhi wangeweka wazi kuwa oysterbay sio upanga...mtu akitaka kujenga nyumba ajenge Mansion...na sio apartments...tangu mwanzo eneo la apartments lilikuwa upanga!!

Kikwete naye aliahidi kwenye kampeni zake za chini kwa chini kuwa angezirudisha .....kumbe naye aliuziwa nyumba oysterbay....,kimsingi kitendo cha Mkapa kuamua kujenga magorofa karibu 100 ya mawaziri na makatibu wakuu maeneo ya masaki ,na mikocheni,na baadhi ya maeneo nyumba za wakuu wa mikoa na wilaya.... ni wazi kuwa na yeye aligundua kuwa alifanya makosa kuuza zile nyumba......
 
Isijekuwa serikali inawalipa posho upande huu.. halafu na wenyewe wanalipwa na watu waliowapangisha upande ule.. halafu mambo yanakuwa juu ya mambo..


du mwanakijiji..kupangisha ....du !! waziri atakayeweka mpangaji kwenye state house[rember nyumba official ya waziri ni ya state]....atakuwa ana njaa ya kufa mtu....atakuwa amefanya kashfa ...amounting kwenda kinyume na kiapo...maana huyo mpangaji kwa kuishi tu pale anaweza kujuwa siri za serikali akitaka .........itabidi ufanyike utafiti kama kweli kati ya wanaoishi kama ndugu mule wanalipa kodi!!

mnajuwa kuwa bado serikali ina tatizo la nyumba zenye hadhi....ni bora wangetenga eneo kama kigammboni...ni karibu na maofisi ili siku pakiwa na daraja serikali ijenge official residence kwa maofisa waliobakia......Tanzania mfano manispaa nyingi hazina official mayors residence....,ukienda mahakama kuu hakuna official CJ residence...yenye hadhi,na majaji wengine pia,hakuna official speakers residence [dar na dodoma]....hatuna official IGP,CP,....Residences...,ukienda jeshini ..siku hizi ma brigedia wanakaa uzwazi...hakuna official CDF...Residence...etc...

Ninapoongelea official residence namaanisha ni nyumba iliyotulia inayoendana na protocal zote za cheo husika kwa kadiri ya sheria na haki stahili....ina maana kwa mfano mkuu wa majeshi akiwa na mgeni awe na uwezo wa kumfanyia reception nyumbani na sio hotelini.......sasa tatizo watu wengi wanafikiri zile nyumba wanozoishi ndizo zenye eneo la nusu eka ni za vyeo vyao...nyumba za serikali duniani kote zipo kwenye madaraja.....sisi chache tulizokuwa nazo tumeuza.......mmomonyoko wa maadili pia unachangiwa na viongozi kuishi ovyo ovyo!!
 
Hivi viongozi wetu wamerogwa, inakuwaje kila administration inakuja eti wanajenga nyumba mpya za mawazi, mara makatibu wakuu, mara magavana nao wanajijengea nyumba mpya. Jamani, si tumepata uhuru toka 1961, sasa wakati wote huo hao mawaziri, sijui makatibu wakuu walikuwa wanakaa wapi?. Hivi kweli hatuna sheria zinazoashiria au kukataza haya mambo ya kila kiongozi kujiamulia amulia kufanya anachotaka kufanya, uugh! sometimes it just makes me sick. Someday something will have to give, tunahitaji a whole system overhaul.
 
Masawila, Baada ya kugundua kuwa wao ni waheshimiwa, kila kitu kinafanywa kufikia hadhi ya uheshimiwa wao. Spika anakataa nyumba anayopewa kwa kuwa si ya hadhi yake. Ikulu nayo kila mwaka inakarabatiwa kwa mabilioni iendane na mpangaji wake ambaye hadhi yake inapanda kila kukicha.
 
Hivi viongozi wetu wamerogwa, inakuwaje kila administration inakuja eti wanajenga nyumba mpya za mawazi, mara makatibu wakuu, mara magavana nao wanajijengea nyumba mpya. Jamani, si tumepata uhuru toka 1961, sasa wakati wote huo hao mawaziri, sijui makatibu wakuu walikuwa wanakaa wapi?. Hivi kweli hatuna sheria zinazoashiria au kukataza haya mambo ya kila kiongozi kujiamulia amulia kufanya anachotaka kufanya, uugh! sometimes it just makes me sick. Someday something will have to give, tunahitaji a whole system overhaul.

wakoloni na baadaye Nyerere walijenga Gov/State quaters ..nyie[sisi] tumeuza..teh teh...sasa tunaaza moja aisee!!

mfano Dar mgawanyiko wa nyumba ulikuwa hivi..
1]goverments/parastatals house grade A[masaki obay]
2]grade B [some in mikocheni and Upanga]
3]grade B -kurasini estate.,na nyuma ya serengeti breweries
4]grade C - TEMEKE sigara club area...etc

Junior quaters in Ilala,Magomeni..etc

na kwa mikoani mnajuwa kuna maeneo yalikuwa yakitwa UZUNGUNI ...hayo ndio maeneo yaliyokuwa na gorverment houses grade A...

Zote zimeuzwa inatia UCHUNGU!!!!...

Then mnalalamika mawaziri wanakunywa rose garden hadi asubuhi ....wanalewa .....LEADERS CLUB iko wapi ...Ambako enzi za mwalimu ndio ilikuwa seniour officers club...kuna cheo ukifikia kinaendana na Ethics....lakini leo hii leaders CLUB ...ni sehemu ya kuchezea NGWASUMA na twangapepeta ....wenyewe sijui wanaita..nini sijui ..jumapili na jumamosi....??? what a waste??? na huo ni mfano wa kilabu za viongozi zilizotapakaa nchini..kila mkoa ulikuwa nayo au wakikosa ....wanakunywa OFFICERS MESS....zipo mfano wa ile ya Oysterbay officers mess.....

ZIKO WAPI ??!!??.....Tumeharibu utaratibu kupita kiasi.....itahitaji muda kurudisha hadhi na nidhamu iliyokuwepo kwa watumishi wa umma!

mnakumbuja mwalimu kwenye hotuba yake mwisho mwisho ali joke kuhusu maadili.......akasema ..uingereza walimfukuza kazi waziri kwa sababu tu alionekana mtaa wa changudoa usiku...pamoja na kuwa hakuonekana na changudoa..!...alikuwa akimaanisha intergrity ya kiongozi inamaanisha pia maisha yake ..na watu wanaomzunguka matendo yao.......lakini leo huwezi kumsema waziri au seniour civil servants ....ambaye amepanga flat magomeni kwa kukosa nyumba...asiende kwa macheni au travertine kupata moja moto moja baridi!!....na wale viongozi wanaoishi kinondoni nyuma ya makaburi [karibu na zile ofisi].....walinzi wao usiku wanakodisha vibanda vya guard qoater getini kwa watu wa chap chap....mabosi zao wamelala ndani......au pengine kama mama hayupo mzee naye anapelekewa!!...ujasiriamali mwingine huo!!
 
Aaagh haya mbona inabidi tuyazoee tu, hii ndio Tanzania yetu tufanyaje sasa na watawala wameamua kutufanya sie wajinga, kwasababu kwa kweli naamini gharama za kujenga nyumba zile zingesaidia sana kuokoa maisha ya watanzania wengi walio vijijini ambao wanakufa kwa kukosa zahanati na dawa, pia ndugu zetu kule wanaosomea chini ya miti..,Viongozi wa nchi hii wana kasumba ya kupenda sana mambo ya kifahari na kuwasahau kabisa waliowapa dhamana hizo ambao wanataabika na makali ya maisha.
sidhani kama kulikuwa na logic ya kujenga hizo nyumba kama wanaojengewa wenyewe hawako tayari kukaa, ni upotezaji wa fedha za walipa kodi tu, utakuta mtu hataki kukaa humo na bado anadai housing allowance...,wana bahati sana hawa kama mimi ndio ningekuwa rais au PM wote wangekaa kwenye hizo Quarters na tena wangekuwa na STAFF BUS..No MASHANGINGI
 
Back
Top Bottom