Nyumba za Mawaziri - nani amehamia kule?

Kama hakuna anayeishi kule basi tukubaliane kwamba serikali hii ni ubabaishaji mtupu. haitimizi inachopanga
 
Mawaziri wenye nyumba zao binafsi kama vile Husen Mwinyi na hao wengine, kwa nini wakaishi pale kambini?

Hata mimi ningeendelea kuishi kwangu kuliko kesho naondolewa uwaziri halafu nahamisha virago vyangu.

Hata uncle Karume kaamua aishi kwenye kasri lake na kuikacha ikulu aliyopangiwa!
 
msanii.. kuna watu wanaishi kule; ninachochokoza hapa ni kina nani wanaishi kule? Itakuwaje kama Waziri kampangishia kimada wake kule au watoto wa mkaza mjomba?
 
Sasa anaishi nani kule?

Utakuta nyumba zote hizo zimeshaandikishwa majina ya mawaziri kuwa wanaishi humo kwa malengo. End of 2015 wata kaa kikao chao cha baraza lao na kuamua kuwa wauziwe kwani si vizuri wakistaafu halafu hawana pa kuishi, unakumbuka mwisho wa kipindi cha BWK?. Theoretically kwa sasa watakuwa wanaishi mawaziri lakini practically nafikiri zitakuwa ni nyumba za Tandu na buibui.
 
Nani alianzisha huu mtindo wa kuuza mali za umma kwa viongozi kinyemela? Na kwa nini wauizwe nyumba hizo? Ina maana kuna wakati rais anayemaliza muda wake naye atataka auziwe Ikulu; tutamkubalia?
 
Sio larisi kwa hawa mawaziri kuweza kukaa pamoja, si wamoja wameunganishwa na nia yao ya kutaka vyeo lakini sio watu wanaoshabihiyana. Wengi walijaribu naona sasa wamerudi kwenye nyumba zao. halafu si unajua tena kamati za ufundi kwa hawa watu hazikauki.

Hivi nani aliwaza kuwaweka mawaziri pamoja kama hostel vile?

Swali zuri kweli; kwani ni nani walioamua hizo nyumba zijengwe? Kama mawaziri ambao ndiyo wahusika wakuu katika maamuzi ya kitaifa wanashindwa hata kujua mahitaji yao binafsi vipi itakua kwa vipaumbele vya taifa? Kwakweli pengine hili ni tatizo zaidi ya tatizo tunaloliona. Biblia yangu inasema mtu akitaka kazi ya uchungaji, uaskofu etc atamani jambo jema lakini inafaa mchungaji awe mtu anayeweza kuongoza nyumba yake mwenyewe... Sasa hili la kwetu linasikitisha kama hakukua na participatory approach katika kujenga hizo nyumba zakwao ni vipi wataweza kuwahusisha common people katika kuleta maendeleo wanayoyahitaji? Hii inaonyesha jinsi tulivyo na poor planning and programming. Uncoordinated development planning approach ambayo mara nyingi ni chaotic. Kila mtu anafanya anachodhani ni sahihi bila ridhaa ya wengine. Matokeo ni maendeleo yasiyokidhi haja ya watu.
 
Mawaziri wenye nyumba zao binafsi kama vile Husen Mwinyi na hao wengine, kwa nini wakaishi pale kambini?

Hata mimi ningeendelea kuishi kwangu kuliko kesho naondolewa uwaziri halafu nahamisha virago vyangu.

Hata uncle Karume kaamua aishi kwenye kasri lake na kuikacha ikulu aliyopangiwa!

karume hata baba yake alikuwa anaishi kwake..infact nyumba anayoishi karume leo alikuwa akiishi baba yake...

hussein mwinyi alikuwa akiishi kwa baba yake msasani[mikocheni]..na ndugu zake wengine...hadi majuzi alipoamia mbezi ya chini.....
 
sasa nani wanaishi kwenye hizo nyumba jamani; we have established kwamba mawaziri na manaibu wao wengi hawaishi huko. Je ziko tupu?
 
Hizo nyumba hazina hadhi hata speaker wetu alikaa hizo nyumba akasema imebidi ahame sababu maji machafu yalikuwa yanarudi ndani badala ya kwenda kwenye karo kwa hiyo hadhi yake si ya Viwango na si ajabu hayo ni matokeo ya asilimia kumi
 
Back
Top Bottom