Nyumba za kupanga uswazi/mkwara?

Makaimati

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
462
87
Hodi hodi hodi Wanajamii,

Hiki ni kisa cha kweli kimetokea huku kwetu.

Endelea kusoma tafadhali:

Kuna mama mmoja alikuwa na nyumba ya kupangisha karibu na nyumba yake alokuwa anaishi. Wapangaji wake wengi walikuwa Askari Polisi kwa sababu ilikuwa pia jirani na Kituo cha Polisi

Bahati mbaya hawa wapangaji walikuwa hawadumu kwa sababu huyu mama alikuwa anapenda kutukana tukana sana.

Akatokea Askari mmoja aliehamishiwa hapa na akitafuta nyumba ya kumtosha na familia yake kubwa. Askari wenzake wakamuelekeza kwa yule bibi huyu wakijiuliza huyu jamaa mpole sana ataweza? Pia walimueleza hio hali lakini kwa shida alokuwa nayo ikabidi aende tu

Jamaa kufika pale, yule mama akamwambia, "Baba nyumba nnayo lakini utaiweza?

Askari akauliza, "Kwanini mama?"

Mama akajieleza, "Baba mimi natukana sana, ndio ila yangu?

Askari akamwambia, "Nadhani tutawezana mama maana na mimi ila hio nnayo lakini mimi nimekuzidi kidogo"

Mama kataka kujua, Enhe kwa vipi?"

Askari akamalizia, "Na kupiga mimi napiga pia"

Askari huyo ameishi nyumba hio na kuzaa watoto watatu humo ndani na amehama mwenyewe kurudi kijijini kwao baada ya kustaafu kazi hivi karibuni.

Mkwara unafaa jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom