Nyumba za Diwani CCM zachomwa moto

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
DIWANI wa Kata ya Idetemya wilayani Geita, Juma Nyembe Machibya (49) wa CCM amepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 51 baada ya wananchi wa kijiji cha Nyabulanda kumvamia na kuteketeza kwa moto nyumba zake nne za bati na mali nyingine kufuatia mgogoro wa eneo la kujenga makao makuu ya kata.

Mali nyingine zilizoteketezwa na wananchi hayo ni pamoja na baiskeli tano, mahindi, mpunga, pikipiki, kuku 21, kondoo mmoja na pesa taslimu, sh milioni 1.6.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Mugeta Jandwa alisema , tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4.54 asubuhi katika kijiji cha Nyabulanda wilayani Geita.

Alisema, sababu ya kuteketezwa kwa mali za Diwani huyo ni wananchi wa kijiji cha Idetemya na Nyabulanda kugombea makao makuu ya ya kata yajengwe katika kijiji cha Nyabulanda.

Jandwa alisema, jeshi la polisi linawasaka wananchi waliohusika na tukio hilo ambapo upelelezi ukikamilika watafikishwa kwenye mikono ya sheria kwa hatua zaidi.

Aidha, Jandwa alisema siku hiyo ya tukio majira ya saa 9 mchana wananchi wa kijiji cha Nyabulanda walimjeruhi kwa mawe kichwani Mkuu wa kituo cha polisi Nyangw’ale E. 2534 Koplo Masunga (43) baada ya kutega mawe barabarani.

Mkuu huyo wa kituo alikutwa na zahma hiyo akiwa na Inspekta Barige wakati wakitoka kuwakamata watuhumiwa wa kosa la kutishia kuua kwa maneno katika kijiji hicho ambapo walitega mawe barabarani na waliposimama ndio wananchi walipoanza kumrushia mawe na kumpata kichwani.

Jandwa aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za kumtishia kumuua Diwani huyo kuwa ni pamoja na Medai Fungame (28), Masumbuko Pius (37) na Stephano Malimi (61).

Hata hivyo alisema hali ya Masunga inaendelea vizuri na kwamba polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio ili hatua zaidia za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa waliohusika.
 
Nawapa Pole sana Mh Diwani na Afande kwa masahibu yaliyowapata...
Haya yote ni kutokana na Ugonjwa wa Uongozi legelege, ugonjwa huo upo mpk ngazi za chini!

Waathirika wa hilo tukio ni imani yangu wakipitisha kikapu cha msaada Mjengoni kwa Walipukaji watawasaidia kutoka ktk posho zao, kama alivyowahi kunukuliwa Kiongozi Mkuu wa walipukaji mjengoni, alipo comment khs Posho!
 
Wananchi wanazidi kugain confidence taratibu kwa sababu ya viongozi wasiojua wajibu wao.Ipo siku watampopoa kiongozi mkubwa zaidi hawa wadogowadogo kama mambo yataendelea hivihivi.
 
Wananchi wanazidi kugain confidence taratibu kwa sababu ya viongozi wasiojua wajibu wao.Ipo siku watampopoa kiongozi mkubwa zaidi hawa wadogowadogo kama mambo yataendelea hivihivi.

Well said!! Lkn umesahau JK alipopolewa Chunya??
 
Poleni sana waathirika. Lakini si walisema TZ kuna amani?
 
Wananchi wanazidi kugain confidence taratibu kwa sababu ya viongozi wasiojua wajibu wao.Ipo siku watampopoa kiongozi mkubwa zaidi hawa wadogowadogo kama mambo yataendelea hivihivi.
<br />
<br />

Mkuu ushasahu wananchi waliwahi kumpopoa kwa mawe Vasco da Gama kule Mbeya?

Sema ipo siku wananchi wataipopoa Magogoni
 
jamani wana geita hasira hiyo wangekuwa nayo siku za nyuma huenda madini yao yangekuwa na maana kwao, kuliko ilivyo sasa ambavyo wanaachiwa mashimo na umasikini wa kupindukia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom