Nyumba ya kiongozi wa CCM Igunga yachomwa Moto

nyumba yenyewe ukiiona kwa ccm ni aibu wakisema wameleta maeendeleo.......... ni ya udongo kibanda cha kuku ...hio laki mukama angemjenge kibanda kingine cha elfu 50
 
MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: "Chadema sisi ni wajanja".Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.

Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

"Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa," alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Mukama alaani
Akizungumzia tukio hilo, Mukama amesema alisema ni lazima lilaaniwe na kila Mtanzania mpenda amani wakiwamo wananchi wa Igunga na akavitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawasaka na kuwakamata waliohusika.

"Ni lazima lilaaniwe kwa sababu halitoi taswira na maana halisi ya kuwa na vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana kwa ubora na sera… hatushindani kwa vitisho, uhuni na hata kumwagiana tindikali," alisema.

Alisema ameshangazwa na mwenendo wa Chadema kuendesha siasa za chuki hususan katika Jimbo la Igunga na kutoa mfano wa Kenya ambako vyama vingi ni vya kikabila lakini hakuna matukio ya aina hiyo.

Alitumia fursa hiyo kupiga kampeni akisema matukio yanayotokea Igunga hivi sasa yanawasaidia Watanzania kukielewa Chadema ni chama cha aina gani na kuwataka Wana-Igunga kukiadhibu hicho kwa kukinyima kura Oktoba 2 ,mwaka huu.

"Demokrasia haiwezi kuanishwa kwa matukio ya kihuni na wale wanaotaka kuipa demokrasia taswira ya hovyo ni lazima waadhibiwe. Njia pekee ya kuwaadhibu watu wa aina hiyo ni kuwanyima kura," alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpa kiongozi huyo msaada wa Sh100,000 ili azitumie kuirejesha nyumba hiyo katika hali iliyokuwapo kabla ya tukio.

CUF waungana na CCM

Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nyandekwa, Emmanuel Ezekiel ambaye alifika eneo la tukio mata tu baada ya Mkama na msafara wake kufika, alisema tukio hilo ni la kihuni na linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

"Unajua kwenye mji unaweza kuwa na watoto watatu wa baba mmoja, mama mmoja lakini akatokea mmoja akawa kichaa msipomdhibiti atawaharibia ule mji," alisema Ezekiel bila kufafanua kauli yake hiyo.

Mwenyekiti huyo alitahadharisha kuwa kampeni katika Jimbo hilo la Igunga ni za mwezi mmoja tu lakini, kama zisipofanyika kwa ustaarabu zinaweza kuzaa uhasama utakaodumu kwa miaka mingi.

Polisi wanena

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kutoka makao makuu ya Polisi, Naibu Kamishna, Isaya Mngullu alisema polisi wanaendelea na upelelezi.

"Ni kweli hilo tukio lipo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana (juzi) na sisi tumeanzisha upelelezi, nipeni muda tukusanye taarifa halafu nitawaita (waandishi) niwapeni taarifa kamili," alisema Mngullu.

Chadema waruka
Lakini Kamanda wa Operesheni za Kampeni wa Chadema, Benson Kijaila jana alikanusha chama chake kuhusika na tukio hilo na kukigeuzia kibao CCM kuwa wao ndicho kilichoshiriki katika tukio hilo.

"Matukio haya wanayapanga wao wenyewe halafu wanasingizia vijana wetu… kama ni kuchoma hiyo nyumba wameichoma wenyewe ni mpango wao huo," alisema.

Kamanda huyo alisema hata tuhuma za tindikali zinazoelekezwa kwa Chadema ni mipango iliyosukwa na CCM na kwamba kama ni watu wenye tindikali, basi CCM ndiyo walionazo.

Tukio hilo la juzi la kuchomwa moto nyumba ya kada huyo wa CCM ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayotokea Igunga na wakati wote, matukio hayo yamehusishwa na wafuasi wa Chadema.

Mwanzoni mwa wiki hii, wabunge wawili na kada mmoja wa chama hicho walishtakiwa mahakamani kwa makosa manne likiwamo la kumdhalilisha na kumwibia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.

Septemba 9 mwaka huu, kijana mmoja anayedaiwa ni mwanachama wa CCM, Mussa Tesha (25) alimwagiwa tindikali usoni na watu anaodai kuwatambua kuwa ni wanachama wa Chadema.

SOURCE: Mwananchi

kazi kwelikweli, democrasia inakaribia ila bado
 
Utabiri umekamilika -- Yaani imefikia CCM wanahaha kulikomboa jimbo kwa kila aina ya mbinu, nguvu inayotumika ni kubwa kuliko maelezo, mbaya zaidi mbinu zingine ni za kitoto zaidi. kweli yamewafika shingoni ila wazee walishasema mshahara wa dhambi ni MAUTI, na huwezi kumfanya mwenzako zuzu all the time, watu wameshawastukia. sasa mauti yenu yanatimia - mpo ICU mkipigania roho isitoke.

Tutasikia mengi as days approching 0 to election day.
 
CCM wameishiwa mbinu za kampeni sasa wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi.
Kama kweli chadema wanahusika kufanya tukio hilo kwanini waache karatasi hapo!
Na kama suala ni kuchoma nyumba kwanini chadema wachome jiko badala ya nyumba anayolala huyo kiongozi!
Hizi siasa uchwara, ambazo hazina budi kupigwa vita na wapenda maendeleo wa Igunga kupitia sanduku la kura!
Mpaka sasa naona ccm hawajagundua kuwa mbinu wanazozitumia zinazidi kuwaharibia!
HAKI HAIJAWAHI KUSHINDWA HATA SIKU MOJA!

mchawi huwa hajitangazi hata siku moja brother
 
kama sept 11, passport ilipeperuka na ikaokotwa ikiwa salama salmin, mazingaombwe haya, kisha wao wanaondoka wanawaacha wana igunga na chuki na kutoelewana.
Eti mtu kachomewa nyumba akashindwa kuuzima moto akaenda kulala akauacha moto unawaka kesho yake akakuta karatasi kwenye hiyo hiyo nyumba ambayo moto wake alishindwa kuuzima inamtaja aliyechoma, hii inaingia akilini kweli? Hizi cheap politics CCM wameingia choo cha kike zinawashusha badala ya kuwapandisha.
 
Watu wengi hapa mnatumia uelewa wenu mkubwa kutoa reasoning kwa tendo hili....lakini je mmejivika uhusika wa watu wengi wa vijijini(hasa wakinamama) wa igunga jinsi wanavyofikiria.wao si kama ninyi.kwa mbinu hii nyepesi,inatosha kuwahadaa juu ya ujanja wa ccm.CDM inahitaji kaz ya ziada kuwaelewesha kina mama hawa ambao kwao dhiki ni sehemu ya maisha yao
 
Eti CHADEMA wamekuwa AL-KAIDA ama AL-SHABAB mpaka wajitangaze kuhusika kwenye milipuko.
What ludicrous and grim!!!!!
Mkitaka kudanganya jaribuni kutumia akili.
 
Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

"Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa," alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

SOURCE: Mwananchi

hata kuanalyse matukio wanashindwa?
Mtu nyumba yake imeungua, amewaita majirani wamezima moto lakini umewashinda kuzima na kuku wake wameungulia humo. Nyuma nzima, cha thamani ni kuku?

Achana na hilo mwana JF, soma hapo bolded-green.

Inawezekana vipi nyumba iungue, uuzime moto ukushinde halafu uamue kulala?
Inaonekana jamaa haunguii nini?
UTATA MTUPU
 
Matukio hayo ni mojawapo ya mafunzo ya kigaidi walifundishwa kufanya hao Greengard walipokuwa mafichoni Singida. Tunashukuru kwamba CDM tayari wameshashitukia njama zote zinazofanywa na CCM. Ila tahadhari polisi Igunga wasijidanganye kula cha juu ( pesa za CCM ) ili kuwakamata na kuwanyanyasa wafuasi au viongozi wa CDM kwa sababu ya ujinga wa CCM, patachimbika.
 
watu wengi hapa mnatumia uelewa wenu mkubwa kutoa reasoning kwa tendo hili....lakini je mmejivika uhusika wa watu wengi wa vijijini(hasa wakinamama) wa igunga jinsi wanavyofikiria.wao si kama ninyi.kwa mbinu hii nyepesi,inatosha kuwahadaa juu ya ujanja wa ccm.cdm inahitaji kaz ya ziada kuwaelewesha kina mama hawa ambao kwao dhiki ni sehemu ya maisha yao

ni kosa kubwa sana kwenda field na kuwachukulia respondents wako hawajui
 
du kifo kweli hakina huruma.ccm wameamua kufa kifo cha tukose wote.hata watoto uliowazaa unaamua kuwaua kisa wewe unkufa?
ccm mungu amenichagua katika wengi kushuhudia kifo chako.nyerere alitabiri,kolimba akatabiri ila hawakupata fursa ya kushuhudia ila mimi nitashuhudia.
 
Eti mtu kachomewa nyumba akashindwa kuuzima moto akaenda kulala akauacha moto unawaka kesho yake akakuta karatasi kwenye hiyo hiyo nyumba ambayo moto wake alishindwa kuuzima inamtaja aliyechoma, hii inaingia akilini kweli? Hizi cheap politics CCM wameingia choo cha kike zinawashusha badala ya kuwapandisha.

ni afadhali mwanaume aingie choo cha kike kuliko mwanamke kuingia choo cha kiume, kukojoa utakuwa muziki wa maana.
 
Jamaa kapata faida!
Bei ya kuku igunga ni elfu 3, kuku 15 ni shilingi 45000, banda la kuku ni sh 30000 'kujenga. Kwahiyo garama zote ni 75,000 amebaki na faida shillingi 25,000:

Kitu cha pili ni kwamba, huyo mwandishi wa hiyo habari ni mwana mapinduzi wa kweli, kwa kuwa alilazimishwa na mazingira ya ajira zetu hizi za kibongo, akaamua awalipue kwa dizaini hiyo!
Big up mkuu, Great thinkers tumekupata vilivyo!
 
Hata CUF wanasema aliyechomewa nyumba ni kada wao na Katibu wao wa Kata. Nani mkweli?
 
Jamaa kapata faida!
Bei ya kuku igunga ni elfu 3, kuku 15 ni shilingi 45000, banda la kuku ni sh 30000 'kujenga. Kwahiyo garama zote ni 75,000 amebaki na faida shillingi 25,000:

Kitu cha pili ni kwamba, huyo mwandishi wa hiyo habari ni mwana mapinduzi wa kweli, kwa kuwa alilazimishwa na mazingira ya ajira zetu hizi za kibongo, akaamua awalipue kwa dizaini hiyo!
Big up mkuu, Great thinkers tumekupata vilivyo!

kwani kilichoungua ni nyumba ya kulala au banda la kuku? utata mwingine huu
 
Back
Top Bottom